Master PLan ya Mji mpya wa Singapore

Master PLan ya Mji mpya wa Singapore

Hata sielewi kilichowavutia ktk master plan ya Singapore kwasababu kwenye dunia ya kwanza hicho ni kitu cha kawaida yaani safari zote mnazochoma pesa za walala hoi kwa kutembea kundi kubwa mmejifunza master plan! Hivi hatuna architecture engineer tanzania? Nafikiri tatizo ni serikali isiyokuwa na mipango, ufisadi na uvivu wa kujituma, nchi inazalisha wasomi kibao kwenye kilimo Lakini watu wanakufa njaa hili nalo tunataka watu waje kutufundisha kulima! Ni kitu gani tunachoweza Kama watanzania? Gossip na ngonjera, tanzania itajengwa na sisi watanzania, Hakuna nchi duniani iliyojengwa na wageni.

..."yaani safari zote mnazochoma pesa
za walala hoi kwa kutembea kundi kubwa"...mkuu umenena haswa...
...safari za viongozi wa TZ nje ya nchi imekuwa kero kubwa kwa walipa kodi..., na habari za uhakika mwezi huu wa sita mama huyu, atakwenda Uingereza kwa ziara ya kikazi, pia rais JK ATAKUWA NA ZIARA huko huko Uingereza, na kufuatiwa ziara ya Makamu wake G. Bilal, na baadaye WIZIRI MKUU Mizengo Kayanza Peter Pinda !
...huu ni ufujaji wa kodi za wananchi.... "wakirudi wanakuja na Master Plan nyingine ya miji mipya"
 
Mbona mlishafanya huo mpango angalia hapa kwenye link (Kigamboni New City) au mnataka kupiga hela nyingine za ili mtutengenezee video nyingine?

Hapo umenena kiongozi. Huyu Prof angeweka sawa hiyo ziara yake na Mhe ilikuwa na malengo gani na suala la Kigamboni limeingiaje ilhal tunajua wazi kuwa mpango wao wa kulazimisha uendelezaji wa Kigamboni ni wa siku nyingi na umeghubikwa na sintofahamu nyingi sana. Msaada ambao Prof ameomba kwa Wasingapore ni wa nini hasa ama anataka kuudanganya umma kwa hizo picha walizopiga huko ili watanzania waamini kuwa sasa Kigamboni itang'aa kama Singapore.

Ni vyema akatambua kuwa hao wenzetu mipango yao ni ya miaka hamsini hadi mia moja ijayo na siyo kama ya akina Prof inayojikita kwenye awamu ya uongozi (miaka 5-10 ) na kuangalia ilani ya chama inayoandaliwa na wanasiasa ili kukidhi matakwa yao binafsi

Cha msingi ni akina Prof na mkuu wake wajue wazi kuwa wenzetu hawaonei aibu wala rushwa, hawafichi wahalifu, wezi na wabadhirifu wa mali ya umma kwenye ikulu ya nchi kwa kuogopa kuwa nchi itatikisika na kuwa kwao sharia ni mwongozo wa kila kitu na haibagui ama kuangalia huyu ni nani na ana uhusiano gani na watawala hususan mkuu wa nchi na wengineo
 
Umesema kupanga ni kuchagua. Tanzania ina zaidi ya wakaazi milioni 45. Zaidi ya milioni 20 kati ya hao wanaishi mijini, au pembezoni mwa miji na kati ya hao, zaidi ya 90% wanaishi maeneo ambayo hayana mipango miji wala makazi yao hayajapimwa.
Ni aibu kwa nchi yenye viongozi na wasomi kuwa wanaongelea Kigamboni miaka nenda rudi, eneo ambalo halitaishi zaidi ya watu laki tano. Hivi inagharimu bilioni ngapi kutengeza karamani kama hako ulikoweka kwenye picha?
Ramani ya Kigambini ipo, na hata kama haitajengwa leo, tunajua kuwa itajengwa tu, hata miaka 50 ijayo.

Mh Waziri nakuomba kwa heshima na taadhima, angalau kwa muda uliobaki nao kuongoza wizara hiyo, tutengenezee mipango miji ya miji hata 20 tu hapa Tanzania. Najua hii nchi ina zaidi ya 'miji' 100, lakini naomba angalau target miji 20. Hizo ramani ziwepo mahali fulani, ili hata baadae wakija viongozi wengine wakute kuna "kazi" ya kufanya. Hii nchi hadi sasa haina dira, na kila kiongozi akija anafanya anavyojisikia kwa sababu haina master plans.
Kwenye hizi nchi zilizoendelea, si ajabu ukakutana na 'pori', kumbe sio pori, ni mji mkubwa tu 'uliojengwa' miaka 40 iliyopita, ila ujenzi wake bado upo katika stage ya kwenye 'karatasi'. Hapo hata aje kiongozi 'nabii', hawezi kubadilisha; ama anajenga, au anapaacha palivyo.
Ingawa kwa sasa pengine hatuna hela za kujenga, lakini hata za kupanga na kuchora hatuna?!!!

Umenena vyema. Katika hiyo miji ishirini Lindi isikosekane. Hata bahari kama ya kigamboni ipo
 
Mimi shida yangu ni hilo neno kutusaidia, sitaki hata kulisikia kwanza ikiwezekana hata tulifute kwenye Lugha yetu, liwe halipo na mtu akilitumia atozwe faini kubwa aua aende Jela!

Kwa nini watusaidie? Kwangu mimi hata kama huo ukichukua miaka 50 kujengwa na iwe hivyo lkn ujengwe na sisi kwa nguvu zetu sisi wenyewe bila mkono wa takataka yoyote kutoka nje, ili miaka 200 baadae tuje kusema tuliujenga huu mji na sio ulijengwa na sijui na wahandisi wa kutoka Singapore, hilo silitaki!
 
Kwanza nikupongeze kwa kuleta mjadala huu hapa kwenye hili jamvi..
Lakini nataka nikuambie jambo moja, Tanzania inayumbishwa na wanasiasa.. porojo zimezidi kuliko utaalamu na utendaji. Utashangaa ukiingia kwenye halmashauri za miji yetu hao wanaoitwa "mipango miji" hawana upeo (exposure) kulingana na kasi ya mabadiliko na teknolojia ya kidunia zaidi ya theory walizosoma vyuoni/darasani.

Pili mahali pengi wanasiasa wamekuwa kikwazo kwa uboreshaji wa miji yetu kwa kisingizio cha kulinda wapiga kura wake.. hatuwezi kufika mama kwa staili hii. Mimi ninashauri kiundwe chombo cha kusimamia na kupanga miji yetu ili kuepukana na ujenzi holela, kiwe na mamlaka ya kuingia kwenye halmashauri zetu na kupitia master plan zilizoko na kutoa mwongozo huku wadau wote wakishirikishwa.
 
Sisi hatuna shida na mipango ipo mizuri tatizo MA CCM YAMEKUWA MAJIZI SANA
 
WanaJF

Kupanga ni kuchagua. Kunahitaji nidhamu na hakuna mchezo wala utani. Huwezi kuwa na mji uliopangwa kama unapenda na kuendekeza uholela na vurugu (chaos). Kinachotakiwa ni kushirikisha wadau wote kupanga malengo na viwango baada ya kupata maoni ya wataalam. Wanaoarithirika na kulazimisha kuhama kupisha maendelezo mapya wanalipw fidia stahiki na endelevu.

Anayedai vinginevyo si msema kweli. WaSingapore wamehaidi kutusaidia katika ujenzi wa Mji Mpya wa Kigamboni. Ninakaribisha maoni yenu hasa nyie mlio nje na mnaishi katika miji iliyopangwa? Je uholela unavumiliwa au kuendekezwa? Tupe habari.


Mama Tibaijuka

Mama,
Nyie kama serikali mmejipanga vipi sasa? Maana hujatueleza katika post hii.....karibu Kwa Mtogole(najua hujawahi kufika) uone hizo "chaos" ambazo in part serikali ni ya kulaumu
 
Dar ilikosewa kitamba sana katika mambo ya ujenzi hivyo kuna haja ya kuona na mpangilio mzuri kwa kigamboni na vipi mpango wa treni za kasi huko kigamboni
 
Asante Mama Tibaijuka, endelea na mipango na pia fanya hivyo hivyo nenda sehemu zilizoendelea ujifunze siri na maarifa ya, nina imani kubwa kwako.
 
Mh, Mb Waziri mama Prof Anna Tibaijuka
Nami pia nikupongeze kwa angalau kuleta hili hapa jamvini, ingawa yaweza kuwa na zaidi ya wengi tunavyo ona! ( maana profesorial eyes has a lot sights). hilo nakuachia.
Naomba niweke maswali nami machache, japo yaweza fanana na wengine walio tangulia
i) Kwanini miji inayo kua kwa kasi haijafanyiwa utaratibu wa kuwekewa master plan? tunasubiri nini? au lini zitakuwa tayari?
ii) kwanini hatuweki miundombinu hata pale serikali imepima na ikauza(tena bei ya juu)? maeneo yanauzwa yanabaki mapori sababu ya ukosefu wa miundo mbinu, je sababu ya kupima inatimizwa kikamilifu?
iii) Hiyo master plan ya Singapore, itatimizwa na serikali, (municipal), Real Estates au individual? na nini mamlaka ya mji kwenye kuitimiza hiyo Master Plan ya mji mpya?
iii) Kwanini serikali inaanzisha benki kwa 100 billion (single benki) kwa nini isianzishe kamapuni ya Real estate? kwa mtaji huo na ikaenda kwenye stock market kupata mtaji zaidi?
iv) kwa nini halmashauri/ Manispaa zetu hazina master plan? na kama zipo kuna sehemu ya nchi hii unaweza kutoa mfano?
Mwisho tatizo tumeruhusu watu wajenge, watu wanajenga kulingana na uwezo wao, usimamizi wa ardhi ni mbovu, sheria za ardhi ama hazifafanuliwi au hazisimamiwi kikamilifu. mwisho wa suluhisho ni serikali kuweza kujenga makazi, na kuwataka wenye uwezo wa kujenga wajenge kulingana na mpango wa serikali. Ni hayo tu kwa sasa.
Asante.
NB: Waziri njoo ujibu mama, yamekuwa mengi sana tangu mwanzo naangalia sioni jibu lako.
 
Umenena vyema. Katika hiyo miji ishirini Lindi isikosekane. Hata bahari kama ya kigamboni ipo

Haya mkuu. Ila inasemekana the next (baada ya Bagamoyo), ni kwetu Chalinze...
 
Daha napata wakati mgumu kukujibu kwani hata mimi sijui hatima ya hii kitu kinaitwa makao makuu ya Nchii inamaana kikija chama kingine kinaweza kikaamua makao makuu yawe LINDI!
Mkuu niliona master plan ya CCM na vitega uchumi kibao huku wakiwa hawana mpango wa kuhamishia makao makuu ya Srikali Dodoma.Kikija chama kingine natumai wanaweza kuifanya kazi hii ndani ya miaka miwili tu kama nia ipo.
 
Mama Tibaijuka,
Tukubali kuwa tulibugi huko nyuma. Lakini it is never too late to improve.

Hivi, how much is needed kuwa na Grand Master Plan ya nchi nzima? At least general tu yenye vitu muhimu vya kuanzia na si lazima iwe too detailed. Hii inaweza kuwa kama blueprint kwa detailed masterplans za baadae kwenye miji hata vijiji na hivyo nchi yetu kuwa ya kisasa zaidi kwa vizazi vijavyo maana sio lazima tufaidi sisi wa sasa.

Hili ni wazo langu
 
Mheshimiwa nadhani kabla wananchi hawajakupa maoni yao ni busara kama ungejibu maswali mengi yaliyoulizwa hapa hususani kuhusu mpango wa Kigamboni. Vile vile wewe ukiwa Waziri una wajibu wa kutoa majibu kwa maswali mbali mbali yanayosumbua vichwa vya Watanzania wengi hususani kuhusu maeneo mengi yaliyooneshwa kuwa ni ya wazi ambayo yamechukuliwa na vibopa wachache walioweka serikali mikononi mwao. Unadhani mmeitendea jamii ya watanzania haki kwa kufanya open space kuwa occupied spaces na kubadilishwa matumizi ya ardhi?
Kama kweli Kupanga ni kuchagua, Kunahitaji nidhamu na hakuna mchezo wala utani kama ulivyosema, unadhani ni sawa hicho kilichofanyika hapo Bibi Titi hayo majengo mawili yaliyonyanyuliwa juzi juzi Viva Towers na Uhuru Heights kuingilia sehemu ya barabara na kuchafua mandhari ya mji?
Ramani halisi ya mipango miji hususan Dar es Salaam mpaka leo imefwatishwa kwa kiasi gani? Ni jambo la busara kutoa majibu na ripoti ya maendeleo ya wizara yako tangu ulipoingia kwa kasi mpya na ari mpya mpaka sasa.
Wasalaaaam
 
Mama Proffesor Anna Tibaijuka,Salaamu.Ninafurahi kuona kwamba umetuonyesha kwamba hata nyie Viongozi wa Nchi hii huwa mnatamani Maendeleo ya Wenzetu wa huko nje.Kila siku huwa najiuliza sana na sipati jibu,kwamba ni kwanini Viongozi wengi wametembelea na wameishi sehemu nyingi duniani,na wanashindwa kuwa na uchungu ama tamaa ya kufanya miji yetu iwe mizuri kama ile ile ya wenzetu....

kuna vitu vingine ambavyo kwa kweli havihitaji gharama kubwa zaidi ya "kuwahubiria na kuwaelewesha wananchi" ili waweze kutoa Ushirikiano katika kusaidia Kampeni za kupendezesha majiji yetu....Hivi majuzi nilikuwa safari ya Kikazi Egypt....Kwa kweli Mama Anna,kwa mara ya kwanza niliweza kuamini ule msemo wa Wahenga usemao "Penye Miti hakuna Wajenzi".....Hivi unaweza kuamini kwamba ukifika katika jiji la Cairo,ambalo joto lake ni karibia centigrade 40,jiji lile ni "Green greeen!!" zaidi ya Dar Es Salaam?.....

Yaani pamoja na jangwa lote walilonalo,wameweza kuyatumia vema maji waliyonayo ili kuweza kuufanya mji uwe Green!,.....tena Summer hiyo...Kwa kweli nilipatwa na "Wivu wa Ki maendeleo " hadi nikaamua kuwauliza wenyeji ni namna gani kwamba mji wao ni Green,wakati kuna joto la ajabu....Wao walicheka,na wakaniambia kwamba "Kila nyumba inathamini sana miti,na tunamwagilia miti yetu karibu kila siku,hata kama maji ni ya shida!!1"....na pia wakaniambia tokea shuleni wanafundishwa tabia kama hiyo!!......Kwa kweli niliumia sana na kujisemeea

"Hivi hawa Viongozi wetu wa Tanzania huwa hawaoni hii hali ya hapa Cairo na wao kufikiria kuhusu upandaji wa Miti katika Viunga vya Miji yetu?"Tukija kwenye suala lako la hiyo Master plan,ninakuelewa kwamba "take home" ama "message sent" yako uliyotaka tuipate ni kutaka kutueleza kwamba "Mambo mazuri yanahitaji Mipango shirikishi kati ya Serikali na Wananchi"...na kwamba Mambo mazuri always yana implications zake kama vile Watu ku be displaced,Serikali kuingia gharama kubwa,na pia kuwepo na Upinzani mkubwa wa suala lolote lile la kuleta Maendeleo kutokana na mchanganyiko wa "Wataka mema ya Nchi" na "Wanaojitakia mema yao binafsi"...Ninaamini kwamba Viongozi wetu hivi sasa kila uchao wanazidi kuwa na "muono mpya" wa Maendeleo.....ukichangia na nguvu za Kelele za wananchi now a days katika kutaka mambo yaende sawa,nina Imani kwamba Tanzania tuitakayo inakuja.....

Wasiwasi wangu ni kwamba Wizara mbalimbali hazifanyi Kazi "kwa same mapigo"....Hivyo basi Area mojawapo ya Maendeleo inakwenda mbele wakati nyingine ina "Lag behind"....na mwisho wa siku Maendeleo ya Nchi ni Wastani wa Maendeleo ya "Sphere"(mambo yanayosimamiwa na Wizara mbalimbali) zote za maendeleo za Nchi.....I mean Wewe katika Wizara yako unaweza kuwa na Mipango mizuri sana,lakini kama katika Wizara nyinginezo mambo yako Ovyo....basi Kasheshe zetu hazitaisha hata siku moja!!!.....Watanzania tunatakiwa tufundishwe na tusaidiwe kuzalisha Mali....tuzalishe Mali in Excess ili tupate ziada ya Kuuza nje na tuweze kupata Fedha za Kigeni....

Watanzania tusitegemee sana kupata Fedha za Kigeni kutoka kwenye mambo kama Madini ama vitu vya ki bahati bahati tu.....Kama tutaendelea kutumia tu kwa kufanya huduma na kutaka tupate mishahara.,then nani atazalisha?Tunatakiwa tuelekezwe uzalendo wa kutufanya tujue kwamba tufanye Kazi kwa bidii...tufanye Kazi!!......Wananchi ni lazima tuelimishwe kwamba "Watanzania bado tuna safari ndefu sana ili kuweza kuweka mambo mazuri...na sio Kizazi chetu ndiyo kitakachofaidi,bali ni Vizazi vijavyo"....Kuna Vizazi huko nyuma vilishakosea!.....Vilikosea!...

Wakati wenzao wa Nchi zilizoendelea walikuwa wanafanya mambo makubwa,Wao walikuwa wanaishi tu....na Sasa ni Zamu yetu kuelewa "huu sio muda wa Kufaidi,bali ni muda wa Kuzalisha mali....kutengeneza mitambo ili tuweze kuendelea"Watanzania siku hizi wanabisha kila kitu....Wao wanataka haki tu...ukiwaambia wawajibike wanasema ati "Unawaonea"...wanasema ati"wao wanajua sheria za kuwafanya wasiwajibike"!!!!!Watu wanapinga kila kitu cha Maendeleo(ni kama ndivyo ilivyo yaani")Haya yote yanatokana na kwamba Watu wamejawa na wasiwasi wa "kuliwa"....

Viongozi muelewe kwamba "Watu wetu tuna wasiwasi sana na nyie kwamba mmekaa huko juu mnakula tu"Tunaomba muanze kufanya Kazi na kuwa wakweli...ninyi ndio mlioshikilia makali......hela yote ya nchi hiii iko mikononi mwenu...na mnajua kabisa "Money is the exchange medium used in Trade"......hata tukifanya Kazi,lakini nyie mkawa mnakula hizo hela......tutaendelea kuonana wabaya....
 
Ili tuondokane na miji holela
lazima kuwepo na nyumba za bei nafuu
watu wawe discouraged kujenga wawe encouraged kununua au kukopeshwa cheap houses..

na serikali iache kupimia watu viwanja,badala yake ipimie makampuni maeneo yajenge nyumba kwa wingi...
 
Mbona mlishafanya huo mpango angalia hapa kwenye link (Kigamboni New City) au mnataka kupiga hela nyingine za ili mtutengenezee video nyingine?

Hivi ni lazima ukurupuke bila kusoma?

Ni wapi Anna amesema wa Singapore watakuja kufanya "mpango" wa Kigamboni, amesema "WaSingapore wamehaidi kutusaidia katika ujenzi wa Mji Mpya wa Kigamboni".

Si lazima upinge hata visivyo pingika, unafikiri hii miji wanakaa CCM pekee? au unafikiri Mawaziri hawa wako pale kwa kuwatumikia wana CCM pekee? Kama huna jibu, waulize wabunge wako wa magwanda huwa wanafanya kazi kwa wote au la!
 
Ili tuondokane na miji holela
lazima kuwepo na nyumba za bei nafuu
watu wawe discouraged kujenga wawe encouraged kununua au kukopeshwa cheap houses..

na serikali iache kupimia watu viwanja,badala yake ipimie makampuni maeneo yajenge nyumba kwa wingi...

Makes a lot of sense "real estate developers".

Itafanya hata "quality" na "standard" za nyumba na miundo mbinu ziwe bora.
 
Mji wa Dar tayari haupo katika mpangilio mzuri (poorly planned or not planned at all). Vibarabara vimejifinya sana na hakuna planned streets, matokeo yake tunapopata mfadhili tunakurupuka kuwabomelea wananchi majengo yao kwaajili ya upanuzi wa barabara. Kwanini tunapo-plan tusi-focus miaka kadhaa mbele kutakuwaje. Sasa basi huko mikoani nako hatutaki kujifunza kutokana na adha inayotokea Dar, bado tunaplan vibarabara vilivyojifinya matokeo yake hapo baadae tutaendelea na bomoabomoa nako huko mikoani. Nashauri waziri tujifunze kutoka Dar, ili huko mikoani tusijekuwa na tatizo kama la Dar. Kupanga ni kuchagua, chagua sasa.
 
Back
Top Bottom