Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,641
- 46,290
Wimbo wa taifa unakuwa mzuri sana pale unapoelezea historia ya taifa husika au unatoa sifa za kipekee za nchi au unapokuwa unahamasisha uwajibikaji/ call for action kwa taifa au vyote vitatu kwa pamoja.
Sasa sisi wimbo wetu unahusisha maombi zaidi mwanzo mpaka mwisho, hauna call for action, historia ya nchi yetu, mwito wa uzalendo au uwajibikaji. Nafikiri nyimbo kama Tazama ramani au Tanzania nakupenda kwa moyo wote zinaweza kutufaa sana. Pia nyingine mpya kabisa zinaweza kutungwa na kuchaguliwa mojawapo.
Au hata huu wa sasa ufanyiwe mabadiliko muhuimu, badala ya kusema Mungu wabariki viongozi wake iwe wabariki WATU wake ili uwe jumuishi. Dumisha uhuru na umoja iongozwe iwe dumisha uhuru, HAKI na umoja ili kuleta msisitizo wa kutendeana haki.
Sisi hatutatukwa wa kwanza kufanya mabadiliko kama haya. Uingereza wao hubadilisha "God save the Queen" na sehemu zote zenye he zinakuwa she wanapokuwa na Malkia kama mtawala, wakipata mfalme wanarudi kwenye "God save the King" na he.
Russia, Canada, Ujerumani na nchi nyingi pia wamewahi kubadilisha au kufanya mabadiliko katika nyimbo zao za taifa