Vitambulisho vya NIDA ndio vitumike kupiga kura wakati wa Uchaguzi

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,861
Kamati ya Uchaguzi wa Taifa (NEC), inatakiwa ishirikiane na mamlaka ya utambulisho wa utaifa (NIDA) katika mchakato wa upigaji kura.

NIDA wanatumia finger print sambamba, na wanachukua taarifa mbalimbali za watu. Hivyo mtu aruhusiwe kupiga kura kwa NIDA na vitambulisho vya kura vifutwe. Na kwa sababu namba ya NIDA ni moja tu, basi mpiga kura aruhusiwe kupiga kura mahali popote kwenye kituo chochote cha kupigia kura Tanzania na kwa wale wa nje ya nchi ubalozini.

Ukipiga kura mfumo uoneshe tayari umeshapiga kura kwa kutia dole gumba (fingerprint) wakati una-confirm ili kuingia kwenye chumba kupiga hili kuepusha mtu kupiga kura mara nyingi au kumpigia mtu mwingine kura.

Pia itasaidia kuepusha wizi wa kura kwa wale wanaopenda kuja na maboksi ya ziada ambayo yana kura zilizochakachuliwa. Hivyo ukitaka kupiga kura unakuwa na Muda yako, unaponyeza kitufe cha mashine ya fingerprint inakubali kwa kuwasha taa ya kijani kwamba wewe ni mtanzania na haujapiga bado kura hivyo unaruhusiwa kuingia ndani kupiga kura, kama wewe sio mtanzania au ulishapiga kura basi mashine itawaka taa nyekundu kukutalia, na kwa wale ambao wataenda kuwapigia kura wenzao ukiweka fingerprint yako basi mashine itasema wewe sio muhusika.

Mashine hiyo itatumika kuhesabu idadi ya fingerprint zilizoruhusiwa kwenda kupiga kura zikiwa na namba ya NIDA... Hivyo idadi ya waliopiga kura ndio idadi hiyo hiyo itatangazwa kwenye vituo hivyo baada ya uchaguzi. Huku CCTV zikifungwa hili ikitokea changamoto basi wanatazama kupitia CCTV.
 
Kamati ya Uchaguzi wa Taifa (NEC), inatakiwa ishirikiane na mamlaka ya utambulisho wa utaifa (NIDA) katika mchakato wa upigaji kura.

NIDA wanatumia finger print sambamba, na wanachukua taarifa mbalimbali za watu. Hivyo mtu aruhusiwe kupiga kura kwa NIDA na vitambulisho vya kura vifutwe. Na kwa sababu namba ya NIDA ni moja tu, basi mpiga kura aruhusiwe kupiga kura mahali popote kwenye kituo chochote cha kupigia kura Tanzania na kwa wale wa nje ya nchi ubalozini. Ukipiga kura mfumo uoneshe tayari umeshapiga kura kwa kutia dole gumba (fingerprint) wakati una-confirm ili kuingia kwenye chumba kupiga hili kuepusha mtu kupiga kura mara nyingi au kumpigia mtu mwingine kura.

Pia itasaidia kuepusha wizi wa kura kwa wale wanaopenda kuja na maboksi ya ziada ambayo yana kura zilizochakachuliwa. Hivyo ukitaka kupiga kura unakuwa na Muda yako, unaponyeza kitufe cha mashine ya fingerprint inakubali kwa kuwasha taa ya kijani kwamba wewe ni mtanzania na haujapiga bado kura hivyo unaruhusiwa kuingia ndani kupiga kura, kama wewe sio mtanzania au ulishapiga kura basi mashine itawaka taa nyekundu kukutalia, na kwa wale ambao wataenda kuwapigia kura wenzao ukiweka fingerprint yako basi mashine itasema wewe sio muhusika. Mashine hiyo itatumika kuhesabu idadi ya fingerprint zilizoruhusiwa kwenda kupiga kura zikiwa na namba ya NIDA... Hivyo idadi ya waliopiga kura ndio idadi hiyo hiyo itatangazwa kwenye vituo hivyo baada ya uchaguzi. Huku CCTV zikifungwa hili ikitokea changamoto basi wanatazama kupitia CCTV.
Haya ni mapendekezo yako au ya NEC ?
 
Vitambulisho vya nida hatuna
Namba ya NIDA itumike, na fingers mashine hili kuja kama ni wewe kweli.... Kama unavyoenda kusajili Laini ya simu na namba ya NIDA ila msajili laini tayari anapata taarifa zako
 
Wazo zuri sana. Shida inakuja watu wengi wa shughuli za mikono fingerprint hazisomi.
 
Wazo zuri sana. Shida inakuja watu wengi wa shughuli za mikono fingerprint hazisomi.
Lazima kuwe na alternative... Either watumia facial recognition mashine kwa sababu picha tayari hipo Nida.

Simu zenyewe hizi za smartphone zina fingerprint na Facial recognition... Yani ukiweka sura tu simu inafunguka hata uwe umepaka mkorogo sijui umenyoa umesuka inafanya kazi, ukiweka fingerprint bado simu inafunguka, Infinix, Tecno zinamfumo huo, serikali nayo lazima ije na alternative, Yani njia mbadala watumie face recognition kama fingerprint ikikataa... hakuna kinachoshindikana kukutambua ulimwengu wa leo
 
Kuna watu wamejiandikisha toka 2017 hadi leo hawana kitambulisho cha NIDA sasa si ndo hawata ruhusiwa kupiga kura mleta mada?
 
Ni idea nzuri yenye kujenga ila CCM hawata kubali uchaguzi ulionyooka wao ndio wako nyuma ya wizi wa ballot.
 
Back
Top Bottom