Huu wimbo wa Mfalme Ninja "Sio Mwizi" unatuhukumu Watanzania. Tubadilike tuliokoe taifa letu

Mto Songwe

JF-Expert Member
Jul 17, 2023
6,016
12,302
Moja ya aina ya mziki niliokuwa nautafsiri kama wa kihuni ni pamoja na aina ya huu mziki toka pwani Singeli.

Ila huu wimbo wa Mfalme Ninja uitwao Sio Mwizi kidogo umebadili fikra zangu kwa ujumbe uliopo ndani ya wimbo huu.

Moja ya maneno yanayopatikana katika ngoma hii yanasema" Kuna wizi wa bandari mabilioni ya fedha imegharimu serikali kuwapiga hamjawaweza".

"Chonde usije niua kwa kwa ajili sh. 500 wapo waliochukua zaidi ya Billion 5 kwani hamuwatambui mnajifanya hamuwajui, kwani hamuwatambui ninyi, mnajifanya hamuwajui".


Kweli Watanzania tunahitaji kubadilika maneno haya yamenigusa.

So, far huu ni wimbo wangu bora toka kufungua huu mwaka.
 
Baada ya kuondoka wakoloni,taifa wakaachiwa viumbe ambao walikuwa na upeo mdogo wa kufikili yaani rangi ya ngozi na akili ni vitu Sawa kabisa.
Na baadhi ya viongozi walisomeshwa na wakoloni England wakakabidhiwa madaraka hata drainage system kwenye mitaa ziliwashinda kujenga
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom