Marekani inapaswa kuacha kuongeza chuki katika suala la Bahari ya Kusini ya China

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
VCG111468797878.jpg


Hivi karibuni, Balozi wa Ufilipino nchini Marekani, Jose Manuel Romualdez alipohojiwa na chombo kimoja cha habari alidai kuwa, Bahari ya Kusini ya China, na si Taiwan, ni sehemu ya hatari, ambapo vita inaweza kuanza wakati wowote.

Siku moja kabla ya hapo, Ufilipino, pamoja na Marekani na Japan, zilirejea tena ahadi yao ya uhuru wa kusafiri na sheria ya kimataifa katika Bahari ya Kusini ya China na Bahari ya Mashariki ya China, na uamuzi wao wa kufanya uratibu wa karibu wa pande tatu kuhusu suala hilo.

Katika siku za karibuni, Ufilipino imeendelea kuichokoza China kuhusu suala la Bahari ya Kusini ya China, huku kivuli cha Marekani kikionekana kuwa nyuma ya suala hilo.

Kwa miaka mingi iliyopita, China imeweka msimamo wake wazi kabisa kwa Ufilipino, kwamba kamwe haitakuwa ya kwanza kufyatua risasi, jambo ambalo ni la msingi. Ingawa, iwe ni wakati wa Amani ama vita, China itasimama kithabiti kuhusu uhuru na mamlaka ya ardhi yake. Hakuna msingi wa kuzusha madai yasiyo na ukweli yanayoweza kufuta uthibitisho wa kihistoria wa mamlaka halali ya visiwa, visiwa vya matumbawe, na miamba katika Bahari ya Kusini ya China.

Mazungumzo ya Amani ndio njia pekee ya kusuluhisha mvutano wowote. China haitaki kuingia kwenye vita na Ufilipino, badala yake, inatafuta amani, kudumisha utawala wa sheria na kufanya mazungumzo ya kina ili kutatua masuala yanayohusiana na migogoro ya mpaka. Amani inapaswa kupewa kipaumbele katika mioyo ya China na Ufilipino, na ingawa kuna mgogoro wa mipaka, bado inawezekana pande hizo zikaketi na kujadiliana, na kujaribu kutafuta suluhisho la amani kwa migogoro hiyo kuliko kuingia kwenye vita, ambayo haitanufaisha upande wowote.

Kama Ufilipino inataka kujibadili na kuwa mbadala wa Marekani, hilo halitakuwa jambo zuri kwa nchi hiyo wala Marekani. Majeshi ya China na Marekani, ambayo sasa yamerejesha tena mawasiliano ya kijeshi, yanapaswa kufanya mazungumzo ya moja kwa moja kwa sababu hakuna kati yao anayetaka vita ama mvutano wa moja kwa moja wa kijeshi.

Ukweli ni kwamba, kuna mwelekeo wa Marekani kufanya kila kinachowezekana kudhibiti ukuaji wa China. Hata hivyo, Marekani inapaswa kuwa na mtazamo halisi kwa kuwa hakuna nchi ama kundi la nchi duniani zinazoweza kudhibiti maendeleo ya China. Haki ya maendeleo ya uchumi kwa njia ya amani ni haki isiyopingika ya watu wa China. Sasa inawezekanaje kwa nchi nyingine kudhani kwamba inaweza kuchukua ama kuharibu njia ya maendeleo ya China, nchi yenye idadi ya watu inayofikia bilioni 1.4?

Jambo jingine ni kwamba, Marekani inapaswa kuachana na ndoto ya jinamizi kuwa China itakuwa dola yenye nguvu zaidi duniani. Ukweli ni kwamba, China haitaki na wala haina nia ya kuwa nchi inayoongoza ama dola yenye nguvu Zaidi duniani. China inataka kuzitendea nchi zote kwa usawa, iwe ni nchi kubwa ama ndogo, zilizoendelea ikiwemo Marekani ama zilizo nyuma kimaendeleo. Msimamo wa China kwa Marekani ni wa wazi kabisa: kila nchi ina imani yake, na haipaswi kulazimisha nchi moja kufuata Imani ya nchi nyingine. Watu wa nchi zote wanapaswa kuishi kwa masikilizano kwa ajili ya manufaa ya wote na kwa lengo la kupunguza mvutano wa kimataifa.
 
China ipo kwenye Nchi zenye migogoro na Nchi inazopakana nazo kama India wamesumbuana sana kule kwenye milima mpaka wanajeshi wao walikua wanazichapa kavu kavu na wanajeshi wa Kihindi sijui kama USA ana mkono wake hapo...
Vita ya karibuni ni China vs Taiwani maana huko muda wowote Taiwani akiamua kurudishia uchokozi wa China watapigana huku USA ndio ana mkono wake mkubwa ila China wanajitambua walipogundua kuwa USA anatumia vita kushusha Uchumi wa baadhi ya Nchi kama Russia na wao akapunguza Meli za kivita zilizo karibu na Taiwan..
 
Back
Top Bottom