Wimbo wa Taifa unazidi kupoteza maana kwa viongozi na wananchi

Kiranja wa jamii

JF-Expert Member
Jan 2, 2023
222
528
Nakumbuka zamani miaka ya mwishoni mwa 90's na hadi mwanzoni mwa miaka ya 2000's jamii ya watanzania walikuwa wanaheshimu sana wimbo wa Taifa hasa hasa panapokuwa na tukio la kitaifa.

Wimbo wa Taifa ukiimbwa watu wote walisimama wima huku mikono yao ikiwa imekunjwa ngumi ya "kike" na kushushwa chini na wote (wengi) waliimba kwa sauti ya juu na kutamka maneno ya wimbo huo barabara kabisa na hata waliopita mita chache ya eneo ambalo wimbo ulikuwa unaimbwa walilazimika kusimama wima.

Kadiri siku zinavyoenda, siku hizi kwenye matukukio ya kitaifa ambayo na viongozi waliopaswa kuhimiza heshima ya wimbo wa Taifa ma DJs ndio wenye jukumu la kuplay wimbo na hakuna sauti za wananchi zinazosikika. Wanasimama huku midomo ikiwa imefumba kana kwamba hawaujui wimbo huo.

Sambamba na hilo, usimamaji wa wima sio lazima wala muhimu, hakuna utulivu na wanaopita karibu na eneo panapoimbwa wimbo wa Taifa hakuna anayejali. Watu wanaendelea na safari zao.

Tabia hii inazidi kujengeka na kuzoeleka kiasi kwamba kuna wasiwasi kama juhudi hazitachukuliwa wimbo wa Taifa utabaki kuonekana kama nyimbo za wasanii wengine na umuhimu wake utapotea.

Naamini wananchi wengi wanaufahamu wimbo wa Taifa vizuri kabisa hivyo sioni sababu ya ku play wimbo badala yake waachwe watu waimbe wenyewe ili kutopoteza umuhimu na kuendelea kuwafanya wananchi wathamini na kuheshimu wimbo wa Taifa.

Kama issue ni kuongeza ladha na kuboresha, ni vizuri DJ a play biti ya blass band tu kwa sauti ya chini ili kuruhusu sauti za wananchi kusikika vizuri na kwa ufasaha kwasababu katika Taifa lililohai wimbo wa Taifa ni nembo ya msingi wa Taifa husika. Kuendelea kuwazoesha wananchi kutoona umuhimu wa wimbo wa Taifa ni kuua Taifa.
 
Hivi hakuna uwezekano wa kuuboresha ule wimbo wa Tazama ramani....., au ule wa Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote.... ili mmoja wao ndiyo uwe wimbo wa Taifa?

Huu wimbo wa Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania, naona kama vile hauendani kabisa na Tanzania ya sasa. Wimbo hauna hata msisimko wa kujenga moyo wa uzalendo kwa wananchi wa kawaida na viongozi! Na ndiyo maana wahuni wanawaza kuiibia tu nchi.
 
Hivi hakuna uwezekano wa kuuboresha ule wimbo wa Tazama ramani....., au ule wa Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote.... ili mmoja wao ndiyo uwe wimbo wa Taifa?

Huu wimbo wa Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania, naona kama vile hauendani kabisa na Tanzania ya sasa. Wimbo hauna hata msisimko wa kujenga moyo wa uzalendo kwa wananchi wa kawaida na viongozi! Na ndiyo maana wahuni wanawaza kuiiba tu nchi.
Hutaki mungu ambariki Nape, mwigulu, makamba, et al??
 
Hivi hakuna uwezekano wa kuuboresha ule wimbo wa Tazama ramani....., au ule wa Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote.... ili mmoja wao ndiyo uwe wimbo wa Taifa?

Huu wimbo wa Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania, naona kama vile hauendani kabisa na Tanzania ya sasa. Wimbo hauna hata msisimko wa kujenga moyo wa uzalendo kwa wananchi wa kawaida na viongozi! Na ndiyo maana wahuni wanawaza kuiibia tu nchi.
...Wabariki viongozi wake,
Hekima, umoja na Amani....!

1.Hiyo hekima wanayo?
2.Umoja wakati Kila kiongozi anawaza kumchongea mwenzake?
3.Amani imebaki midomoni na njia ya kutafutia Kura.
 
Hutaki mungu ambariki Nape, mwigulu, makamba, et al??
Dah! Mimi huo wimbo siimbi kwa kweli. Maana una kila dalili za kupitwa na wakati, au kuwa irrevant.

Yaani unatuhamasisha tumuombe Mungu awabariki viongozi wetu ambao wengi wao ni wezi, mafisadi, wabinafsi, wachawi, wazinzi, vilaza, miungu watu, majangili, wezi wa kura, wezi wa mali za umma, majangili, wabadhirifu, wahuni, nk.

Mimi hapana aisee.
 
Mtu akipoteza matumaini halafu aheshimu wimbo huku ananjaa tumboni huo utakuwa wimbo au ni miayo tu.
 
Back
Top Bottom