Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar: Kumbe Waarabu Hawakufukuzwa! Walikimbia Wenyewe - Mzee Sukari

Maturanya

Member
Joined
Sep 10, 2013
Messages
32
Points
95

Maturanya

Member
Joined Sep 10, 2013
32 95
Pasco
Kwanini huupendi ukweli?
Kuwa mkweli japo ukweli wauma!.

Hivi ukaenda Hospitali ukapawa dawa ambazo huzitaki lakini ni kwakuwa tu huzitaki, ila ndo tiba nzuri na si nzuri tu bali yafaa kwa maradhi yako,

Sasa Daktari aogope kukugeiye dawa hiyo kwakuwa weye hutaki?! na ukaulizwa kwanini kutotumia dawa hizi?! Ati sitaki tu maana sizitaki,
Sa huzitaki ilhaal waumia kwa maradhi?

Kunywa ni faida kwako na baadaye utajapata poo kabisa, lakini usivoshukurani waeza keti kimya bila mrejesho ila si kitu, wanzio watakuwa waishayua tatizole nini!!

Ondosha haya, tuambie hapa ya nini kuyaita ......... matukufu?

Paschal Kajibu mara nyingi hili swali mi nafikiri watu waseme kwanini sio matukufu, au muwaulize kwanini wanasema ni matukufu
 

Maturanya

Member
Joined
Sep 10, 2013
Messages
32
Points
95

Maturanya

Member
Joined Sep 10, 2013
32 95
Umejibu kama layman afadhali ungebaki kushangaa pasipo kueleza maana ya uafrika. Umeleta suala jingine la "races" ambalo ni somo tofauti. Hata hivyo, wazo la kuwa kuna dhana au wazo la kuwa na "races" mara nyingi hutumika katika kuwabagua tu binadamu na hutumia kirahisirahisi bila tafaukuri ya kina. Hii ndiyo kusema kuwa, kati ya jamii ya binadamu, suala la "races" halina maana zaidi ya kuwajenga watu dhana ya "kibaguzi". Ieleweke kwamba binadamu wote wanaoishi ni jamii ya "homo-sapiens". Dhana ya "racism" ndiyo pia hupelekea kundi la jamii ya binadamu kujiona ni bora kuliko wengine. Tafakari mfano dhana ya mimi Mhutu na wewe mtutsi ilivyoleta maangamizi. Haya yote ni matokeo yatokanayo na dhana ya "races". Hii dhana haijumuishi tu rangi ya ngozi bali ni tu vingi, vinasaba, lugha, mipaka ya kijografia, nk. Turudi kwenye swali, uafrika ni nini na kuwa mwafrika maana yake nini?
hujamjibu
 

Maturanya

Member
Joined
Sep 10, 2013
Messages
32
Points
95

Maturanya

Member
Joined Sep 10, 2013
32 95
Pasco uambiwe mara ngapi , Nyerere alimkamata Shamte , Waziri Mkuu wa serikali halali ya Zanzibar na kumuweka jela za Tanganyika kabla ya huo uitwao muungano hapo April 26 , 1964.

hujaelewa tu kuwa mapinduzi ni moja ya mikakati ya Nyerere kutekeleza ajenda za kuichukua Zanzibar chini ya uongozi wa kanisa katoliki . ??
Hii ni hoja ya bei rahisi kabisa
 

battawi

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2014
Messages
859
Points
500

battawi

JF-Expert Member
Joined Mar 29, 2014
859 500
Yani tatzo tunapowasema waarabu kwa mabaya yao wao wanahisi tunasema uislamu
Karibu miaka 60 tangu uhuru wa Tanganyika,na Miak57 ya Uhuru wa Zanzibar kisha 56 ya Mapinduzi bado tunaendelea kuwalaumu waarabu,?
Au tunatafuta Uchochoro wa kukwepa ukweli wa kuwaletea neema na kile tulichowaahidi Raia.
Kiwango cha umasikini na Maradhi kila uchao kinakua ,
Maendeleo hayaendani na ongezeko la mahitaji ya Raia wenu,
Chama Tawala kinangangania Madaraka kisultani,
rasilimali zimeshindwa kuwanaufaisha wananchi,
Munalaumiana wenyewe kwa wenyewe eti mikataba feki,wazungu wabaya nk.
Semeni ukweli,
Mbona Viongozi Mukitoka Madarakani Munakuwa Matajiri wa kutupwa?
ACHENI KUANGANYA RAIA NA KULETA VISINGIZIO
 

Remote

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2011
Messages
19,011
Points
2,000

Remote

JF-Expert Member
Joined May 20, 2011
19,011 2,000
Karibu miaka 60 tangu uhuru wa Tanganyika,na Miak57 ya Uhuru wa Zanzibar kisha 56 ya Mapinduzi bado tunaendelea kuwalaumu waarabu,?
Au tunatafuta Uchochoro wa kukwepa ukweli wa kuwaletea neema na kile tulichowaahidi Raia.
Kiwango cha umasikini na Maradhi kila uchao kinakua ,
Maendeleo hayaendani na ongezeko la mahitaji ya Raia wenu,
Chama Tawala kinangangania Madaraka kisultani,
rasilimali zimeshindwa kuwanaufaisha wananchi,
Munalaumiana wenyewe kwa wenyewe eti mikataba feki,wazungu wabaya nk.
Semeni ukweli,
Mbona Viongozi Mukitoka Madarakani Munakuwa Matajiri wa kutupwa?
ACHENI KUANGANYA RAIA NA KULETA VISINGIZIO
Hayo yote hayahalilishi mambo mabaya yaliyofanywa na waarabu
 

battawi

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2014
Messages
859
Points
500

battawi

JF-Expert Member
Joined Mar 29, 2014
859 500
Hayo yote hayahalilishi mambo mabaya yaliyofanywa na waarabu
Sasa nusu karne bado munamtafuta mchawi wa maendeleo yenu.
Tafakuri,acheni kukwepa ukweli.
Karume alijenga viwanda.
Nyerere Alijenga Viwanda.
Kaja Mwinyi nchi hata sembe kwa foleni,maharege yasiyowiva mpaka kwa magadi,Sembe la njano.
Jumbe naye Hali ya biashara ilikufa zanzibar,maduka yalikuwa yanauzwa ndizi mbivu na mkaa.Serikali ikafungua maduka ya chakula(maduka ya ukoo)
Kaja Mkapa kauza viwanda ,
Kaja kikwete kaleta wawekezaji wa Umeme Richmond na Kuleta wawekezaji wa nje wengi .Kaua UDA na kaanzisha Mwendo kasi.Kaanzisha umeme wa gesi na mkaa wa mawe.
Kaja Magufuli ,Serikali inafufuwa viwanda tena,Mwendo kasi unauzwa,Serikali inaanzisha tena Vyanzo vipyza vya umeme,ule wa gesi basi, sasa wa maji.
Kaja salmini kasema Mafuta hakuna Zanzibar,wapinzani waongo.
Kaja Sheni Anajenga Moll Zanzibar,Na anataka kuchimba mafuta,lakini Hana 'sovereignty' kwa hiyo mafita hayachimbiki.

Hiyo ndo nchi yako unayoishi,kila kiongozi huja na Mipango yake binafsi,wote wa chama hicho hicho CCM
kila ajaye huja na Sera yake ,
Hakuna Sera ya Taifa ndomaana wakikaribia kuondoka madarakani ,hukwapua kwapua na kujineemesha wenyewe binafsi na kusepa.
Kisha wakitaka kutafuta Kuungwa mkono dhidi ya wapinzani huleta Storia za chuki za kikoloni.

Hivi bado na wewe ni mateka tuu au na wewe ni mfaidika wa system?
ZINDUKA ,GANGA YAJAYO LISHALOPITA SI NDWELE
Wewe umeshika Waarabu na utumwa,tazama wenzio hawa CCM hawatoki kuomba huko.
 

Attachments:

Remote

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2011
Messages
19,011
Points
2,000

Remote

JF-Expert Member
Joined May 20, 2011
19,011 2,000
Jamani naomba tuelewane kwenye hili tunapowasema waarabu hatuusemi UISLAMU. Hizo unazotaja ni changamoto nyingine na zinahitaji upembuzi wake
Sasa nusu karne bado munamtafuta mchawi wa maendeleo yenu.
Tafakuri,acheni kukwepa ukweli.
Karume alijenga viwanda.
Nyerere Alijenga Viwanda.
Kaja Mwinyi nchi hata sembe kwa foleni,maharege yasiyowiva mpaka kwa magadi,Sembe la njano.
Jumbe naye Hali ya biashara ilikufa zanzibar,maduka yalikuwa yanauzwa ndizi mbivu na mkaa.Serikali ikafungua maduka ya chakula(maduka ya ukoo)
Kaja Mkapa kauza viwanda ,
Kaja kikwete kaleta wawekezaji wa Umeme Richmond na Kuleta wawekezaji wa nje wengi .Kaua UDA na kaanzisha Mwendo kasi.Kaanzisha umeme wa maji mkaa wa mawe.
Kaja Magufuli ,Serikali inafufuwa viwanda tena,Mwendo kasi unauzwa,Serikaliinaanzisha tena Vyanzo vipyza vya umeme,ule wa gesi basi, sasa wa maji.
Kaja salmini kasema Mafuta hakuna Zanzibar,wapinzani waongo.
Kaja Sheni Anajenga Moll Zanzibar,Na anataka kuchimba mafuta,lakini Hana 'sovereignty' kwa hiyo mafita hayachimbiki.

Hiyo ndo nchi yako unayoishi,kila kiongozi huja na Mipango yake binafsi,wote wa chama hicho hicho CCM
kila ajaye huja na Sera yake ,
Hakuna Sera ya Taifa ndomaana wakikaribia kuondoka madarakani ,hukwapua kwapua na kujineemesha wenyewe binafsi na kusepa.
Kisha wakitaka kutafuta Kuungwa mkono dhidi ya wapinzani huleta Storia za chuki za kikoloni.

Hivi bado na wewe ni mateka tuu au na wewe ni mfaidika wa system?
ZINDUKA ,GANGA YAJAYO LISHALIPITA SI NDWELE
Wewe umeshika Waarabu na utumwa,tazama wenzio hawa CCM hawatoki kuomba huko.
 

battawi

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2014
Messages
859
Points
500

battawi

JF-Expert Member
Joined Mar 29, 2014
859 500
Jamani naomba tuelewane kwenye hili tunapowasema waarabu hatuusemi UISLAMU. Hizo unazotaja ni changamoto nyingine na zinahitaji upembuzi wake
SIMPLE MIND DISCUSES PEOPLE,
MIDDLE MIND DISCUSES EVENTS,
GREAT MIND DISCUSES IDEA.
NIMEKUELEWA. endelea kupanda mbegu ya chuki Zanzibar.
 

battawi

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2014
Messages
859
Points
500

battawi

JF-Expert Member
Joined Mar 29, 2014
859 500
Taifa hili limedorora kimaendeleo kwa sababu ya ubaguzi uliojificha.
Hapa nchini Waislamu wanalalamikia mfumo kristo,serikalini.Serikali kimyaaa.
Hivi sasa kuna malalmiko ya harufu ya Ukabila, Serikali kimyaaa.

Kuna malalamiko ya Uwe CCM ndo utapata ajira, kimyaa

Huku zanzibar imeshakuwa kawaida. serikali ,hupati ajira mpaka uwe kada -kimyaaa,
Kila siku za mapinduzi zikikaribia story ni zile zile,waarabu,waarabu huku nchi inapotelea mikoni mwa mkoloni mweusi.

Mbona siku ya uhuru wa tanganyika ikiwadia ,Hayatajwi madhambi ya Muingereza? na Mjerumani?

Aliyewachinja Machifu zaidi ya 50 kwa mpigo?
Leteni basi na stori za kuuwawa mkwawa na boma lake lote kule Iringa,haikuwa Udhalimu ule

Tusikilize keshokutwa 9 Dec siku ya uhuru wa tanganyika.Utasikia Mizinga na gwaride tuu,basi.
Kwa nini?
kwa sababu ya Ule mfumo ulio watukuza Wazungu na kuwaponda waarabu kisa Dini zao ilhali wote ni wakoloni.

Musitupige changa la macho bwana,

Ttusha waelewa .

Msilete za kuleta story za cathedral la Mkunazini Unguja. .
Tanganyika yenyewe hivi sasa imegeuka kuwa Mkoloni Thidi ya Zanzibr
Lukuvi si aisema wazi,"hatuiachii ZNZ kwa sababu wataleta uislamu tusioupenda, na kuwarudisha waarabu".Halafu eti munasema Muungano?
Tumeshawasoma-CHUKI NA UDINI NDO AJENDA ZA WATANGANYIKA WAKRISTO.
 

battawi

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2014
Messages
859
Points
500

battawi

JF-Expert Member
Joined Mar 29, 2014
859 500
Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni kile kinachobakia baada ya kuondoa yote uliyofundishwa darasani.

Kwa mujibu wa Einstein kuna watu wakiondoa yale waliyofundishwa darasani, vichwa vyao vinabaki vitupu. Kitu pekee walichojaza kichwani ni walichofundishwa darasani. Hawa ndio hujisifia vyeti, au idadi ya "digrii" walizonazo. Hawana akili, japo wana elimu.

Einstein alisema hakuna uhusiano kati ya elimu na akili. Kuna watu wana elimu lakini hawana akili, na wengine wana akili lakini hawana elimu. Ni bora uwe na akili ukose elimu, kuliko uwe na elimu ukose akili.

Icons wa Sayansi kama Isaac Newton, Galileo Galilei na Archimedes of Syracuse hawakuwa na elimu yoyote ya cheti, diploma wala degree, lakini walikua na AKILI. Ugunduzi wao mpaka leo unaiongoza dunia.

Akili siku zote ni "superior" kuliko elimu kwa sababu akili ndio ilibuni elimu. Yani watu wenye akili walikaa wakaweka utaratibu wa mtu kukaa darasani na kujifunza kwa kipindi fulani, kisha apimwe kwa mitihani na atunukiwe cheti. Ubunifu huo ulifanywa na wenye akili. Kama huamini jiulize mtu wa kwanza kutunukiwa degree duniani alifundishwa na nani?

So mtu mwenye akili lakini akakosa elimu, ni msaada kwa jamii kuliko mtu mwenye elimu lakini akakosa akili. Mark Zukerberg hakumaliza shule lakini kwa kutumia akili amebuni mifumo rahisi ya mawasiliano kupitia mtandao.

Yeye ndiye mmiliki wa Facebook, Whatsapp na Instagram. Wale maprofesa waliomuona "kilaza" darasani leo wanatumia ubunifu wake kuendesha maisha yao. Kama sio FB basi wanatumia Instagram au Whatsapp. Maprofesa wenye elimu kubwa wamezidiwa ujanja na "kilaza" mwenye Akili.

Usijidharau kwa uchache wa madarasa ulionayo, unaweza kuwa na akili nyingi kuliko mwenye degree 4.

Kumbuka Einstein alisema akili ni kile kinachobakia baada ya kuondoa yote uliyofundishwa darasani. Jiulize ukiondoa yale uliyofundishwa darasani unabaki na nini? Yani ukiondoa hiyo diploma, degree au PhD unayojivunia, kichwa chako kinabaki na nini?

Kama kuna kitu kinabakia basi hicho kinachobakia kinaitwa "AKILI". Na kama hamna kinachobakia basi hilo bichwa halina tofauti na mtungi wa gesi.
 

doriani

Member
Joined
Nov 24, 2019
Messages
39
Points
125

doriani

Member
Joined Nov 24, 2019
39 125
Battawi. Ukweli fitna zinatoka Bara kuja Zanzibar. Hawa watanganyika ndio chimbuko la fitna yetu. Na hivi sasa wameshakamata serikali na kwenye nafasi nyeti na hivi sasa wanataka kufanikisha kuwepo na Serikali moja. Maana Turufu za Chama cha CCM hivi sasa ni wale wanachama wao wenye uhusiano wa pande mbili baba Tanganyika mama Zanzibar au kinyume chake maana hawa wanaweza kupigania nafasi yoyote kama sharia inavyotaka mmoja wa wazi I wako wawili awe amezaliwa pale. Mfano mzuri ni mtoto wa Mwinyi Tanganyika yupo na Zanzibar yupo watu wa aina hii ndio Turufu nzuri za Chama. Wale CCM baba zao na Mama zao wote ikiwa wametokea Zanzibar wana nafasi ndogo sana hivi sasa. Kwa hivyo CCM Zanzibar imegawika kweli kwa Sera hiyo ya sasa hivi.
 

bopwe

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2013
Messages
1,700
Points
2,000

bopwe

JF-Expert Member
Joined Oct 1, 2013
1,700 2,000
Katika moja ya hotuba zake za Hadhara Abeid Aman Karume mzaliwa wa Malawi na mama Congo alinukuliwa akisema tuta wahilikisha waraabu walobaki hadi Kwa Zanzibar Mwarabu awe tunu..akasisitiza kwa sauti yake akitoa mfao..Mwaraaaaabu yuuuule yaani kama umeona nyota ya jaha.
Lakini Mungu mkubwa
 

Forum statistics

Threads 1,380,556
Members 525,826
Posts 33,774,581
Top