Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,494
- 113,590
- Thread starter
- #301
Mkuu Maalim Mohamed Said, hakuna popote niliposema kuwa Zanzibar kuna watu hawastahili kuwapo ndani ya visiwa vile!.Pasco,
Kipi kinachokufanya wewe uamini kuwa Zanzibar kuna watu
hawastahili kuwapo ndani ya visiwa vile?
Ikiwa kufungua uzi wa kuufungua uzi ni wewe tujadili hili la
nani ni raia wa Zanzibar na nani si raia.
Nilichosema huko nyuma na nina sema tena na tena, Zanzibar ina wenyewe halisi Wazanzibari, waliokuwa chini ya Utawala wa Mwinyi Mkuu!, na Zanzibar ina wageni waalikwa, utawala wa Sultani, uliokaribishwa na Mwinyi Mkuu ili kumdhibiti Mreno asiviteke visiwa hivyo!.
Huyo mgeni mwalikwa, Sultani baada ya kukaribishwa kwa kazi maalum tuu, ile kazi ilipokamilika, yeye alihamia jumla!, sii yeye tuu bali na kuhamisha makao makuu ya ufalme wake toka Bara Arab nchi ya Oman na kuihamishia bara la Afrika katika visiwa vya Zanzibar, yeye sasa sio mgeni mwalikwa tena, sasa yeye ndio akawa mtawala wa Zanzibar na sii tena Mwinyi Mkuu!.
Kwa kadri miaka ilivyopita, ukoo wa Sultani mgeni na wote aliokuja nao, wakazaliana na kuzaliana na kuzaliana hadi kuwa wengi ajabu!. Wageni wote hawa waliozaliwa Zanzibar sii Waarabu tena bali wote ni Wanzanzibari wenye asili ya Waarabu, na muingiliano na wenyeji, ukatengeneza kizazi chengine cha machotara ambao nao ni Wazanzibari pia!. Ulifikia wakati wageni wote waliokuja kutoka Omani, waliishatangulia mbele ya haki, na wazaliwa wao wote waliofuatia, wamezaliwa Zanzibar, hivyo kwa kizazi kilichopo, na utawala uliopo waliamimi visiwa hivyo ndio kwao, ndio mali yao na kuvitawala ni haki na halali yao, tena hawa waliopo hawakuijua habari ya Mwinyi Mkuu wala kujua kulikuwa na makubaliano gani kati ya Mwinyi Mkuu kumkaribisha Sultani na kumpisha kiti!.Waliopo maadamu wamezaliwa Zanzibar na wamezaliwa katika ukoo wa Sultani, kwao Zanzibar ni kwao, Zanzibar ni yao na kila kilichomo ni mali yao!, hivyo na kuitawala milele ni halali yao!.
Katika miaka hiyo, pia kizazi cha wenyeji ukoo wa Mwinyi Mkuu na watu wao, wenye Zanzibar yao, kiliendelea kuzaliana na kuongezeka!, kikafikia kipindi zile sababu zilizomfanya Mwinyi Mkuu kuwakaribisha wageni kuja kuitawala Zanzibar, hazikuwepo tena!. Hakuna ajuaye makubaliano kati ya Mwinyi Mkuu na Sultan Sayyed Said yalikuwaje!. Hivyo wenye Zanzibar yao wakaanza kuhoji na kuitaka Zanzibar yao kutoka kwa wageni wenyeweji waliojimilikisha visiwa hivyo!.
Jee wajua kiliwakuta nini wajukuu hawa wa Mwinyi Mkuu waliodai haki yao?!, naomba hili nisiliseme humu, likazua mjadala mwingine kwa watu kubaki midomo wazi kwa kutoamimi kuwa binadamu mmoja anaweza kumfanyia unyama wa kiwango hicho binaadamu mwingine, kunaweza kupelekea watu tukaishia kuapizana humu!.
Harakati hizi za wenye chao kuidai haki yao, dhidi ya dhulma ya mgeni mwenyeji aliyepora hali na halali yao, ilifikia mwisho kwa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar!, mwenye chake alichukua kilicho chake mwenye halali nacho, kwa kufanya waliochofanya, huku mgeni mwenyeji aliyeamini na yeye hicho alichonacho nacho ni chake na halali yake, hivyo hicho alichofanyiwa na wenyeji ni dhulma!.
Wakati mmoja anashangilia kurejesha kilicho chake mikononi mwake kwa kuyaita ni Mapinduzi Matukufu, yaliyorejesha hishma ya ukoo wa Mwinyi Mkuu kwenye visiwa hivyo, na kushangilia kwa neno "Mapinduzi Daima" ambayo yalihusisha umwagaji mkubwa wa damu!, mwingine anaililia damu iliyomwaika kwa kuielezea ni dhulma kubwa waliofanyiwa na wamwagaji damu hao!.
Mada yangu ya uzi huu ni shuhuda wa kilichotokea siku hiyo, ambapo wahusika wakuu wote ni Wazanzibari, mpindua na mpinduliwa, sasa kuna watu wanadhani mpinduliwa alitimuliwa toka katika visiwa hivyo!, ukweli ni kuwa hakuna aliyefukuzwa katika visiwa hivyo!, waliovikimbia visiwa hivyo, walikimbia wenyewe!, hawakufuzwa!.
Zanzibar ni ya wote, wenye halali yao, na wageni wakaribishwa ambao sasa sasa nao wamegeuka wenyeji!.
Jumatatu njema!.
Pasco