Afghanistan ya sasa chini ya utawala wa Taliban. Yazidi kuimarika karibu kwenye kila nyanja

SNAP J

JF-Expert Member
Dec 26, 2013
7,079
7,976
Tangu mwaka 2021ambapo kikundi cha wanamgambo wenye itikadi kali ya kiislamu cha Taliban kiliposhika hatamu nchini Afghanistan, na kuondoka kwa aibu majeshi ya Marekani yaliyokaa nchini humo kwa takribani miaka ishirini tangu Marekani ilipoivamia hiyo, karibu habari zote zinazoripotiwa na vyombo mbali mbali vya habari duniani zimekuwa karibu zote ni mbaya. Ni kama vile dunia imeshazoea baada ya kuaminishwa ya kuwa hakuna jema litakalotoka nje ya utawala wa kidemokrasia- utawala ambao Taliban waliukataa.

Hata pale Taliban inapofanya mambo mazuri, yamekuwa ama yakigeuzwa na kuripotiwa kama mambo mabaya ama kutoripotiwa kabisa.

Mfano halisi wa hili ni pale serikali ya Taliban ilipochukua hatua ya kupiga marufuku ya kilimo cha opium poppy, zao ambalo ndio hutumika kuzalisha madawa ya kulevya kama vile heroin na cocaine bado baadhi ya vyombo vya habari vya kimagharibi viliukosoa.

Ifahamike ya kuwa Afghanistan ilikuwa ni miongoni mwa nchi kinara kabisa duniani kwa kilimo cha opium.

Lakini mwishoni mwa mwaka jana 2023, Umoja wa Mataifa kupitia kitengo cha kupambana na madawa ya kulevya ulichapisha tafiti zilizoonyesha kuwa uzalishaji wa opium nchini Afghanistan umepungua kwa asilimia 95- Jambo ambalo Umoja huo uliipongeza utawala wa Taliban kwa jitihada hizo kubwa za kihistoria.


Mbali na hilo, Serikali ya Taliban imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali za kuijenga Afghanistan mpya ila juhudi hizo zimekuwa zikisua sua na kuingia dosari kutokana vikwazo vingi vya kiuchumi walivyowekewa na mataifa ya magharibi.

Jambo lililopelekea Taliban kutafuta njia nyinginezo mbadala kama vile kutumia rasilimali madini ya copa na lithium kama dhamana ili kupata mikopo kutoka
Asian Infrastructure Investment Bank.

Pia wamekuwa na ushirikiano mzuri na serikali ya China ambapo sasa hivi kuna makampuni ya kichina yanayojenga miundombinu ya mabara bara ya viwango vya lami ili kuweza kuviunganisha vijiji, miji, na majimbo nchini humo ambapo asilimia kubwa ya geografia yake ni milima na mabonde.

Sio hivyo tu, hivi majuzi Umoja ufahamikao kama Shanghai Cooperation Organisation (the SCO countries) ambayo yanajumisha nchi wanajumuiya kama vile ;

#China.
#Kazakhstan
#Kyrgyzstan
#Russia
#Tajikistan
#Uzbekistan
#India
#Pakistan

Yamesaini makubaliano ya awali (MoA) katika kilele cha kongamano la Usafirishaji nchi wanàchama wa SCO uliofanyika katika mjii mkuu wa Tashkent, nchini Uzbekistan.

Nchi hizo zimeadhimia kujenga two transport corridors zitakazopita katika mataifa yafuatayo:

1).Belarus – Russia – Kazakhstan – Uzbekistan – Afghanistan mpaka Pakistan

2). Russia - Caspian Sea - Turkmenistan - Uzbekistan mpaka Kyrgyzstan

Hivi sasa tuvyoongea, vijiji vingi vya Afghanistan vimeanza kuunganishwa kwa bara bara za viwango vya lami kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa hilo .

Hali kadhalika, Afghanistan sio tena taifa la kigaidi, machafuko, vita, wala la kuuza ngada. Sifa mbaya mbazo zimekuwa zikiliandama taifa hilo kwa miaka mingi.

Sasa hawa jamaa wa Magharibi, haswa Marekani, habari kama hizi hawataki dunia izisikie maana ni AIBU kwao kwani kwa muda wa miongo miwili hivi toka alipoivamia nchi hiyo kwa kile alichokiita ni mapambani dhidi ya ugaidi, na kusimika utawala wa kidemokrasia- hakuna cha maana alichokifanya, zaidi ya kuiacha magofu nchi hiyo, huku yeye akiendelea kunufaika kwa kuiba rasilimali na kufanya biashara ya kuuza dawa za kulevya.

Hakika, utakubaliana nami ya kuwa Afghanistan ya sasa chini ya utawala wa Taliban huwezi kuifananisha hata chembe na ile ya miaka ishirini iliyopita ya utawala Marekani na vibaraka wake Kabubl-bases Islamic Republic of Afghanistan.View attachment 2859174View attachment 2859173
IMG_20240101_123238.jpg


Sent from my Redmi 8A using JamiiForums mobile app
 
Mimi binafsi hawa watu weupe huwa nawaheshimu sana wakiamua jambo fulani.

Taliban nawafuatilia kwa karibu moves wanazo fanya hasa zinazogusa economics Taliban watakuwa mfano wangu mwepesi, wa haraka na wa kueleweka nitakao jifunza step by step kwa macho yangu bila kusimuliwa kama mageuzi ya kiuchumi yakitiki.

Hawa watu weupe wakiamua kubadilika au kubadili jambo fulani wako makini sana.

Sekta ya nishati, madini, miundombinu, viwanda nazifuatilia taratibu pia Indonesia ana kitu
 
Kabisa na kusoma ni haki yakimsingi kabisa ya kila mtu
Nafikiri kuna utaratibu waandaa kuhusu wanawake kupata elimu pasina kuathiri misimamo na itikadi zao za kiimani.

Sifahamu sana kuhusu itikadi zao za kiimani zinasema nini kuhusu wanawake na masuala ya kazi na elimu nikifahamu hata kidogo nami nikichanganya za kwangu nitajiridhisha je, ni sahihi kwa misingi yao ya kiimani kufanya kile wanacho fanya juu ya wanawake hasa katika masuala ya kiimani ?
 
Back
Top Bottom