Sarah Simbaulanga: Mwanamke wa kwanza kuiba pesa ndefu katika historia ya benki zote nchini

Nakumbuka kesi ya Maumba yalitajwa mafuta fulani ya mgando aliyokuwa anatumia kwenye shughuli yake, basi yale mafuta ukinunuliwa nyumbani kwenda nayo boarding skuli unaona noma kishenzi!-yale mafuta kama kuna mtu anayakumbuka tafadhali

Yolanda au Ayu??
 
Duh, kweli tumetoka mbali, wakti wa simba ulanga nafikir nilikua la sita au saba,....na hiyo ya maumba jinsi walivyoisiliba kweny magezeti nakumbuka mtaani kwetu kila fundi cherehani mwanaume alikua anaonekana kama 'potential maumba'...

kipindi hicho cha mwinyi kupat pesa kwa kufanya deals na ulaghai, watu wakiita mishen tauni ndio kilianza kushika mizizi, na kuwa a way of life kwa watu wengi hata shule zilikua zinaoenka sio muhimu sana...

ya utapeli enzi hizo kuna vibao vilitoka kama kile kinakibwagizo 'bwana mangushi nakupa pole sana watu hao ni walaghai, wanaitwa matapeli eehh' wenye kumbukumbu watukumbushe bendi gani, kama sikose Maneti(?)
 
Our own bonnie and clyde. Sasa Tollywood yetu ingekua navipaji ingeigiza true story kama hizi kukumbusha na kuamsha fikra za wananchi wa Tz. Lakini ni sijui kanumba kaiba mke wa ray,sijui nani anamdharau mumewe baadae anakuja kujujta. Zimekua overdone!
 
kuna vibao vilitoka kama kile kinakibwagizo 'bwana mangushi nakupa pole sana watu hao ni walaghai, wanaitwa matapeli eehh' wenye kumbukumbu watukumbushe bendi gani, kama sikose Maneti(?)
Kipindi hicho radio ni moja ukitoka nyumbani mziki umeanza unaweza kwenda kwa jirani kuumalizia.... mi nakumbuka enzi za Mwanameka.... "Uliposikia eeh eeh, kwamba Musa ameoa, kaoa mke wa ndoa, ukataka na kulia uhuni ukaweka kando... mwanameka umeleta maneno, umeuvunja unyumba wa Musa...."

Those were the days.
 
Those were the days, the days of our lives.
Gazeti la mfanyakazi ndio lilikuwa kama mwanahalisi ya sasa

Mhariri na mwandishi wa habari za kiutafiti alikuwa Marehemu Stanslaus Katabalo.....alikuwa aliishi Ilala sharifu shamba........walimfix yule miaka ya baadaye ya kufikia 90....inahisiwa ilihisiwa na mafisadi wa mwanzo wa vitalu vya uwindaji...na LOLIONDO GATE yao.....huyo kwa sasa ungeweza kumfanananisha na SAED KUBENEA.

Nashangaa sijaona waandishi wa habari wakimuenzi huyu STAN K..na waandishi wengine waliokufa kwenye mazingira ya aajabu ajabu.

Hivi nani anajuwa HEMED KIWANGA aliyekuwa mwandishi/mhariri wa habari za starehe wa MFANYAKAZI yupo wapi?
 
Kesi ambazo zilitamba ni ile kesi ya uhaini ya miaka ya 80. Hii ya Simbaulanga ya mwaka 89 ilikuwa cha mtoto kwanza Nyerere alikuwa ameshang'atuka. Watu walikuwa wanakatazwa kupaki Range Rover karibu na benki. Hii nchi bana tumetoka mbali kweli. Maaskari wana vigolf wanamfukuza mwizi anayeendesha Range.
 
Mwanakijiji hebu weka habari kwa kirefu ,mie hata simwelewi wala jina sijawahi kulisikia
Ni miaka gani hiyo na wapi??
sio wote tumewahi kumsikia huyu dada Sara Simbaulanga
Nawakakilisha!
 
Duh, kweli tumetoka mbali

ya utapeli enzi hizo kuna vibao vilitoka kama kile kinakibwagizo 'bwana mangushi nakupa pole sana watu hao ni walaghai, wanaitwa matapeli eehh' wenye kumbukumbu watukumbushe bendi gani, kama sikose Maneti(?)

Kaka Madago hiyo AVATOR yako hapo juu ......inatukwanza wenye nani hii za karibu....trully speaking ....nimeona tu sasa nimemzuia shemeji yako kuondoka ....
na nilichotaka kuandika kimeondoka chote......sijui inakuwaje hii.....
 
Nakumbuka kesi ya Maumba yalitajwa mafuta fulani ya mgando aliyokuwa anatumia kwenye shughuli yake, basi yale mafuta ukinunuliwa nyumbani kwenda nayo boarding skuli unaona noma kishenzi!-yale mafuta kama kuna mtu anayakumbuka tafadhali

nadhani rays au reizi
Mhhh maumba in action, duh nilikuwa madarasa ya mwanzo ya p/s wakati janga hili linatokea nakumbuka nilivyopata shida kuelewa maana ya neno kunajisi na kulawiti....maumba amelawiti na kunajisi wanafunzi...ooh sentensi hii ilinichukua muda kuilelewa

mix with yours
 
Kweli kabisa mwanakijiji huyu mama aliwahi, maana enzi zile wizi ulikuwa haulindwi wala kusukiwa mikakati IKULU kama ilivyo sasa ambapo angechukua kiualaini na kuzikuta nje zinamsubiri badala ya kukimbia na bulungutu.

Hapo penye nyekundu ndipo panaponichosha. Ina maana siku hizi IKULU ni PANGO LA WANYANG'ANYI?
 
Kesi ambazo zilitamba ni ile kesi ya uhaini ya miaka ya 80. Hii ya Simbaulanga ya mwaka 89 ilikuwa cha mtoto kwanza Nyerere alikuwa ameshang'atuka. Watu walikuwa wanakatazwa kupaki Range Rover karibu na benki. Hii nchi bana tumetoka mbali kweli. Maaskari wana vigolf wanamfukuza mwizi anayeendesha Range.

na Kuna ile kesi ya mauaji ya kimapenzi ya ASHA MKWIZU, nani anaikumbuka humu?, nayo ilikuwa hot kweli that time

Kesi ya Sara Martin Simbaulanga aka Khadija Kimbau, ukiingalia kiundani ilikuwa imejaa Mapenzi zaidi ya maendeleo binafsi, ilikuwa inaonekana yule mama alikuwa ameisha kabisa kwa Toroha M Toroha na ndie aliyekuwa mastermind wa ile move yote
 
Do you guys remember advocate maarufu enzi hizo MURTAZA LAKHA....those were the days sio wanasheria [baadhi] wa siku hizi wanakutana kupanga ushindi wa mezani kati ya wakili wa mashtaka /mshtakiwa na hakimu....na kutoa ushindi kwa mteja[malalamikaji au mlalamikiwa] anayelipa fee kubwa zaidi.

wanasheria wapunguze nao tamaa ya pesa. Wanasheria wengi siku hizi wanatajirika haraka haraka kwa njia haramu...just angalia wakili wa TANESCO ...wanaitwa REX ATORNEYS na Mwanasheria mkuu walivyo collaborate kuiingiza TANESCO kingi!!!..wamekula kote kote!!
 
ndiyo point niliyotaka kuleta.. kwanini tulikuwa very serious wakati ule..? Leo kuna mama mwingine anatuhumiwa kuiba bilioni 1.3 na hakuna watu wanaoshtuka!

Sasa hivi thamani ya shilingi imeshuka imefikia kipindi hiyo bil. mtu anaita vijisenti tu
 
Watu walikuwa wanakatazwa kupaki Range Rover karibu na benki. Hii nchi bana tumetoka mbali kweli. Maaskari wana vigolf wanamfukuza mwizi anayeendesha Range.

Eee bwana ee umenikumbusha mbali! Hivi kweli ilikuwepo hiyo sheria ya kukataza Rangerover karibu na benki au tulikuwa tunadanganyana simulizi za Willy Gamba?
 
Back
Top Bottom