Mapokezi ya Heche na ToneTone yavunja rekodi Mbeya

Mapokezi ya Heche na ToneTone yavunja rekodi Mbeya

Duh, Chadema ikiitisha maandamano sijui itakuaje.
 
View attachment 3614894
View attachment 3614895
Kwa namna ambavyo Serikali imeudharau mkoa wa Mbeya ambao ndiyo unalisha nchi kwa chakula na ambayo ndiyo lango la kwenda Zambia, DRC na Malawi, naungana na wana Mbeya Kuchangia ToneTone. Cc Erythrocyte, ChoiceVariable
Nimetoa alama ya "nzuri" kwenye mada hii, specifically si kwa namna mwonekano wa wanaMbeya wanavyoonyesha mwamko wao kwa ukombozi wa taifa hili, alama hiyo "nzuri" imechagizwa na aliyeleta mada yenyewe na kuweka hizo picha.

Tumesutana sana humu JF katika wakati mgumu sana walipotufikisha hawa watawala waovu. Kama hujashiriki kumuua mTanzania kwa mikono yako mwenyewe na kusherehekea tendo hilo....

Sitaki kusema sasa hivi kwamba tugange yajayo; bila ya kujutia yaliyoingia moyoni na akilini...

Tuendelee mbele waTanzania, nchi yetu itarudi mikononi mwa waTanzania wenyewe karibuni.
 
Kudharau baadhi ya Sehemu sio mbeya tu ni sehemu Nyingi.

Solution hapa ni Serikali ya Majimbo.
Wakuu wa .mikoa wakichaguliwa itakuwa vizuri na kwenue katiba kuwe na alocation of fund za maendeleo kwa kila mkoa na mkuu wa mkoa awajibike kwa wananchi.
Tuwe pia na district attorneys wa kichaguliwa ndio wawe waendesha mashtaka amba hawateuliwi ila wachaguliwe na wanachi wa sehemu husika hivyo hawataonea watu maana wanajua hawatachaguliwa.
 
Kuliko kumpigia kura yule kigagula Tulia Ackson au huyu Patrick Mwalunenge, nitampigia kura mpinzani yeyote atakayetokea. Haya mazezeta siyataki tena.

Eti Jiji la Mbeya likikuwa na Naibu Spika 2015-20 halafu Spika 2020-25, na Spika ndiyo boss wa Wabunge wote na uwaziro wao. Ameshindwa kuifanya Mbeya ipate kilomita 22 zabbarabara ya lami?

Kwa sasa Urambo na Makambako ziapendeza kuliko Mbeya
Seriously mie nilikuwa nakusoma toka kitambo hiyo ulikwa mwanamabadiriko. Nilikuambia wewe jamaa ni kama unauma na kupuliza ila ukisoma between the lines wewe ni mpinzani ndakindaki. Ila baadae ukaja kwa kasi sana kuwatetea wauaji wa watanganyika, dah! nikawa najiuliza mbona huyu mshikaji hakuwa hivi? Nini kimempata. Hatimaye leo umerudi kwenye asili yako. Asili haijifichi boss, karibu tena kuwasemea wanyonge, japo tunajua impact yetu hapa JF sio kubwa lakini bora kidogo kuliko kukosa kabisa
 
Tatizo CCM wanaiba kura vibaya mno
Yaan Tume ya Uchaguzi inarundika kura kwa CCM

Hakuna mwaka CCM wamewashinda Chadema kwa ufuasi na wingi wa watu kwenye mikutano, lakini siku zote CCM wameibuka na ushindi wa kishindo!

Mwaka jana tu 2025 kwenye uchaguzi mkuu CCM waliondoka na kura milioni 28 na asilimia 98; CCM hawatishwi na wingi wa watu wanawaunga mkono Chadema, wanaogopa Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi tu; na hawataruhusu katiba mpya, Tume huru ya uchaguzi , na sheria zinazotoa usawa kwenye chaguzi zetu.

Vv
 
View attachment 3614894
View attachment 3614895
Kwa namna ambavyo Serikali imeudharau mkoa wa Mbeya ambao ndiyo unalisha nchi kwa chakula na ambayo ndiyo lango la kwenda Zambia, DRC na Malawi, naungana na wana Mbeya Kuchangia ToneTone. Cc Erythrocyte, ChoiceVariable
Hiki unachosema sio unapenda, bali ni ukweli ulioshindwa kuuficha. Kwa hiki kinachoendelea sasa, cdm wamefanikiwa kuondoa dhana lukuki ikiwemo chama bila ruzuku hakiwezi kufanya shughuli zake. Na ile dhana kuwa bila kushiriki uchaguzi chama kinajifia, dhana hii imekufa rasmi, kuwa chama cha siasa sio ruzuku bali ni uungwaji mkono wa wafuasi wake. Kwa sasa cdm wamegawa wananchi, kiasi kuwa ccm itabidi wajishike sana na vyombo vya dola, kinyume na hapo itaenda kuishi kaburi moja na KANU ya Kenya.
 
Nimetoa alama ya "nzuri" kwenye mada hii, specifically si kwa namna mwonekano wa wanaMbeya wanavyoonyesha mwamko wao kwa ukombozi wa taifa hili, alama hiyo "nzuri" imechagizwa na aliyeleta mada yenyewe na kuweka hizo picha.

Tumesutana sana humu JF katika wakati mgumu sana walipotufikisha hawa watawala waovu. Kama hujashiriki kumuua mTanzania kwa mikono yako mwenyewe na kusherehekea tendo hilo....

Sitaki kusema sasa hivi kwamba tugange yajayo; bila ya kujutia yaliyoingia moyoni na akilini...

Tuendelee mbele waTanzania, nchi yetu itarudi mikononi mwa waTanzania wenyewe karibuni.
Labda umechelewa kunielewa, mimi napenda amani itawale ni sikubali kudai haki katika misingi ya uvunjifu wa amani.

Non-violence is a weapon of the strong.- (Mahatma Gandhi)
 
Mkiulizwa matumizi mnamsingizia CAG!
Komaeeni wafadhili wamekatika baada ya kutakiwa maelezo kwenye miamala yao
 
Seriously mie nilikuwa nakusoma toka kitambo hiyo ulikwa mwanamabadiriko. Nilikuambia wewe jamaa ni kama unauma na kupuliza ila ukisoma between the lines wewe ni mpinzani ndakindaki. Ila baadae ukaja kwa kasi sana kuwatetea wauaji wa watanganyika, dah! nikawa najiuliza mbona huyu mshikaji hakuwa hivi? Nini kimempata. Hatimaye leo umerudi kwenye asili yako. Asili haijifichi boss, karibu tena kuwasemea wanyonge, japo tunajua impact yetu hapa JF sio kubwa lakini bora kidogo kuliko kukosa kabisa
Tunapishana pale tu tunapitafuta haki kwa kutumia vurugu, na mimi siyo muumini wa kambi hiyo.

Passive resistance is a method of securing rights by personal suffering; it is the reverse of resistance by arms. -Mahatma Gandhi)
 
Kwenye maendeleo ya nyumbani kwetu sina itikadi. Kwanza naiunga sana sera ya CHADEMA ya majimbo kuliko huu ujinga wa pato lote la taifa kugawanywa hadi kwenye mikoa isiyo na productivity
Kwenye maendeleo ya nyumbani kwa wengine ndo una itikadi?
 
Kwenye maendeleo ya nyumbani kwa wengine ndo una itikadi?
Sasa kama Mbeya inazalisha 6% ya GDP (Pato ghafi la Taifa) ikiwa nyuma ya Dar, Arusha na Mwanza halafu Serikali inakwenda kujenga mikoa ya wavivu kama Tabora, Mtwara na Ruvuma au Dodoma, kwanini niunge hiyo itikadi mbovu??
 
Back
Top Bottom