October
JF-Expert Member
- Oct 5, 2009
- 2,145
- 92
Nimekua nikitafakari Wimbo wetu wa taifa nikabaini kua una mapungufu kadhaa ambayo aidha yangetakiwa yarekebishwe au kutafuta wimbo mbadala.
Kwanza wimbo huu si wimbo wenye asili ya Tanzania ni wimbo tulioiga kutoka Afrika Kusini. Nionavyo mimi hii si dalili nzuri kuiga wimbo wa taifa na kutumia wimbo ambao hauna asili ya nchi unayoiwakilisha. Sidhani kama Tanzania tumekosa ubunifu kiasi cha kuiga wimbo wa nchi nyingine. Kuna sababu gani ya msingi kungiwa wimbo na wazulu?
Pili naona kwamba wimbo wetu haumjali mtanzania na wala haumpi kipaumbele hata kidogo, Hii inadhihirishwa na ukweli kwamba mambo baraka kwa mtanzania zimetajwa katika beti la pili, badala ya kuwa Beti la kwanza. Hii ni aibu na laana kwa watanzania. Tunajilaani wenyewe kwa kuwajali wageni kuliko sisi watanzania. Bahati mbaya hali hii imekua kama self fulfilling prophecy, ndio maana wageni wanatetemekewa na wenyeji wanaonekana mafala ndani ya nchi yao.
Huu wimbo umepitwa na wakati, Unazungumzia kudumisha uhuru wakati hakuna nchi inyotawaliwa sasa hivi. Ilikua sawa wakati wa kupigania uhuru na kipindi cha ujamaa kuwa na wimbo kama huu lakini sasa mambo yamebadilika, nchi zote zimejikomboa, wale tuliojipendekeza kuwasaidia kupigania uhuru wameshapata uhuru wao, hawatujali wala kututhamini na huku sisi tunaendeleza wimbo wa enzi hizo.
Vilevile naona wimbo huu haumjengei mtanzania mapenzi na nchi yake, haumfanyi mtu kuwa proud na nchi yake. Hakuna kitu chochote kinachozungumzia uzuri wa nchi yetu wala uzuri wa watanzania au ushujaa wa watanzania….hakuna.
Naomba tuendeleze mapungufu ya wimbo huu...
Napendekeza wimbo wa ‘Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote….' ukifanyiwa marekebisho kidogo ungefaa zaidi