Mapinduzi Day: Maswali ya Mapinduzi Yasiyojibika

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,918
30,259
KUTOKA JF MAPINDUZI DAY MORNING TRUMPET: YALE AMBAYO SIKUYASEMA

Nimekuwa nikishambuliwa kwa maneno makali nikilaumiwa kuwa nilikuwa nakwepa maswali niliyokuwa nikiulizwa mtangazaji wa AZAM TV kijana Kennedy.

Kweli nilikuwa nayakwepa baadhi ya maswali yake kwa kumtahadharisha kuwa historia ya Zanzibar si nyepesi kuelezeka kama anavyodhani.

SWALI: MAISHA BAADA YA MAPINDUZI

Jambo la kwanza katika mapinduzi ni damu iliyomwagika pasi na sababu wakati wa mapinduzi na baada ya mapinduzi.

Vigumu kwangu kujibu swali hilo kwa kueleza kuwa kwa mara ya kwanza baada ya mapinduzi Zanzibar ilijikuta ina jela za mateso na mauaji.

Haya yalikuwa mambo mapya kwa Wazanzibari.

Masultani walitawala lakini wameondoka hawana damu zinazotiririka katika vidole vyao.

Ningeweza pia kueleza kuhusu chaguzi sita zilizofanyika Zanzibar baada ya kurejeshwa vyama vingi na matatizo yanayogubika chaguzi hizi na damu zilizomwagika katika kila uchaguzi.

Ningeweza nikauliza kama marais wote waliotokana na chaguzi hizi kweli walishinda au walichukua uongozi kwa nguvu za silaha?

Ningeweza nikaeleza hayo na kuhitimisha kwa kuuliza wapi ulipo utukufu wa mapinduzi na uhalali wa serikali.

Si kila swali linajibiwa.

1705169778339.png

Mwandishi na vitabu vya historia ya mapinduzi Azam TV​
 
Back
Top Bottom