Ukweli Mchungu wa Mapenzi: Kutoka Dopamine Hadi Machungu

Ukweli Mchungu wa Mapenzi: Kutoka Dopamine Hadi Machungu

bless on

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2026
Posts
1,164
Reaction score
2,841
Wanawake Ukiwanyima Tu pesa Kauli Inayofuata Ni "Wanaume Wote Ni Mbwa" Hii kauli Ilitokana Na Mapenzi Watu wanajiua Kisa mapenzi Laiti haya Mapenzi yangekuwa mtihani wa taifa wengi tungekuwa tunarudia darasa kila mwaka Na ndio maana wanakwambiya Mapenzi Hayana Mwenyewe.

Wengine wakati Tumeingia Kwenye mapenzi tulianza kwa kujiamini huku Tukisema Hapa naoa Kabisa Huku Ukijisemea Mwenyewe Alikuwa Wapi Muda Wote Jamani? Halafu miezi mitatu baadaye tunajikuta tunafuta picha zote, Namba na kujaribu Kumove On. NNa Hapa Ndipo Utaelewa Kuhusu mapenzi Kuwa si mchezo wa kitoto ingawa watu Wanachukulia Kawaida Sana.

Uhalisia wa mapenzi ni kwamba Kila mtu anaingia akiwa na matumaini makubwa lakini si wote wanaotoka wakiwa salama kihisia kwani maumivu ni makubwa sana Mwanzoni mwa mapenzi kila kitu huwa kitamu Ujumbe wa “Umeshindaje?” unahisi kama zawadi ya milioni moja Simu ikilia usiku hata kama ni saa tisa unapokea Halafu Kauli Inayokuja ni kwamba Nimekumiss hivyo Tu halafu una enjoy mwenyewe na Hiki ndio kipindi hiki ambacho ubongo wako unakuwa umelemewa na chemical ya dopamine Ndani Ya Mwili Wako Yani Hapo Husikii wala Huambiwi Kuhusu Mpenzi Wako.

Baada ya muda mambo yanaanza Kubadilika Sasa Unaanza kuona tabia halisi ya Mpenzi wako Yule aliyekuwa anakujibu haraka sasa anaandika “sawa.” Yule aliyekuwa anakupigia kila siku sasa anakupigia wiki Hapa ndipo wengi wanachanganyikiwa sasa wakiamini Kuwa tayari Wameshaibiwa Wengine wanaanza kulalamika, wengine wanaanza kuchunguza simu na wengine wanaanza kuomba ushauri kwa marafiki utasikia Tu "Oyah Shemeji Yenu Anazingua" Ukweli ni kwamba mazungumzo yakipungua sio kama mnakaribia kuachana bali ni mapenzi yanaingia hatua ya uhalisia sasa Yani Kujuana.

Kwani Mapenzi ya kweli ni yapi? Achana na yale mapenzi ya Good morning na good night pekee Bali Ukimpenda mtu kweli, hutamfuatilia sana kwa kile anachokifanya hutamdhibiti kama boss Yani Kitu cha Msingi ni Mawasiliano na Kuelewana Tu.
Wengi huumia kwa sababu wanapenda kupita kiasi bila kujipenda kwanza Wanajitoa hadi wanajisahau. Wanabadilisha tabia, ndoto na marafiki kwa ajili ya mtu mmoja Halafu siku ikitokea anaondoka wao hubaki wakiwa wamepotea Mapenzi hayapaswi kukufanya uwe kivuli cha mtu mwingine bali inabidii iwe wewe Tu.

Mapenzi Yanapaswa kukufanya uongeze uwezo w Kufikiria Na Nguvu ya mahusiano, ugomvi ni kama chumvi kwenye chakula Bila chumvi hakuna ladha, ukiweka nyingi sana chakula kinaharibika Wapenzi watagombana, watatofautiana na wakati mwingine watakwazana Sana Tu Lakini tofauti iko kwenye namna wanavyotatua changamoto Zao.

Kama ndoto zako zinakufa kwa sababu ya mpenzi wako hapo kuna shida Mtu anayekupenda kweli lazima atakuinua Tu Wala sio kukupoteza au kukushusha. Atakutia moyo ufanye biashara, ujiendeleze na uwe bora Hatakuogopa ukifanikiwa, wala hatakudharau ukishindwa.

Mapenzi Hayatapata Mwalimu wake hata Yule Unaemkubali kuwa ni mzee wa Kubadilisha mademu au ni demu anaebadilisha san mabwana lakini kuna mtu wake mmoja ambaye anamtesa sana.

Kwa kifupi ni kwamba hakuna fundi wa mapenzi na pia Kila Mtu Ana Yule Mtu wake ambae anamkubali Sana kiasi kwamba Hata kama ameshaoa lakini ikitokea fursa aje Yule anaempenda basi ndoa inavunjika Hiyo Ndio Nguvu ya mapenzi...
 
Back
Top Bottom