Mara yako ya mwisho kupiga kura ilikuwa mwaka gani? Kwanini?

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,116
Kuna watu wamepoteza ari ya kupiga kura kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu.

Wapo wanaosema waliacha kwa kuwa hawana imani kama kura wanazipiga ndizo zinaamua mshindi, wanaona kama uchaguzi ni kiini macho tu hivyo wamekata tamaa ya kushiriki.

Wengine wakidai wanajichosha kwenda kuwachagua, viongozi ambao hawatekelezi mambo waliyoahidi hivyo wameokata tamaa ya kwenda kuwachagua.

Kila mtu aliyakata tamaa ya kushiriki zoezi zima la uchaguzi anazo hoja, japo anahitaji kutafakari kwa kina kwani kususia zoezi la uchaguzi ni sawa na kuacha kubeba silaha katikati ya vita, inabidi watu waendelee kupiga kura kutokana na umuhimu wa zoezi hili kwani ni haki yao ya msingi ya kikatiba na pia kuimarisha Demokrasia nchini.

Je, wewe mara yako ya mwisho kupiga kura ilikuwa lini? Kwenye uchaguzi upi?

Ni sababu zipi zilikufanya ikawa ndio mara yako ya mwisho, na jeuna mtazamo gani juu ya zoezi hilo lililombele yetu?
 
Ilikuwa ni 2015. Nilizolewa na upepo wa lowasa
Kituo ni tabata liwiti

Kura yangu nilimpa lowasa ila baadae nikatokea kumkubali lowasa Mpaka nikajuta kwanini kura yangu nisingemuongezea chief magufuli
 
Kuna watu wamepoteza ari ya kupiga kura kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu.

Wapo wanaosema waliacha kwa kuwa hawana imani kama kura wanazipiga ndizo zinaamua mshindi, wanaona kama uchaguzi ni kiini macho tu hivyo wamekata tamaa ya kushiriki.

Wengine wakidai wanajichosha kwenda kuwachagua, viongozi ambao hawatekelezi mambo waliyoahidi hivyo wameokata tamaa ya kwenda kuwachagua.

Kila mtu aliyakata tamaa ya kushiriki zoezi zima la uchaguzi anazo hoja, japo anahitaji kutafakari kwa kina kwani kususia zoezi la uchaguzi ni sawa na kuacha kubeba silaha katikati ya vita, inabidi watu waendelee kupiga kura kutokana na umuhimu wa zoezi hili kwani ni haki yao ya msingi ya kikatiba na pia kuimarisha Demokrasia nchini.

Je, wewe mara yako ya mwisho kupiga kura ilikuwa lini? Kwenye uchaguzi upi?

Ni sababu zipi zilikufanya ikawa ndio mara yako ya mwisho, na jeuna mtazamo gani juu ya zoezi hilo lililombele yetu?
Kura yangu ya kwanza ni kwa mbowe 2005 na kura yangu ya pili ni kwa Magufuli 2015.
Nitapiga kura tena siku atakapo gombea mtu atakaye vaa viatu vya Magufuli, hii sio leo wala kesho ila ipo siku Magufuli atarudi kwa namna nyingine.
 
Back
Top Bottom