Marekani hawajaiacha Afghanistan kwa bahati ambaya. Huenda wakamtumia jasusi wao aliyekuwa makamu wa Rais, Amrullah Saleh

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,400
Marekani leo imetangaza kuongeza vikosi vya majeshi wapatao 1,000 ili kuongeza na kuimarisha ulinzi katika uwanja wa ndege wa Kabul.

Aliekuwa rais wa serikali ya vibaraka Ashraf Ghani ambae amekimbilia Oman amedaiwa kutoroka na kiasi kikubwa cha fedha kutoka benki kuu ya Afghanistan na magari manne pamoja na familia yake yote na watu wote wa karibu.

Lakini makamu wake bwana Amrullah Saleh amebaki nchini humo lakini katika maficho yaliyoko katika jimbo la Panjshir ambalo ni bonde lenye ambalo bado halijatwaliwa na Taliban.

Bonde hilo la Panjshir lipo kaskazini mashariki wa Kabul (maili 93) na karibu kabisa na mpaka na China, na bwana Saleh inadaiwa alikimbilia huko siku ya jumapili.

Jimbo hili la Panjshir lilikuwa chini ya ilokuwa Urusi kwenye miaka ya tisini kabla ya kuendelea kujitawala bila uwepo wa Taliban na limekuwa hivyo hadi leo.

Baadae hiyohiyo jumapili jioni Saleh akatuma ujumbe Twitter akisema yeye hatojisalimisha kwa Taliban na hatokaa nao chini ya dari pamoja, kisha kusema ana watu zaidi ya milioni moja wanaomuunga mkono.

1629209226714.png


Juu: ujumbe wa Saleh Twitter

Katika ujumbe wake huo akaendelea kusema kwamba hawatawaruhusu Taliban kuingia Panjshir na tupo tayari kupigana nao kwa nguvu zote.

Zipo pia taarifa zisizothibitrishwa zikidai kuwa bendera ya Panjshir ya Northern Alliance tayari imepandishwa katika bonde hilo.

Pia taarifa zingine zinadai watu wengi wamekimbilia katika bonde hilo linalosifika kwa ulinzi dhidi ya mashambulizi yoyote.

Lakini tumfahamu Amrullah Saleh ni nani?

Akiwa bado mdogo sana akipigana vita ya kuikomboa Panjshir pale ilipokuwa kwenye vita na Taliban kwenye miaka ya tisini.

Baadae akaingia katika serikali ya Afghanistan lakini akawa miongoni mwa watumishi wa serikali walotimuliwa baada ya Taliban kuingia Kabul na kuanza kutawala.

Bwana Saleh hapo mwanzo alikuwa ni mpiganaji wa Panjshir ambae baadae kuteuliwa na serikali ya Ghani kuwa mkurugenzi wa idara ya usalama na kisha baadae kuwa makamu wa raisi.

Ila hapo nyuma baada ya tukio la September 11 mwaka 2001 ambapo nchini Marekani majengo mawili marefu na pacha (Twin Towers) yalilipuliwa kwa mabomu yalotegwa kwenye ndege mbili tofauti, Saleh akaajiriwa na CIA na kuwa mtu wao yaani "asset".

Kitendo hicho kilimwezesha kuwa na mamlaka na kuweza kuunda idara ya ujasusi mwaka 2004.

Itakumbukwa mwaka 2010 mmoja wa viongozi wa Taliban bwana Baradar alikamatwa na majasusi wa Pakistani ISI na inasemekana ni kwa agizo la bwana Saleh.

Baradar akakaa jela bila kufunguliwa mashtaka mpaka Donald Trump alipokuja kumuombea baada ya mazungumzo na Taliban na serikali ya Ghani.

Kuunda idara ya ujasusi ya Afghanistan chini ya serikali kibaraka ya Ghani na uwepo wa majeshi ya kigeni kulimwezesha bwana Saleh kuwa na idadi kubwa na vyanzo na watoa taarifa yaani "informers" walotapakaa hadi mpakani na Pakistani na walokuwa wakiwachunguza Taliban kwa kila hatua walopita.

Lakini mwaka 2010 bwana Saleh alitimuliwa baada ya shambulio la kwenye mkutano wa amani ulokuwa ukifanyika mjini Kabul.

Akiwa nje ya ulingo wa siasa bwana Saleh bado liendelea na vita kwa Taliban na baadae mwaka 2018 bwana Ghani akamkaribisha kwenye serikali yake kuongoza wizara ya mambo ya ndani.

Baadae akateuliwa kuwa makamu wa raisi Ghani na ni wakati huo Marekani ilipoanza kuondoa majeshi yake nchini Afghanistan na pia kuwepa majaribio kadhaa ya kumuua yalofanywa na Taliban.

Mwezi Septemba mwaka 2020 Bwana Saleh akakoswakoswa kuuawa baada ya bomu kutupwa kwenye msafara wake mjini Kabul na watu wapatao 10 kufa.

Baadae Sahel akaibuka kwenye video huku akiwa amefunga kitambaa mkono wa kushoto ukiwa umejeruhiwa akiapa kuendelea kupigana na Taliban hadi mwisho.

Hivyo Marekani na utulivu wao kuhusu sakata hili la Taliban kuchukua nchi ndani ya wiki mbili badala ya siku 90 zilosemwa na Marekani, ni dalili tiosha kwamba kuna mpango B na C.

Pia inatufunza kwamba nchi za magharibi huwa hawakai sehemu bure bila kuwekeza katika kila sekta.

Hapo tutakapoona Taliban wakifanya wanachoahidi au la, majeshi ya kigeni yatarudi Afghanistan kwa njia zingine kupitia watu kama Amrullah Saleh.
 
Hakuna mpango wowote!

Ukweli ni kwamba wameshindwa vita.

Na vita siyo kurushiana risasi tu na kudondosheana mabomu.

Vita ni propaganda, itikadi, subira, nia, na intangibles nyingine kama hizo.

9/11 ni mwezi ujao.

Na Taliban watakuwa madarakani.

Talk about things coming full circle….
halafu watu wenye fikra km zako ni hovyo kabisa! Unadhani mmarekani anatoka virginia california huko aje kandahar kupgana vita badala ya kula bata kwenye fukwe za miami! Hawa jamaa wao walifocus huko wakilenga mafuta na madawa ya kulevya, kuna ushahidi mpk wa video CIA wakiyalinda mashaba makubwa ya opium huko iraq na pakstani! Kuthibitisha hiko nachosema ni kuwa jana tu Washngton imesema kuwa itahamishia nguvu kazi DRC kuliko na mzozo hii ni danganya toto pale wanatafuta madini ambayo yanatumika katika electric energy tecknologies( electric batteries n.k) mafuta so dili tena miaka michache ijayo! Yaani itafika tym kuiona sheli ya mafuta itakuwa vigumu kama kuiona internet cafe kwa sasa
 
halafu watu wenye fikra km zako ni hovyo kabisa! Unadhani mmarekani anatoka virginia california huko aje kandahar kupgana vita badala ya kula bata kwenye fukwe za miami! Hawa jamaa wao walifocus huko wakilenga mafuta na madawa ya kulevya, kuna ushahidi mpk wa video CIA wakiyalinda mashaba makubwa ya opium huko iraq na pakstani! Kuthibitisha hiko nachosema ni kuwa jana tu Washngton imesema kuwa itahamishia nguvu kazi DRC kuliko na mzozo hii ni danganya toto pale wanatafuta madini ambayo yanatumika katika electric energy tecknologies( electric batteries n.k) mafuta so dili tena miaka michache ijayo! Yaani itafika tym kuiona sheli ya mafuta itakuwa vigumu kama kuiona internet cafe kwa sasa
Marekani tayari wametangaza juzi kwamba magari ya mafuta mwisho 2030.

Uingereza nao tayari waliishasema mwisho 2030.

Hawa hufanya mambo kwa mpango na mikakati mikubwa.

Tayari viwanda vya batteries vinajengwa kufikia 2025 vitakuwa vimekamilika tayari kuanza kizalisha.

Hivyo uko sawa kabisa.
 
Back
Top Bottom