Kama tumekata tamaa kiasi hiki kwenye suala la kupiga kura, kuna matumaini ya kupata viongozi bora?

Precious Diamond

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
397
993
Wakuu,

Haya ni baadhi ya majibu kutoka kwenye uzi huu;

Kwanini hupigi kura licha ya kuwa una sifa zinazokuruhusu kufanya hivyo?

Majibu haya yanaakisi majibu ya wengi juu ya zoezi la kupiga kura na kuwachagua viongozi bora kwa maendeleo ya nchi.

Kama haya ndio majibu ya wengi wetu, ina maana tumekata tamaa tunasubiri muujiza? Kama sio, tunatakiwa kufanya nini ili zoezi la kura lisiwe tu jambo la kukamilisha ratiba, badala yake iwe nafasi ya kupata viongozi bora kwa maendeleo ya taifa?

Kumbuka sisi tunaolalamika ndio tupo kwenye Tume kama wafanyakazi, ndio tunaotetea vyama vyetu vishinde hata kama tunaona havifai, ndio tuna mapenzi na mtu kiasi cha mgombea kujihakikishia ushindi, ndio tunatumika kuiba kura, ndio tunaotumika kuanzisha vurugu nk.

Ni kweli hakuna cha kufanya?

Kama mshindi anajulikana kwanini ujihangaishe?

Foleni ya kupanda Mwendo Kasi inatutosha bwashee

Sina muda wa kupanga foleni kuchagua kiongozi asiyeweza kushinda.

Napanga foleni kupiga kura halafu niliyemchagua akishinda baada ya mwaka anahamia chama kingine kuunga mkono juhudi!

Tume ya uchaguzi inaundwa ma Rais, ambae kama sio anatetea kiti chake basi chama chake kimesimamisha mgombea, halafu matokeo ya Urais yakitangazwa hayapingiki popote, sasa ya nini nikapoteze muda wangu kituoni?

Nimeapa kutokupiga kura kwa sababu kuu tatu;

1. Nimegundua pasipo na shaka kura yangu haiheshimiwi, maana mshindi anaamuliwa na mamlaka badala ya mimi mpiga kura!

2. Tume ya uchaguzi siyo huru! Wateule karibia wote wanateuliwa na Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama tawala.

3. Marokeo ya Rais hayawezi kupingwa na chombo chochote kile cha kisheria, hata kama ni batili/yamepikwa.

Kwa sababu napoteza muda tu kuanzia kujiandikisha mpaka siku ya kupiga kura ilhali mimi kula yangu mpaka nitoke niangaike ndio nipate!

Kwahiyo siwezi acha familia yangu iteseke niende kupiga kura.
 
Wakuu,

Haya ni baadhi ya majibu kutoka kwenye uzi huu;

Kwanini hupigi kura licha ya kuwa una sifa zinazokuruhusu kufanya hivyo?

Majibu haya yanaakisi majibu ya wengi juu ya zoezi la kupiga kura na kuwachagua viongozi bora kwa maendeleo ya nchi.

Kama haya ndio majibu ya wengi wetu, ina maana tumekata tamaa tunasubiri muujiza? Kama sio, tunatakiwa kufanya nini ili zoezi la kura lisiwe tu jambo la kukamilisha ratiba, badala yake iwe nafasi ya kupata viongozi bora kwa maendeleo ya taifa?

Kumbuka sisi tunaolalamika ndio tupo kwenye Tume kama wafanyakazi, ndio tunaotetea vyama vyetu vishinde hata kama tunaona havifai, ndio tuna mapenzi na mtu kiasi cha mgombea kujihakikishia ushindi, ndio tunatumika kuiba kura, ndio tunaotumika kuanzisha vurugu nk.

Ni kweli hakuna cha kufanya?
Si kila kiongozi aliyechaguliwa kwa kura za wananchi ni KIONGOZI BORA. Kuna uwezekano mkubwa ukamchagua kiongozi bomu na kumuacha kiongozi mzuri kwa maendeleo.
Kuna nchi ina chama kimoja tu, lakini leo mpaka leo hii ni moja kati ya tatu bora Duniani.

Ngoja nisimalize utamu, maana kuna mifano lukuki ambayo hata mwenyewe unaijua. Alamsik!
 
Hakuna mifano mizuri kwa wenye mfumo kwa wetu? Wao wamefanyaje na sisi tunakwama wapi?
 
Ni mpumbavu pekee ndio atapoteza muda kwenda kupiga Kura kwenye taifa hili.Tanzania hakuna uchaguzi bali ujinga wa mtu mweusi kwenye sanduku la Kura.
 
Sasa Mkuu usipopiga kura utampata wapi kiongozi unayemtaka? Na utapata wapi nguvu ya kulalamika akija asiyemtaka wakati hukutaka kushiriki kuchagua?
Ninaemtaka hajawahi kushinda hata akishinda. Na tulishaambiwa hata tukipiga kwingine, wengine watatengeneza serikali. Sasa nahangaikia nini!! Bora huo muda nikauze visheti vyangu.
 
Ni kwasababu kati yetu kuna wapumbavu wanaoendekeza maslahi yao mbele bila kufikiria wengine. Lakini ndio kusema tumeshindwa kuwabadilisha hawa kabisa kuwatoa tongotongo wakaona ukweli?
 
Wakuu,

Haya ni baadhi ya majibu kutoka kwenye uzi huu;

Kwanini hupigi kura licha ya kuwa una sifa zinazokuruhusu kufanya hivyo?

Majibu haya yanaakisi majibu ya wengi juu ya zoezi la kupiga kura na kuwachagua viongozi bora kwa maendeleo ya nchi.

Kama haya ndio majibu ya wengi wetu, ina maana tumekata tamaa tunasubiri muujiza? Kama sio, tunatakiwa kufanya nini ili zoezi la kura lisiwe tu jambo la kukamilisha ratiba, badala yake iwe nafasi ya kupata viongozi bora kwa maendeleo ya taifa?

Kumbuka sisi tunaolalamika ndio tupo kwenye Tume kama wafanyakazi, ndio tunaotetea vyama vyetu vishinde hata kama tunaona havifai, ndio tuna mapenzi na mtu kiasi cha mgombea kujihakikishia ushindi, ndio tunatumika kuiba kura, ndio tunaotumika kuanzisha vurugu nk.

Ni kweli hakuna cha kufanya?
Hayo majibu yote ndivyo wanavyoamini watu wote wenye umri wa kupiga kura !
Ila hiyo ya kusema anaenda kutafuta kula yake badala ya kwenda kupiga kura hiyo haina mashiko .
Bila Katiba mpya bora ! Watu wataendelea kupungua katika kupiga kura kila uchaguzi !!
 
Back
Top Bottom