Hivi kabila lina libido au ni watu?

Hivi kabila lina libido au ni watu?

Namshakende

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2021
Posts
844
Reaction score
2,184
Leo nimeona nilete hapa hili jambo linaloniumiza kichwa na huenda linawakuta watu wengi kimya kimya. Kuna wakati unatamani kupenda na kupendwa, lakini unajikuta unakutana na ukuta sio kwa sababu ya tabia yako au ulivyo, bali kwa sababu ya "kabila lako".

Nimekuwa nikikataliwa na warembo mara kwa mara pindi ninapowatongoza, na sababu kubwa inayotajwa au kuashiriwa ni kabila langu. Kabila hili limejengewa sifa mbaya ya "wapenda ngono" kwenye jamii na hasa mitandaoni. Hali hii imenikosesha wanawake wazuri.

Sijui ni kwa nini kabila langu limepakazwa maneno haya ambayo kiuhalisia si kweli. Je, ni kwa sababu jina lenyewe linasound kama ngono? Au ni mitandao ya kijamii inachochea haya mambo kiasi kwamba mtu anapoteza thamani yake halisi? Ukweli ni kwamba linachafua taswira ya watu wengi ambao hawana tabia hizo chafu zinazodaiwa.

Naamini hakuna kabila ambalo watu wake wote wana tabia zinazofanana. Tabia ni za mtu binafsi, si za kabila. Mtu anapaswa kuhukumiwa kwa maadili yake, mwenendo wake na namna anavyowatendea wengine, si kwa jina la ukoo au kabila analotoka.
 
Kuna kitu kisaikolojia kinaitwa projection, mtu anajifanya anachukia kitu fulani hadharani ili tu kuficha jinsi anavyokitamani kwa siri kubwa ndani ya moyo wake.

Mbona sijawahi kuona mtu mwenye nazo wa kabila lenu akikataliwa kwa kisingizio cha kabila?
Unazo za kutosha mzee?

Maana kwenye ulimwengu huu wa sasa, financial security ndio inayofuta ubaguzi wowote ule na si kingine.
 
Siku hizi Nina tatizo la macho au sijui kusoma.
Title imenichanganya sana
 
Kuna kitu kisaikolojia kinaitwa projection, mtu anajifanya anachukia kitu fulani hadharani ili tu kuficha jinsi anavyokitamani kwa siri kubwa ndani ya moyo wake.

Mbona sijawahi kuona mtu mwenye nazo wa kabila lenu akikataliwa kwa kisingizio cha kabila?
Unazo za kutosha mzee?

Maana kwenye ulimwengu huu wa sasa, financial security ndio inayofuta ubaguzi wowote ule na si kingine.
🔨🔨🛠️
 
Leo nimeona nilete hapa hili jambo linaloniumiza kichwa na huenda linawakuta watu wengi kimya kimya. Kuna wakati unatamani kupenda na kupendwa, lakini unajikuta unakutana na ukuta sio kwa sababu ya tabia yako au ulivyo, bali kwa sababu ya "kabila lako".

Nimekuwa nikikataliwa na warembo mara kwa mara pindi ninapowatongoza, na sababu kubwa inayotajwa au kuashiriwa ni kabila langu. Kabila hili limejengewa sifa mbaya ya "wapenda ngono" kwenye jamii na hasa mitandaoni. Hali hii imenikosesha wanawake wazuri.

Sijui ni kwa nini kabila langu limepakazwa maneno haya ambayo kiuhalisia si kweli. Je, ni kwa sababu jina lenyewe linasound kama ngono? Au ni mitandao ya kijamii inachochea haya mambo kiasi kwamba mtu anapoteza thamani yake halisi? Ukweli ni kwamba linachafua taswira ya watu wengi ambao hawana tabia hizo chafu zinazodaiwa.

Naamini hakuna kabila ambalo watu wake wote wana tabia zinazofanana. Tabia ni za mtu binafsi, si za kabila. Mtu anapaswa kuhukumiwa kwa maadili yake, mwenendo wake na namna anavyowatendea wengine, si kwa jina la ukoo au kabila analotoka.
Kabila lina watu wenye silka, hulka na tabia zinazofanana
 
Back
Top Bottom