Kijukuu cha Tanzania
Member
- Dec 6, 2025
- 6
- 3
Mashirika ya haki za binadamu nchini Tanzania, yakiwemo Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), yalikumbwa na changamoto za kiutendaji na kiusalama wakati na baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025, katika mazingira ya mvutano mkubwa wa kisiasa na ulinzi mkali wa vyombo vya usalama.
Changamoto hizo ni pamoja na kukamatwa kwa watendaji wake, kunyang’anywa vifaa vya kazi, kuvamiwa na vyombo vya usalama na mashirika mengine kuhusishwa na matumizi ya fedha haramu.
Katika wiki zilizotangulia uchaguzi, mashirika hayo yalionya kuhusu kupungua kwa nafasi ya kiraia, yakieleza kuwa kuongezeka kwa vizuizi vya shughuli za kisiasa, mikusanyiko ya umma na upatikanaji wa taarifa kulihatarisha uaminifu wa mchakato wa uchaguzi. Hata hivyo, walieleza kuwa mapendekezo yao ya mageuzi na mazungumzo hayakuzingatiwa kikamilifu.
Siku ya uchaguzi na katika kipindi cha mara baada ya matokeo, taarifa za vurugu, kukamatwa kwa watu na madai ya matumizi ya nguvu kupita kiasi na vyombo vya usalama zilijitokeza katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Mashirika ya haki za binadamu yaliripoti matukio yaliyowahusisha waandamanaji, wafuasi wa vyama vya upinzani, waandishi wa habari na raia wa kawaida, ambapo baadhi yao walidaiwa kushikiliwa bila kufunguliwa mashtaka wazi.
Hali hiyo ilizidishwa na kusitishwa kwa muda kwa huduma za intaneti na mawasiliano ya kidijitali, hatua ambayo mashirika hayo yalisema ilikwamisha kwa kiasi kikubwa juhudi zao za kufuatilia matukio, kukusanya ushahidi na kutoa msaada wa kisheria kwa wakati. THRDC, LHRC na TLS yalisema kusitishwa kwa intaneti kulikiuka haki ya kupata taarifa na uhuru wa kutoa maoni, hasa katika kipindi muhimu cha kidemokrasia.
Wafanyakazi wa LHRC Kukamatwa
LHRC ilieleza kuwa baadhi ya wafanyakazi wake na waangalizi wa uchaguzi walizuiwa au kuhojiwa walipokuwa wakitekeleza majukumu yao ya ufuatiliaji, huku maeneo mengine yakizuiwa kufikika.
Shirika hilo limesema hatua hizo zilipunguza uangalizi huru na kuongeza hatari kwa watetezi wa haki za binadamu waliokuwa kazini.
Katika tukio hilo, Wafanyakazi na wadau wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) walivamiwa usiku wa kuamkia Novemba 12,2025 katika Hoteli ya Whitesands, Dar es Salaam, walipokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kikazi huku vifaa na vitambulisho vyao vikichukuliwa baada ya uvamizi huo. LHRC ilitoa taarifa ya uvamizi huo uliombatana na vitisho na unyanyasaji huku kikidai kuwa uvamizi huo unadhoofisha jitihada za watetezi wa haki za binadamu katika kutekeleza majukumu yao.
"Tukio la usalama lilitokea katika Hoteli ya Whitesands ambapo wafanyakazi wetu walikuwa wakitekeleza shughuli za kawaida. Usiku huo, hoteli yote iliwekwa chini ya ulinzi mkali, na timu yetu ilikumbana na vitisho na unyanyasaji. Vifaa vyao vilikamatwa na waliagizwa kuripoti katika ofisi ya Makosa ya jinai Kanda ya Dar es salaam, kwa mahojiano na uchunguzi," ilisema taarifa ya LHRC.
Ingawa vifaa vyao vilirudishwa Lakini pia kituo hicho kilieleza wasiwasi wake juu ya usalama wa vifaa hivyo na athari zake kwa usalama wa wafanyakazi wa LHRC na watetezi wa haki za Binadamu.
"Tunatiwa wasiwasi zaidi kwamba tukio hili limetokea wakati ambapo Jeshi la Polisi limehusishwa na matumizi ya nguvu kupita kiasi na vitisho dhidi ya wananchi, hali ambayo sasa imewafikia wafanyakazi wetu." Ilisema LHRC.
Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) yavamiwa:
Mwezi mmoja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi, Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) kilipanga kufanya maandamano kupinga kukamatwa na kudhalilishwa kwa mwanachama wake, Wakili Deogratius Mahinyila alipokuwa akihudhuria kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu Mahakama Kuu Dar es Salaam Septemba 15, 2025.
Hata hivyo, Septemba 22, 2025 iliyopangwa kuwa siku ya maandamano hayo, ofisi za TLS zilizo mtaa wa Chato jijini Dar es Salaam zilizingirwa na magari ya Polisi.
Tukio hilo liliibua mjadala mkubwa kuhusu vitisho kwa Taasisi za haki za binadamu katika uhuru wa utendaji kazi ingawa baada ya Tukio hilo TLS ilisisitiza kuwa haitakubali kufanya kazi kwa woga wala hofu.
"TLS itaendelea kutimiza majukumu yake kwa ueledi bila woga , upendeleo wala hofu wala husda katika kuhakikisha utawala wa sheria na haki za binadamu zinasimamiwa na kuheshimiwa."
Mbali na suala hilo, Rais wa TLS, Boniface Mwabukusi aliibuka na kukemea vitisho vinavyowakabili mawakili wanaosimamia kesi za Matukio ya Oktoba 29, jambo lililoibua mjadala wa viashiria vya udhibiti wa utendaji kazi wa mawakili katika kutetea maslahi ya umma. Mwabukusi alikemea tabia hiyo na kuiita kuwa ni "kubaka mfumo".
Kwa upande mwingine, TLS ilifungua kesi kupinga uhalali wa zuio la watu kutoka nje katika kipindi cha uchaguzi na hatua nyingine za dharura zilizochukuliwa na mamlaka husika.
"Tumefungua shauri Mahakama Kuu dhidi ya IGP Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Tanzania.Tunataka IGP atuambie na kuieleza Mahakama pamoja na Umma alikopata mamlaka ya kutoa amri ya kufungia watu ndani nchi nzima. Kwa kuwa amri ile ilikuwa ya Muda mfupi atuambie alichukua hatua gani kulinda usalama wa watu waliokuwa mbali na makazi yao, watoto na wananchi wanao lala mitaani ambao hawana makazi alifanya nini kuhakikisha usalama wao kabla ya kutoa tamko. Na aieleze Mahakama na Umma hiyo kazi Maalum ni ipi? na inahusianaje na vifo na mashambulio dhidi ya Raia katika makazi yao katika siku hizo za zuio?" Alisema Wakili Boniface Mwabukusi ambaye ni Rais wa TLS, kuhusu hatua hiyo huku akiongeza kuwa mambo yote yatawekwa hadharani bila vificho.
Picha ya Akili Mnemba"Hakuna Uhalifu ambao utafunikwa, Everything will be Exposed na TLS itachukua hatua za Kisheria ndani na nje ya nchi. Tumeanza," alisema Wakili Mwabukusi.
TLS ilieleza kuwa hatua hizo zilikuwa na athari za moja kwa moja kwa haki za kikatiba na ziliweka mfano hatarishi kwa uhuru wa raia.
Kesi hiyo bado ipo kwenye hatua za usikilizwaji.
Watetezi Haki za Binadamu kukamatwa
THRDC pia ilieleza wasiwasi kuhusu usalama wa watetezi wa haki za binadamu, ikisema hali ya vitisho na hofu iliongezeka miongoni mwa wanaharakati waliokuwa wakirekodi madai ya ukiukwaji wa haki.
Mtandao huo ulisema mazingira hayo yaliwalazimu baadhi ya mashirika kupunguza shughuli au kufanya kazi kwa tahadhari kubwa.
Katika taarifa zao baada ya uchaguzi, mashirika hayo yalitoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi huru kuhusu madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu, kuachiliwa kwa watu waliokamatwa kinyume cha sheria na kurejeshwa kwa uhuru kamili wa kiraia.
Aidha, yalihimiza serikali kushirikiana na asasi za kiraia katika juhudi za kurejesha imani ya umma na kuzuia vurugu katika chaguzi zijazo.
Mratibu Kitaifa wa THRDC, Wakili Onesmo Olengurumwa, alitoa wito kwa serikali kuwasikiliza wananchi na kile wanachohitaji ili kurejesha amani na imani na kuzuia vurugu katika chaguzi zijazo.
Olengurumwa alisisitiza kuwasikiliza wananchi kisha kuwepo na ukweli na uwajibikaji "Hakuna uponyaji wa Taifa bila ukweli, uwajibikaji, na wahanga kushiriki kikamilifu,” alisema Olengurumwa.
Alionya kuwa bila kufuata misingi hiyo, jitihada zozote za maridhiano zitakuwa ngumu kuzaa matokeo, hasa kutokana na ukubwa wa maumivu na hasara iliyopatikana.
Aidha, Wakili Onesmo amesisitiza kuwa Tanzania ina nafasi ya kujenga upya misingi ya haki, utu na amani, endapo mchakato wa maridhiano utaendeshwa katika misingi ya uwazi, ukweli na uwajibikaji na dhamira ya dhati.
Hitimisho
Wachambuzi wanasema changamoto zilizowakumba mashirika ya haki za binadamu wakati wa uchaguzi wa 2025 zinaakisi wasiwasi mpana kuhusu hali ya demokrasia, utawala wa sheria na uwajibikaji nchini Tanzania, pamoja na umuhimu wa nafasi ya asasi za kiraia katika kulinda haki za binadamu wakati wa vipindi vya mpito wa kisiasa.
Wakili Hamis Mayombo, Wakili Mwandamizi kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), amesema kuwa watetezi wa haki za binadamu ni kiungo muhimu katika jamii, hususan katika kuimarisha utawala wa sheria na demokrasia, kwani wao husimamia na kulinda haki za msingi za wananchi.
Amesema licha ya umuhimu wao, watetezi wa Haki za binadamu wamekuwa wakikumbana na changamoto nyingi katika utekelezaji wa majukumu yao, hali inayodhoofisha uhuru wa utendaji kazi wao na ufanisi wa kulinda haki za binadamu kwa ujumla.
Mayombo ametoa wito kwa Serikali na vyombo vya dola kuzingatia Katiba na sheria za nchi, pamoja na kutenganisha wazi majukumu ya watetezi wa haki za binadamu na shughuli za wanasiasa wa upinzani.
Amesema changamoto kubwa inayojitokeza ni mtazamo potofu wa baadhi ya mamlaka kuwaona watetezi wa haki za binadamu kama wanasiasa wa upinzani, jambo ambalo si la kweli. Amefafanua kuwa watetezi hao hufanya kazi zao kwa misingi ya sheria, kwa lengo la kubaini sheria zinazokiukwa na kuhakikisha haki zote zinalindwa na kuheshimiwa.
“Mtazamo huo sio sahihi na ndio chanzo cha changamoto nyingi zinazowakabili watetezi wa haki za binadamu. Natoa wito kwa vyombo vya dola, badala ya kuwabugudhi watetezi wa haki za binadamu, wawe mstari wa mbele kuwalinda ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi, huku kila mmoja akiwa salama na huru kufanya kazi kwa mujibu wa sheria,” anasema Mayombo.
Aidha, amewahimiza watetezi wa haki za binadamu kujiweka mbali na siasa ili waweze kusimama katikati na kutetea haki za yeyote anayodhulumiwa bila upendeleo, akisisitiza kuwa utawala wa sheria na demokrasia hauwezi kuimarika bila ulinzi na uhuru wa watetezi wa haki za binadamu.
Changamoto hizo ni pamoja na kukamatwa kwa watendaji wake, kunyang’anywa vifaa vya kazi, kuvamiwa na vyombo vya usalama na mashirika mengine kuhusishwa na matumizi ya fedha haramu.
Katika wiki zilizotangulia uchaguzi, mashirika hayo yalionya kuhusu kupungua kwa nafasi ya kiraia, yakieleza kuwa kuongezeka kwa vizuizi vya shughuli za kisiasa, mikusanyiko ya umma na upatikanaji wa taarifa kulihatarisha uaminifu wa mchakato wa uchaguzi. Hata hivyo, walieleza kuwa mapendekezo yao ya mageuzi na mazungumzo hayakuzingatiwa kikamilifu.
Siku ya uchaguzi na katika kipindi cha mara baada ya matokeo, taarifa za vurugu, kukamatwa kwa watu na madai ya matumizi ya nguvu kupita kiasi na vyombo vya usalama zilijitokeza katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Mashirika ya haki za binadamu yaliripoti matukio yaliyowahusisha waandamanaji, wafuasi wa vyama vya upinzani, waandishi wa habari na raia wa kawaida, ambapo baadhi yao walidaiwa kushikiliwa bila kufunguliwa mashtaka wazi.
Hali hiyo ilizidishwa na kusitishwa kwa muda kwa huduma za intaneti na mawasiliano ya kidijitali, hatua ambayo mashirika hayo yalisema ilikwamisha kwa kiasi kikubwa juhudi zao za kufuatilia matukio, kukusanya ushahidi na kutoa msaada wa kisheria kwa wakati. THRDC, LHRC na TLS yalisema kusitishwa kwa intaneti kulikiuka haki ya kupata taarifa na uhuru wa kutoa maoni, hasa katika kipindi muhimu cha kidemokrasia.
Wafanyakazi wa LHRC Kukamatwa
LHRC ilieleza kuwa baadhi ya wafanyakazi wake na waangalizi wa uchaguzi walizuiwa au kuhojiwa walipokuwa wakitekeleza majukumu yao ya ufuatiliaji, huku maeneo mengine yakizuiwa kufikika.
Shirika hilo limesema hatua hizo zilipunguza uangalizi huru na kuongeza hatari kwa watetezi wa haki za binadamu waliokuwa kazini.
Katika tukio hilo, Wafanyakazi na wadau wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) walivamiwa usiku wa kuamkia Novemba 12,2025 katika Hoteli ya Whitesands, Dar es Salaam, walipokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kikazi huku vifaa na vitambulisho vyao vikichukuliwa baada ya uvamizi huo. LHRC ilitoa taarifa ya uvamizi huo uliombatana na vitisho na unyanyasaji huku kikidai kuwa uvamizi huo unadhoofisha jitihada za watetezi wa haki za binadamu katika kutekeleza majukumu yao.
"Tukio la usalama lilitokea katika Hoteli ya Whitesands ambapo wafanyakazi wetu walikuwa wakitekeleza shughuli za kawaida. Usiku huo, hoteli yote iliwekwa chini ya ulinzi mkali, na timu yetu ilikumbana na vitisho na unyanyasaji. Vifaa vyao vilikamatwa na waliagizwa kuripoti katika ofisi ya Makosa ya jinai Kanda ya Dar es salaam, kwa mahojiano na uchunguzi," ilisema taarifa ya LHRC.
Ingawa vifaa vyao vilirudishwa Lakini pia kituo hicho kilieleza wasiwasi wake juu ya usalama wa vifaa hivyo na athari zake kwa usalama wa wafanyakazi wa LHRC na watetezi wa haki za Binadamu.
"Tunatiwa wasiwasi zaidi kwamba tukio hili limetokea wakati ambapo Jeshi la Polisi limehusishwa na matumizi ya nguvu kupita kiasi na vitisho dhidi ya wananchi, hali ambayo sasa imewafikia wafanyakazi wetu." Ilisema LHRC.
Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) yavamiwa:
Mwezi mmoja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi, Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) kilipanga kufanya maandamano kupinga kukamatwa na kudhalilishwa kwa mwanachama wake, Wakili Deogratius Mahinyila alipokuwa akihudhuria kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu Mahakama Kuu Dar es Salaam Septemba 15, 2025.
Hata hivyo, Septemba 22, 2025 iliyopangwa kuwa siku ya maandamano hayo, ofisi za TLS zilizo mtaa wa Chato jijini Dar es Salaam zilizingirwa na magari ya Polisi.
Tukio hilo liliibua mjadala mkubwa kuhusu vitisho kwa Taasisi za haki za binadamu katika uhuru wa utendaji kazi ingawa baada ya Tukio hilo TLS ilisisitiza kuwa haitakubali kufanya kazi kwa woga wala hofu.
"TLS itaendelea kutimiza majukumu yake kwa ueledi bila woga , upendeleo wala hofu wala husda katika kuhakikisha utawala wa sheria na haki za binadamu zinasimamiwa na kuheshimiwa."
"Tumefungua shauri Mahakama Kuu dhidi ya IGP Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Tanzania.Tunataka IGP atuambie na kuieleza Mahakama pamoja na Umma alikopata mamlaka ya kutoa amri ya kufungia watu ndani nchi nzima. Kwa kuwa amri ile ilikuwa ya Muda mfupi atuambie alichukua hatua gani kulinda usalama wa watu waliokuwa mbali na makazi yao, watoto na wananchi wanao lala mitaani ambao hawana makazi alifanya nini kuhakikisha usalama wao kabla ya kutoa tamko. Na aieleze Mahakama na Umma hiyo kazi Maalum ni ipi? na inahusianaje na vifo na mashambulio dhidi ya Raia katika makazi yao katika siku hizo za zuio?" Alisema Wakili Boniface Mwabukusi ambaye ni Rais wa TLS, kuhusu hatua hiyo huku akiongeza kuwa mambo yote yatawekwa hadharani bila vificho.
Picha ya Akili Mnemba