Masikini wasipewe vibali kujenga mjini. Huchafua miji na vijumba vyao

Kuna kitu kinaitwa mixed economy, masikini na matajiri wanategemeana. Capitalists waliliona hili, huwa wanajenga apartments katikati ya mji na kuweka flats chache wanaziita affordable flats kwa wasio na uwezo.

Tajiri anatengeneza biashara na masikini anategemea ajira katika biashara hizo..
 
Habari Wakuu!

Kama kichwa kinavyoeleza hapo, ingawaje Masikini naye mtu japokuwa hana kitu lakini hatuwezi kuukataa ukweli kuwa Masikini ndio mashetani yanayoishi na kuonekana live kwa macho yetu wenyewe.

Kuna watu hapa watasema nawasema vibaya MASIKINI, wengine watasema najisikia, nawadharau na kuwatolea maneno makali hao Masikini. Lakini nataka kusema hapa mimi mwenyewe ni masikini, hivi mambo niyasemayo hapa yananihusu hata Mimi.
Sisi masikini ni mashetani tunaoishi live katika macho ya nyama.

Tatizo la miji kuwa michafu, na watu kujenga pasipo mpangilio linasababishwa na Masikini. Unajua masikini ni mashetani hivyo hawanaga mipangilio, wapo rafu wanajenga hovyo hovyo.

Kama ingekuwa amri yangu, masikini leo hii wasingepewa ruhusa/kibali kujenga kwenye miji na majiji makubwa. Wakaishi huko porini huko kwenye mashamba wakalime.

Serikali kama inataka miji ijengwe kwa mpangilio mzuri basi lazima litolewe tamko kuwa Masikini hawatapewa kibali cha kujenga mijini, na mtu yeyote anayetaka kujenga nyumba mjini anapaswa awe na kiasi cha pesa kisichopungua milioni 50.

Masikini wawekewe sheria kali zitakazowabana ili wasilete ushetani wao Duniani.

Kama wanataka kuishi mjini basi serikali ijenge nyumba za kupanga, au mashirika na makampuni ndio yafanye kazi hiyo kujenga Apartments ili hao masikini wapange.

Matajiri sina neno nao, nafahamu wao wanamuwakilisha Mungu kwani Mungu ni tajiri, ndio maana matajiri hujenga na kuweka mambo/vitu vyao katika mpangilio mzuri.

Miji yote iliyotekwa na masikini lazima iwe michafu inayonuka, vijumba vimejengwa hovyo hovyo Kama takataka.

Masikini wajengewe miji Yao huko nje kabisa ya miji au maporini huko wakae wenyewe, au Kama wanataka kuishi mjini basi wapangishe nyumba zilizojengwa na serikali au matajiri.

Sitaki kuzungumzua habari ya machinga jinsi wanavyovuruga miji na kusababisha uchafu wakaapo barabarani.

Niishie hapa Masikini wenzangu wasije nipiga mawe, najua wataniona lakini ukweli nimewapa, wengine watanichukia lakini hilo halinipi shida kwani mashetani ni kawaida Yao kuwa na chuki.

Mashetani yakikupenda jua ni Kwa unafiki na yanakitu yanakihitaji kutoka kwako.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dodoma
kumbuka hao matajiri wote walikuwa masikini, na wewe tajiri wa leo unaweza kuwa masikini wa kesho. utakuja uambiwe uondoke pia.Mungu akusaidie.
 
Ubaya ni kwamba shetani hua halali anskusikiliza tu unavyo jisemesha ipo siku utsikumbuka hii kauli yako


Shetani si ndio hao masikini,
Najua hawalali huwaga wanasubiri anguko la tajiri au wanamfanyia hila ili aanguke, badala ya wao kuhangaika kuondoka kwenye huo umasikini walionao

Huyo Shetani ni boya Kama maboya wengine.

Wenye MUNGU wala hatusumbui
 
Umeongea ukweli kabisa..majiji yote tanzania serikali ichukue ardhi..kisha ijenge magorofa katika mpango mzuri wa mji..na kuyapangisha..yeyote atakaye taka kuja mjini haruhusiwi kujenga bali kuja kupanga..hapa serikali itapata pesa maisha yake yote.

#MaendeleoHayanaChama


Masikini tutakukatalia maana tutakuambia tunahaki ya kujenga Kama matajiri ilhali uwezo huo hatuna.

Tukijenga vibanda vyetu tunashindwa hata Kuzitunza Bustani, yaani kunakuwa Kama kuzimu.
Mitaa yetu masikini ni mfano halisi WA kuzimu
 
Shetani si ndio hao masikini,
Najua hawalali huwaga wanasubiri anguko la tajiri au wanamfanyia hila ili aanguke, badala ya wao kuhangaika kuondoka kwenye huo umasikini walionao

Huyo Shetani ni boya Kama maboya wengine.

Wenye MUNGU wala hatusumbui
Haya bwana maybe unaijua kesho yako
 
Back
Top Bottom