Biashara inayostawi kati ya China na nchi za nje inatoa ishara gani?

Yoyo Zhou

Member
Jun 16, 2020
72
111
VCG111474631418.jpg

Takwimu zilizotolewa hivi karibuni na Idara Kuu ya Forodha ya China zinaonesha kuwa, kuanzia mwezi Januari hadi Februari mwaka huu, thamani ya jumla ya biashara ya bidhaa kati ya China na nchi za nje ilikuwa dola bilioni 930.86 za Kimarekani, ambalo ni ongezeko la asilimia 5.5 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hicho.

Kati ya biashara hiyo, mauzo ya bidhaa za China kwa nchi za nje yalikuwa dola bilioni 528.01 za Kimarekani, ambalo ni ongezeko la asilimia 7.1, na maagizo ya bidhaa kutoka nchi za nje yalikuwa dola bilioni 402.85 za Kimarekani, ambalo ni ongezeko la asilimia 3.5, hali ambayo ni nzuri kuliko ilivyotarajiwa na mashirika mbalimbali duniani. Je, biashara inayostawi kati ya China na nchi za nje imetoa ishara gani muhimu?

Kwanza, hali nzuri ya biashara kati ya China na nchi za nje inaashiria kuimarika zaidi kwa uchumi wa China. Biashara ya nje ni moja ya injini muhimu ya ukuaji wa uchumi wa China na inatoa nguvu kubwa ya maendeleo ya uchumi wa China. China ina uwezo mkubwa zaidi wa utengenezaji bidhaa duniani, biashara ya nje inatoa soko pana na fursa kubwa kwa maendeleo ya sekta za utengenezaji nchini China.

Wakati huo huo, biashara ya nje pia imesukuma maendeleo ya sekta nyingine zinazohusiana, zikiwemo uchukuzi, usafiri wa ndege na meli, na mambo ya kifedha, ambazo zinachangia sana maendeleo ya uchumi wa China.

Katika mkutano wa Bunge la Umma la China na mkutano wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China iliyofungwa hivi karibuni, serikali ya China imeweka lengo la ukuaji wa uchumi kwa mwaka huu kwa asilimia 5. Hali nzuri ya biashara na nje inatoa msingi imara kwa China kutimiza lengo hilo.

Pili, muundo wa wenzi wa kibiashara wa China umeboreshwa. Katika miezi miwili iliyopita ya mwaka huu, Umoja wa Nchi za Asia ya Kusini Mashariki (ASEAN) umeendelea kuwa mwenzi mkubwa zaidi wa kibiashara wa China.

Takwimu zinaonesha kuwa jumla ya thamani ya biashara kati ya China na ASEAN imeongezeka kwa asilimia 8.1, ikichukua asilimia 15 ya thamani ya jumla ya biashara kati ya China na nchi za nje. Wakati huohuo, thamani ya jumla ya biashara kati ya China na nchi zilizojiunga na ujenzi wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” imeongezeka kwa asilimia 9.

Tangu China itoe pendekezo hili, biashara imeendelea vizuri, na sasa biashara kati ya China na nchi zilizojiunga na pendekezo hilo inachukua asilimia 47.3 ya jumla ya biashara kati ya China na nchi za nje.

Ingawa Marekani inaendelea kuweka vikwazo kwa biashara yake na China, lakini mauzo ya bidhaa za China kwa Marekani yameendelea kuongezeka kwa kiasi kikubwa katika miezi miwili ya kwanza ya mwaka huu.

Hata hivyo, kama mwenzi mkubwa zaidi wa zamani wa kibiashara wa China, hadhi ya kibiashara ya Marekani kwa China sasa imeshuka hadi nafasi ya tatu, na kiwango cha biashara kati ya nchi hizo mbili ni sawa na asilimia 23 tu ya jumla ya biashara kati ya China na nchi za “Ukanda Mmoja, Njia Moja”.

Tatu, muundo wa bidhaa zilizouzwa na China kwa nchi za nje unaendelea kuboreshwa. Katika miezi miwili ya kwanza ya mwaka huu, bidhaa za China zilizouzwa zaidi ni pamoja na magari, ambayo yalikua kwa asilimia 15.8, vifaa vya umeme majumbani, ambavyo vilikua kwa asilimia 24.3, na meli ambayo ukuaji wake ulifikia asilimia 180.

Aidha, katika kipindi cha miezi miwili iliyopita, mauzo ya mitambo ya umeme ya China kwa nchi za nje yamechukua zaidi ya asilimia 59 kati ya bidhaa zote zilizouzwa na China kwa nchi za nje.

Ingawa Marekani na baadhi ya nchi za Magharibi zimeendelea kuiwekea vikwazo China katika uwanja wa teknolojia ya juu, lakini takwimu za biashara zimethibitisha kwamba, China imepiga hatua kubwa katika utengenezaji wa bidhaa za hali ya juu.
 
Back
Top Bottom