October
JF-Expert Member
- Oct 5, 2009
- 2,145
- 92
- Thread starter
- #21
Lakini pia tatizo kubwa tulilinalo mbele ya watu wa dunia nyingine Ni uafrica kwanza ndipo Tanzania.Yaani ukitaja wewe ni Mwafrica mtu hana haja ya kuuliza nchi gani.Moja kwa moja mtu hategemei jema kutoka kwako.Na hii ni kwasababu Africa tu wamaskini wa kila kitu yaani hadi upendo tunauwana ovyo. Nadhani Mungu akianza kwa kubariki Africa Then Tanzania ni jambo jema zaidi.Kumbuka Tanzania imo Africa kwaiyo mungu anaweza kuanzia hata Tanzania.
Asante kwa hoja zako, Naomba kupingana na wewe, Mimi nadhani ni muhumu kuiweka Tanzania mbele kama tai katika kila kitu, Charity begins at home.
Sijui ni kwa nini tumekua na hii kasumba ya kuwatanguliza wageni na kuona ni wa maana kuliko sisi watanzania wenyewe. Nadhani sisi ndio nchi pekee duniani yenye kasumba hii ya kuthamini wageni kuliko wananchi wake.
Ninaposema hivi simaanishi kuwachukia wageni, La hasha nina maanisha kuwathamini watanzania na kuwaenz, kuwajengea moyo wa uzalendo n.k. Kama sisi wenyewe tusipojithamini ndani ya nchi yetu ni nani atakaayetujali?
Kwa nini unataka Mungu aanza kuibariki Afrika na sio Tanzania? Kwanini asianzie kuibariki Tanzania na baraka zikifurika zimiminikie katika nchi nyingine za kiafrika? Kwanini unadhani sisi hatustahili na wanaostahili ni wengine kwanza? Huoni kwamba wewe umeshajitolea mhanga kubaki maskini kwanza mpaka wengine wapate ndio na wewe upate?