Master PLan ya Mji mpya wa Singapore

Master PLan ya Mji mpya wa Singapore

Mkuu Dr F. Ndugulile una maoni gani hapa?
Mji mpya wa kigamboni unajengwa na Wasingapore?



attachment.php
 
Last edited by a moderator:
Kwanza ninategemea sana mchango wa ndugu yetu @Dr F.Ndugulile kwa kuwa mradi wa kigamboni umetajwa humu.Natumai kwamba kutokana na mchango wa huyu bwana tutapata point ya msingi ya kurejea.Tena nakumbuka wakati waziri anawasilisha bajeti yake, Ndugulile alionekana kutoridhika na akawa anataka kutoa taarifa ila Spika akamzuia.Huu ndio wakati wako ndugu Faustine ndugulile.

Tukirudi kwenye mada; Mimi ningeomba tu kufahamu mambo kadhaa ya msingi kutoka kwa waziri.

1. Ni kwanini Miji ya tanzania hasa Dar es salaam haina mpangilio ukilinganisha na miji mingine Mfano tu hata mji jirani kabisa Nairobi? (kujua tatizo ni nusu ya kulitatua.)


2. Ni kwa nini hata sasa , makazi mapya yanaendelea kujengwa katika ardhi ambazo hazijapimwa mfano Chanika?


3.Ni kwa nini serikali Haiajiri wahitimu wa taaluma ya ramani na upimaji wa kutosha ili kuiwezesha miji inayojengwa kuanzia sasa iwe ya kuwango kwa kuwa mwanzo tulishakosea? Ikumbukwe wapo wataalam wanahitimu kila leo na hawana ajira!

Ni hayo tu kwa sasa.
 
Hivi Mama Tibaijuka_kale kajengo ka gorofa 6 ulikoamuru kavunjwe kweli kamevunjwa....?...just curiuos to know.
 
Pole na kazi mama Tiba, lakini pia si vibaya ukajibu tuhuma zifuatazo kuondoa wingu juu ya mradi huu, Mnamo tarehe 7/December 2012 inasadikika wewe mheshimiwa waziri ulisafiri kwenda nchini Thailand ambako ulikutana na wakuu wa kampuni kutoka China kusaini mkataba wa ujenzi wa mji kisasa wa Kigamboni. Mheshimiwa kwa mujibu wa vyanzo mhimu wewe utapata 3% kama aksante kutoka kwenye kampuni hii kutoka nchini china?

Pia kuna lawama kutoka kwa wadau wakuu ikiwemo wabunge na madiwani ambao ni wawakirishi wa wananchi hukuwashirikisha katika maamuzi juu ya mkataba huu na mradi kwa ujumla.

Mwisho tungependa kujua ni lini zabuni ya ujenzi wa mji wa kigamboni ilitangazwa kwa mujibu wa Public Procurement Regularity Authority-PPRA, ni kwa kupitia mtandao gani au gazeti gani la hapa nchini au nje ya nchi ilitangazwa (International Competitive Procurement-ICP) ili tujirishe kuwa kulikuwa na uwazi katika diri hili. kwa mujibu wa PPRA thamani ya mradi huo hauwezi kuwa Single source au International shoping. Tunaomba kujua sisi wananchi wa kawaida.
 
Mkuu Anna Tibaijuka nasapoti hoja yako ila kwa mawazo tofauti!

Suala la masterplan ni suala la serikali inajenga ama property developer? Ukiangalia picha hapo chini ni mji wa mwanza, watu wanakimbilia milimani na matokeo yake miundombinu inakuwa shida kuwafikia na kuongeza makazi holela.

Ninachoomba suala la upimaji wa ardhi ipewe sekta binafsi na serikali ibaki kuwa wasimamizi wa zoning. Sababu kubwa ni urasimu uliopo serikalini..viwanja vikipimwa mwaka huu mnaweza kukaa hadi miaka 3 hamjui nini hatma yenu nami ni mmoja wa wahusika coz toka mwaka 2010 kuna viwanja vilipimwa mpaka leo jiji wapo kimya.

Mimi nashauri hiyo kazi wapewe property developers
 
Mbona mlishafanya huo mpango angalia hapa kwenye link (Kigamboni New City) au mnataka kupiga hela nyingine za ili mtutengenezee video nyingine?

Hiyo ya Singapore si plan ya Kigamboni bali ni mfano wa wenzetu walivyojipanga,Nadhani sector ya makazi inahitaji mawazo mapana ili kurekebisha palipokosewa na kukubali matokeo yake kwa pande zote serikali na wananchi.
 
Tatizo ni kuwa maoni ya wananchi huwa hamuyasikilizi kusema ukweli, ila mnasikiliza ya wachache wanaomiliki tz. Naamini wananchi hatungependa kuona mnahangaikia kigamboni wakati dar ina maeneo mengi ya kurekebisha kama kujenga apartments sehemu mbalimbali, ku control kodi za nyumba, kupunguza foleni kwa kujenga angalau flyovers ubungo na tazara, kujenga barabara muhimu za ring ('ring roads') n.k.

Mama Tibaijuka kuna vitu mkivifanya kama nchi mtaonekana kweli mnafanya kazi lakini vipaumbele vyenu sijui huwa mnavitoa wapi! Leo mnajenga bandari ingine wakati hizi tatu na nzuri hazifanyi vizuri na zinahitaji kuboresha kwa gharama ndogo tu.

Anyway, nyie ndo wenye nchi kwa sasa ila wajukuu wenu watakuja kuwashangaa sana.
 
WanaJF

Ninakaribisha maoni yenu hasa nyie mlio nje na mnaishi katika miji iliyopangwa? Je uholela unavumiliwa au kuendekezwa? Tupe habari.

Mama Tibaijuka
mweshimiwa waziri uholela ni uzembe tena uzembe wa serikali, pale upangaji wa mji unapokuwa uko nyuma na kasi ya ukuaji wa mji iko mbele ndio matokeo yake. tusitegemee kujenga miji yetu kwa staili ya kuwaacha watu wajenge holela alafu tuje kuwafidia na kuwahamisha. ni gharama kubwa sana kujenga mji uliokwisha vurugika na hapo tunazungumzia watanzania wa kipato cha kati na chini kuwaondoa mijini.

Kutokupanga miji kufanya gharama za kuweka huduma za jamii kuwa ghali zaidi maana ukitaka kuweka barabara unatoa fidia, ukitaka kupeleka maji unatoa fidia. mheshimiwa waziri tafuta mbinu za kunusuru miji yetu. punguza gharama za upimaji ili kila mtu ajenge katika kiwanja kilichopimwa.

Hapa sio lazima uwafidie wananchi waondoke bali eneo la upimaji mnaweza kukubaliana na wanachi wa eneo husika serikali inaleta wataalamu kupima, wananchi wanachangia gharama kidogo za kuchonga barabara katika eneo husika na kila anayeuza kiwanja serikali inachukua asilimia Fulani.

hapa lengo serikali isifanye kama biashara bali iwe ni mbinu ya kupunguza gharama na kuelekea kupata mapato zaidi. mfano swala la kurasimisha shughuli zote za biashara ili ziwe zinalipa kodi haliwezekani katika makazi holela. hapa serikali inakosa mapato mengi kutokana na shughuli za biashara zisizolipa kodi. swala la anwani za makazi haliwezekani katika makazi holela.

Kwa kujumuisha mbali na kufikiria miji kama kigamboni tunaomba ututengenezee miji inayokua kuelekea mbagala, gongo la mboto, kimara, bunju iliyopangika na hapa si lazima tupate hati kama garama za kutengeneza ramani ni kubwa bali angalau maeneo yakue yakiwa yako katika mpangilio mzuri na miji mingine nchini pia.

Mtu unataka kujenga kuwe na eneo lilipitishwa tayari kuwa ni la ujenzi wa nyumba za makazi. Tulikuwa tunawacheka wazaramo kuwa wanaukimbia mji lakini sasa naanza kuona hata serikali inatumia staili hiyo hiyo
 
Ningefurahi kuona maoni rasmi ya CDM kupitia jembe Halima Mdee
 
Last edited by a moderator:
Hi Prof,
Kwanza nikupe pongezi kwa ujasiri wako wa kujiunga na JF ambao wanasiasa wenzio wengi wanaichukulia JF kama kaa la moto na sumu kwao (Nkamia na wenzie) BUT pia hapa ndipo utapata mawazo sahihi na true reflection ya Wananchi wako dhidi ya Nchi yetu.

Kwa kusema hivyo nirudi kwenye Topic, Mama Professeri Mimi naona Tanzania kama Tanzania tumeshajifunza mengi sana toka kwa wenzetu, hatuhitaji kujifunza tena bali tunahitaji kuyaweka kwenye vitendo yale tuliyojifunza. hatuhitaji kuja na mipango miji mingine wakati hata hio tuliyonayo hatujatekeleza hata mmoja au nusu yake pengine. Pita kwa mtogole, Pita maeneo mengine ambayo kila mtu anajenga anavyopenda, rushwa imetamalaki kila pembe. Mimi niko tayari kufanya kazi pamoja na wewe kama utakua na nia ya kweli....
 
Kwanza nianze kwa kukupongeza prof. Tibaijuka kwa kuileta hii mada hapa, pili nimepitia michango ya watu wengine kwa kweli yote nayaunga mkono na ukiyaangalia kwa jicho la tatu utagundua kuwa ninyi ambao mmepewa dhamana ya kuendesha serikali ndio mnaoturudisha nyuma.

Nikianza na wewe binafsi sina wasiwasi na exposure yako umetembelea miji mingi na bila kusahau mchango wako ukiwa un habitat kwa nini hamjifunzi? Kwanini hamyatekelezi hapa nyumbani? Sheria zipo tena nzuri sana kwanini hamzitumii na kuzitekeleza? Hayo yote ya master plan mpaka napaka kichefuchefu nikisikia hilo neno, zipo nyingi sana hapa kwetu wenzetu wanauthubutu wakutenda lakini sio serikali hii sikivu ya ccm.

Samahani hapa lengo langu si kuleta uchama bali kueleza ukweli namna propaganda zilivyoingia kwenye mambo muhimu ya nchi sina budi kusema kuwa serikali ya ccm kwa muda wote huu mliokuwa madarakani mmetuangusha wananchi na wapenda maendeleo. Onyesheni mfano prof. Shirikiana na wasomi wenzako mliopo kwenye baraza la mawaziri kuueleza huu ukweli miji yetu inatia kinyaa kwa kweli, ndio maana kwa sasa ofisi yoyote ya mashirika makubwa kama un n.k. Zipo nairobi kwanini? Miundombinu mizuri kuna makazi ya maana

ushauri wangu; anzeni kuonyesha mfano ktk hiyo mnayoiita master plan ya kigamboni fanyeni tathimini ya haki muwapatie chao waathirika wote wa mradi kuendana na soko halisi la sasa utaona kama kuna mwananchi yoyote atakaepinga.
 
Tunamuomba Mama Pro, Tibaijuka kujibu tuhuma dhidi yake kuhusu mradi waKigamboni ili kuondoa wingu juu ya mradi huu, Mnamo tarehe 7/December 2012 inasadikika Mheshimiwa Waziri alisafiri kwenda nchini Thailand ambako ulikutana na wakuu wa kampuni kutoka China kusaini mkataba wa ujenzi wa mji kisasa wa Kigamboni. Mheshimiwa kwa mujibu wa vyanzo mhimu wewe utapata 3% kama aksante kutoka kwenye kampuni hii.

Pia kuna lawama kutoka kwa wadau wakuu ikiwemo wabunge na madiwani ambao ni wawakirishi wa wananchi hukuwashirikisha katika maamuzi juu ya mkataba huu na mradi kwa ujumla.

Mwisho tungependa kujua ni lini zabuni ya ujenzi wa mji wa kigamboni ilitangazwa kwa mujibu wa Public Procurement Regularity Authority-PPRA, ni kwa kupitia mtandao gani au gazeti gani la hapa nchini au nje ya nchi ilitangazwa (International Competitive Procurement-ICP) ili tujirishe kuwa kulikuwa na uwazi katika diri hili. kwa mujibu wa PPRA thamani ya mradi huo hauwezi kuwa Single source au International shoping. Tunaomba kujua sisi wananchi wa kawaida.
 
Mkuu nilikuwa nashauri,tujaribu kupanga miji yetu vizuri katika hizi Wilaya mpya zinazoanzishwa kwa kufuata Mipango miji ya kisasa:

[1].Tutafute wilaya mpya chache tuanze nazo na iwe mfano kwa Madiwani,kwani wao ni waamuzi katika ngazi ya chini wasio elewa umuhimu wa kuwa na miji uliopangika.
[2].Wilaya mpya na miji isianzishwe au kutangazwa mpaka Master Plan inayozingatia Mpango Miji ya kisasa imepitishwa na Wizara ya Ardhi.
[3].Maafisa Mipango miji wengi walio Wilayani wajengewe uwezo kwa kufanya study Tour katika miji iliyopangika,ili kuwa na uelewa wa pamoja katika kutekeleza majukumu yao.
[4].Mamla za kusimamia miji ziundwe ili kusimamia mipango miji,mfano Dodoma imekuwa ilivyo kwa sababu ya nguvu ya Serikali Kuu,na Mamlaka ambayo haingiliwi na wanasiasa(madiwani)
[5].itungwe sheria inayoruhusu upana wa barabara za mitaa kuwa pana zaidi kama ulaya,ili kuepuka adha ya foleni kwa miaka ijayo.

[6].Master Plan za Wilaya mpya ziwe zinatangazwa ,sambamba na tangazo la kuanzishwa kwa Wilaya Mpya,ilim kuvutia wawekezaji,na kuharakisha ukuaji wa miji mipya.
[7].Baadhi ya mipango mikakati iliyopo katika Bajeti iwe inabadilisrabihwa ili kukidhi malenge ya ukuaji wa miji;mfano badala ya kuweka Mkurabita,au Mkukuta,Tuingize kipengele cha kutenga bajeti za Master Plan na upimaji wa viwanja na upanuzi wa miji na utunzaji wa maeneo ya wazi.
 
Mh. Prof. Mama Anna Tibaijuka Kajumulo nashukuru sana kutupatia nafasi hii na kama mchangiaji mmoja anavyosema kuwa mawazo huwa yayasikilizwi lakini wacha niandike tu!
  1. Uliwahi kusikika ukisema kipindi fulani kuwa ukitua na ndege katika miji yetu na hasa Dar es Salaam, ukiwa na mgeni unaweza hata kuangalia pembeni kufuatia mpangilo mbovu wa mji unaofanya uonekane kama 'takataka'. Hii ni kweli lakini umefanya juhudi gani hadi sasa tangia uingie wizarani kurekebisha (angalau) hali hii!??
  2. Katika mji wako wa Muleba ambao ni mdogo sana na kujaliwa uoto wa asili mzuri unaonekana kupimwa lakini ni kwa asilimia ndogo tu. Mwaka juzi vilipimwa viwanja na kuuzwa kwa bei kubwa kulinganisha na fidia kiduchu sana iliyotolewa lakini hadi sasa hata barabara hazijachongwa na matokeo yake ujenzi holela unanyemelea maeneo hayo hayo yaliyopimwa! Unaweza kutupa mwanga kidogo juu ya hili pia?
 
Wahaya wananchekeshaga sana. Mi nilidhani ni watoto wa shule tu ndio hawajui kiliandika neno AHIDI kumbe hata huyu bi mkubwa naye ni vivo hivo. Wameahidi na siyo wamehaidi.
 
Mkuu Anna Tibaijuka nasapoti hoja yako ila kwa mawazo tofauti!

Suala la masterplan ni suala la serikali inajenga ama property developer? Ukiangalia picha hapo chini ni mji wa mwanza, watu wanakimbilia milimani na matokeo yake miundombinu inakuwa shida kuwafikia na kuongeza makazi holela.

Ninachoomba suala la upimaji wa ardhi ipewe sekta binafsi na serikali ibaki kuwa wasimamizi wa zoning. Sababu kubwa ni urasimu uliopo serikalini..viwanja vikipimwa mwaka huu mnaweza kukaa hadi miaka 3 hamjui nini hatma yenu nami ni mmoja wa wahusika coz toka mwaka 2010 kuna viwanja vilipimwa mpaka leo jiji wapo kimya.

Mimi nashauri hiyo kazi wapewe property developers

Mkuu Halmashauri zimeshindwa kusimamia ukuaji wa miji.Yaani Dodoma isingekuwa na chombo kilichoundwa kusimamia mji,Dodoma isingepangika vile.

Serikali pia iongeze fedha katika miji mingine na ikiwezekana iundwe Mamlaka ambayo haitakuwa inaingiliwa na Madiwani,kwani wao wanachangia usimamizi mbovu wa miji.

Wavamizi wa maeneo ya wazi wakitaka kuvunjiwa,wanasiasa wamekuwa wanatetea kwa sabubu za kulinda kura zao wakati wa uchaguzi.
 
Mama!

Kwanza nikusifu, nikiongozi wakwanza aliyetoa mawazo ya nini amaeona ulaya baada ya ziara?

Maana huwa tunajiuliza viongozi wetu wakisafiri huko nje huwa hawaoni jingine la ziada zaidi ya shopping za C & A?

Lakini sasa!

Kwa mapnaglio wa mipango miji uliopo Tanzania, na ukosefu wa nidhamu wa walionao vijana wako pale ardhi sijui kama hayo yatatekelezeka?

mfano ni juzi tu ndio nimekusikia "kumbe kutoa leseni ya biashara bila kujua matumizi ya ardhi inakokwenda kuwekwa hiyo biashara ni kosa?
 
Why Kigamboni? Nikiangalia Resources zinazokwenda hapo sipati justification.

La swali la msingi, tunataka kufanya Land Reclamation Tanzania? Kwa nini?
Na kama hatuhitaji, kwa nini mlienda kujifunza?

Kuna case moja ya TZ na mikaratusi Australia nayo ilikuwa hivi hivi
 
WanaJF


Ninakaribisha maoni yenu hasa nyie mlio nje na mnaishi katika miji iliyopangwa? Je uholela unavumiliwa au kuendekezwa? Tupe habari.

Umesema kupanga ni kuchagua. Tanzania ina zaidi ya wakaazi milioni 45. Zaidi ya milioni 20 kati ya hao wanaishi mijini, au pembezoni mwa miji na kati ya hao, zaidi ya 90% wanaishi maeneo ambayo hayana mipango miji wala makazi yao hayajapimwa.
Ni aibu kwa nchi yenye viongozi na wasomi kuwa wanaongelea Kigamboni miaka nenda rudi, eneo ambalo halitaishi zaidi ya watu laki tano. Hivi inagharimu bilioni ngapi kutengeza karamani kama hako ulikoweka kwenye picha?
Ramani ya Kigambini ipo, na hata kama haitajengwa leo, tunajua kuwa itajengwa tu, hata miaka 50 ijayo.

Mh Waziri nakuomba kwa heshima na taadhima, angalau kwa muda uliobaki nao kuongoza wizara hiyo, tutengenezee mipango miji ya miji hata 20 tu hapa Tanzania. Najua hii nchi ina zaidi ya 'miji' 100, lakini naomba angalau target miji 20. Hizo ramani ziwepo mahali fulani, ili hata baadae wakija viongozi wengine wakute kuna "kazi" ya kufanya. Hii nchi hadi sasa haina dira, na kila kiongozi akija anafanya anavyojisikia kwa sababu haina master plans.
Kwenye hizi nchi zilizoendelea, si ajabu ukakutana na 'pori', kumbe sio pori, ni mji mkubwa tu 'uliojengwa' miaka 40 iliyopita, ila ujenzi wake bado upo katika stage ya kwenye 'karatasi'. Hapo hata aje kiongozi 'nabii', hawezi kubadilisha; ama anajenga, au anapaacha palivyo.
Ingawa kwa sasa pengine hatuna hela za kujenga, lakini hata za kupanga na kuchora hatuna?!!!
 
Back
Top Bottom