Mapenzi na ukabila.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapenzi na ukabila....

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Lizzy, Aug 4, 2011.

 1. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #1
  Aug 4, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hivi kuna mtu yeyote anaeweza kujitosa hapa akasema na kuthibitisha kwamba kwenye UKOO wake wote hamna wezi..wadada wanaojiuza... wadada warahisi kupatikana...watu wakorofi...wavivu...wambea...wasiojua mapenzi..wanaojali/kupenda pesa (as if hao wapondaji wenyewe hawapendi) ...wahuni ...matapeli...wenye viburi...wenye dharau... wenye sura na mumbo unayoona wewe ni mabaya...wabahili...wachoyo...wanaopenda/oa/olewa kwa pesa n.k achilia mbali kwenye KABILA lake?!Kama wapo ningependa kuwajua ili na sie tusioisha kusemwa kila siku tujifunze toka kwao.

  Ukweli na kwamba tabia ya mtu haitakiwi kuwa defined na wapi alipotoka (hata familia yake) bali na vile alivyo.Stereotypes hua zipo kwaajili ya wale waliotofauti na wanaokua stereotyped...kuwasaidia wale wa nje kuwalebel wenzao vibaya ili wao wajione/hisi kwamba ni bora hata kama sio kweli.Ndio maana hata wazungu (sio wote) bado wanatuona Waafrika kama wanyama..wanaamini hatuna akili japo wapo waaAfrika wenye akili kuliko wazungu wengi tu.Ila hili wazo linawafanya wao wajione wako juu.Kama ambavyo sisi wenyewe tunafanyiana kwanzia nchi na nchi..mkoa na mkoa...kabila na kabila..ukoo na ukoo na hata familia hii na ile.Kwenye swala zima la mapenzi naamini kabisa kwamba kabila haiplay role yoyote...kwahiyo achaneni na habari za sijui kabila hili hivi na lile lile.Kama unamjua mtu personally unaweza kumjudge yeye kwa vile unavyomjua na sio zaidi ya hapo.Pili....kama wewe hukupata experience nzuri na mtu wa sehemu fulani haina maana itakua hivyo hivyo kwa wengine wote.Ndio maana hata mwanamke /mwanaume unayemuona wewe kwamba hafai bado anakutana na mtu mwingine na anapendwa utadhani yeye ndio kila kitu.Kwahiyo waache wenzio nao wapate experience zao....kama wewe hukufanikiwa mwache mwingine nae ajaribu bahati yake.

  Nasema yote haya maana hili swala la kuchambua makabila ya watu humu limezidi na linaboa kwakweli.Sijali kama ni langu au la mtu mwingine....ishu ni kwamba inachosha!!Mbaya zaidi ni kwamba yote mnayosema yanaweza kufanywa na yeyote hata anaetoka nchi nyingine achilia mbali wa kabila tofauti!

  Alafu hivi hamchoki maana pamoja na sifa zote za ajabu ajabu mnazoyarushia haya makabila bado wadada wake wanaolewa SANA na wakaka wake wanaoa SANA ndani na nje ya makabila yao.Bado tu hamjagundua kwamba haisaiidii muachane nayo?!Maana kama ingekua inasaidia for the past few years usingesikia watu wa haya makabila wameoa wala kuolewa!

  Mwisho...kama umempenda mtu na tabia yake inaendana na wewe upendavyo endelea nae...kama makabila ni muhimu sana tafuta wakwenu ili tabia zenu zifanane badala ya kuanza kuchambua ya wengine visivyo.Mapenzi kila mtu anaweza akayajua na kila mtu anaweza asiyajue...yote inategemea wawili wapendanao wanavyoyachukulia.
   
 2. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #2
  Aug 4, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  no comment....................
   
 3. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #3
  Aug 4, 2011
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  vipi kuhusu wale wanaodhani wako juu kumbe hamnazo tena hawavutii na ni vingulu-bange?? tuwahusishe na makabila yao pia?
   
 4. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #4
  Aug 4, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  I believe you spoke from the heart...message sent and delivered, especially to Rejao, et al !
   
 5. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #5
  Aug 4, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  This is the truth and I think the msg sent and accepted if not delivered and noted.
   
 6. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #6
  Aug 4, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Ahsante sana Lizzy kwa kulisemea hili. Laiti hili bandiko lingewekwa kwenye notice board kubwa ili watu wengi walione!!

  Kama ingekuwa enzi zetu na viboko shuleni, watu wanaondekeza hizi mambo walitakiwa kuchanwa njiti (kuchapwa viboko)....Mara nyingi naishia kusoma hayo mambo yao na kubaki mdomo wazi..

  Labda siku moja wataekewa kuwa wamepotoka!
   
 7. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #7
  Aug 4, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Lizzy labda wewe watakusikiliza,mi nshakemea nimechoka.Stereotyping/bashing ni udhalilishaji mtupu na hauna maana yoyote. Mimi nimeamua yangu macho tu nisije tukana mtu bure wakati hata simjui maana huenda akawa mkwe!
   
 8. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #8
  Aug 4, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160

  ...lol...Lizzy asante mdada,...almanusura wangelitaja na langu hapa, walishamaliza kanda ya kaskazini, nyanda za juu kusini, kanda ya kati...wakawa wanaelekea huko mwisho wa reli! Ila, kiukweli pamoja na kulichukia hili, bado ukabila una sehemu kubwa kwenye mahusiano, hasa tunapokwenda tambulisha wachumba makwetu.

  Halikwepeki hili.
   
 9. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #9
  Aug 4, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mbu halikwepeki ila kisiwe kigezo cha kudetermine mapenzi au mahusiano. Na by the way ile ya kucaregorize kuwa watu wa kigoma ni wapenda nanihii au wa rukwa nao ni wapenzi wa njia ya giza au wachagga ni wezi au magogo au wauwaji wa waume au wazaramo wacheza ngoma haitakiwi kuwepo. Maana sio kuwa kwa mmoja ashawahi kufanya hivzo basi wote ni wa hivyo na hawafai kuoa. Kila mmoja ana mapungufu yake na huwezi pata mtu mmoja ambaye ni perfect asilimia mia.
   
 10. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #10
  Aug 4, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Aaaaaaaaaaaarrrrrrqqgggggghhhhhhh.........!!!!!! Kwakweli hii tabia inakera sana tena saaanaaaaaaaa. Cha kushangaza thread zenyewe nyingi ni wanawake tu. Ooooh mara wanawake wa kabila hili, wanawake wa kabila lile, ooooh sijui nini nini.......plus ma brah brah brah brah kibaoooo as if wao ni wasafi sana ebbo!
   
 11. G_crisis

  G_crisis JF-Expert Member

  #11
  Aug 4, 2011
  Joined: Jun 19, 2011
  Messages: 715
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Mwembe wenye matunda ndo hurushiwa mawe!
  Hizo mada za makabila haziwezi isha humu!
  Tena mda sio mrefu utaona thread ya kabila humu
   
 12. First Born

  First Born JF-Expert Member

  #12
  Aug 4, 2011
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 5,315
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  umemaiza yote! tena kwa kukazia na kuonyesha wazi kabisa umechukia kabisa na usingependa madharau ya aina yoyote. nimekupata bibie
   
 13. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #13
  Aug 4, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,713
  Trophy Points: 280
  mamkwe umenenea.........tatizo linabaki kwa wazazi/walezi na mawazo yale ya enzi zile.....wanasahau tabia ni ya mtu sio kikundi cha mtu....hayo ya magogo labda ilikuwa zamani sio waleo ......au wanaua waume kwa ajili ya mali wangapi wanafanya hayo na ukiwauliza watoka wapi utapata majibu tofauti......kilichopo jamii kubadilika hasa wenye mitazamo hasi
  mamkwe usinibanie bana nipo fit kila idara:heh:
   
 14. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #14
  Aug 4, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,173
  Likes Received: 1,177
  Trophy Points: 280
  Lizzy abarikiwe! Nimemaliza.
   
 15. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #15
  Aug 4, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Duh...kwanini tabia binafsi ya mtu ihusishwe na tabia yake kama kabila lake lote haliko hivyo?Alafu pia mtu kujiona yuko juu kama haihusiani na yeye kudharau wengine kuna tatizo gani?Mwache tu ajione ipo siku atagundua kwamba wapo walipo juu yake!!

  Mzee DC kwakweli inachosha na kushangaza kwa wakati mmoja.Yani hamna limit ya vitu ambavyo watu wanaandika hapa bila kufikiria ubaya na chuki wanazojaribu kusambaza.Natamani kweli hilo la kuwatembezea hawa watu mboko lingekua linawezekana!!

  Bishanga nafurahi kwamba umejiamulia kukaa kimya badala ya kubishana na hawa watu maana unaweza jikuta unakasirika bure.
   
 16. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #16
  Aug 4, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  MBU siwezi kukataa kwamba haijalishi maana kuna watu hata rangi ya ngozi tu inaweza kuwa tatizo kwenye mapenzi yao kwahiyo hamna cha ajabu hapo.Ila sasa isiwe njia ya kusakama wengine siku nenda siku rudi kama vile hizo tabia wanazo wao tu!!

  KiSWEET hujakosea ...yani full blah blah!!

  Mkwe hawa watu sijui ni kwamba macho na masikio yao hua yanafungwa hayo mambo yakiwahusu watu wasio wa haya makabila maarufu kwa kuchanwa maana ni kama wanaamini kabisa kwamba kwenye haya makabila tu ndo kuna hizi tabia.
   
 17. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #17
  Aug 4, 2011
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Asante dada! kweli umekereka..
   
 18. Shantel

  Shantel JF-Expert Member

  #18
  Aug 4, 2011
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 2,021
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Duh ni mbaya ila halikwepeki kabisa, nahisi lingeanzia somo kwa wazazi wetu kwanza , maana wao ndio wanaotujaza hii kitu mu kichwa zetu
   
 19. Tulizo

  Tulizo JF-Expert Member

  #19
  Aug 4, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 849
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Thanks Lizzy..umemaliza mzizi wa fitina....kama mdau alivyosema hapo juu..inabidi hii topic tui-pin!

  Mimi binafsi hili suala limekuwa linanikera sana kulinganisha mapenzi na makabila. Sasa siye tuliopendana na wahindi inakuwa issue kweli kweli kufanya wakubalike kule nyanda za juu...muda mwingi tunapoteza kuwa mameneja uhusiano kuweka mambo sawa..

  Anyway, Mimi msimamo wangu unabaki kuwa mapenzi, mahusiano hayana demokrasia. Ni vizuri tukaheshimiana kama ndugu na ukoo lakini huwezi kunipangia niishi na nani..
   
 20. M

  MORIA JF-Expert Member

  #20
  Aug 4, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 528
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ni kweli utani haukwepeki ktk jamii ya kitz..hili limeanza tangu mababu..ktk utani utasikia ukweli,chumvi na pumba..utani ulitumiwa kupeleka msg au kuchekeshana tu..hakuna kabila lisilo kasoro alizozitaja lizzy hapo juu..lizzy bwana harusi anaambiwa 'usiende mlisha bint yetu mbwa, tena ukumbini'..ni utani tu tembeeni..hata huko kaskazini wenyewe kwa wenyewe wanataniana/pigana vidongo eg,chagga vs pare/gogo...na kuna vijembe btn chaggas(m'chame,k'bosho,huru,old moshi,m'rangu&rombo)..ni utani tu usiokuwa na ukweli wa moja kwa moja.
   
Loading...