Mapenzi na ukabila....

Lizzy,
Nadhani waliokuelewa wamekuelewa na wasiokulewa basi sijui kama watakuelewa.
Nichangie senti sumuni, hili ni tatizo la exposure. Kama umeishi kijijini kidogobasi au Mtimbira bila kuwa na maingiliano na watu wengine, dunia utakayokuwa unaijua ni hiyo. Utajua kuwa mchele ni kwa ajili ya pepeta tu,kwasababu hujaona wali au pilau.

Moja ya mambo mazuri ya boarding school au JKT ilikuwa ni kukutanisha watu wenye tabia tofauti na mitazamo tofuati ili walete uwiano na kujua kile wasichokijua. Kwa bahati mbaya hali ya siku hizi hairuhusu hivyo na kwahiyo kijana aliyesikia hadithi kuwa Tanga kuna paka wanaongea anabaki kuamini hivyo. Yule aliyesikia Sumbawanga kuna wachawi basi anaamini hivyo n.k.

Hao wanaosema ya tabia, ukabila n.k sio kwamba wana chuki, ni exposure tu! Nimeishi sehemu nyingi sana, na makabila mengi na watu wenye tabia mbali mbali. Ninajua tabia ya mtu haihusiani na chochote ila yeye mwenyewe.
Huko nilkopitia shule,jeshini na makazini kumenisaidia sana kuijua dunia hii.

Nina hakika wanaoandika hayo ipo siku wataangalia thread zao na watajutia wanayoyaandika.
 
Makabila mengi yanayosakamwa ni yale ambayo kwa namna moja au nyingine huwa yanakatabia ka kujiona bora sana kuliko mengine na kupelekea inferiority kwa mengine. Ili kushusha bei ni kupaka tu kwenda mbele, na waandiakayo si uongo ni kweli ''ila tu hakuna balance ya ya kujustfy kuwa yasiyoandikwa ni mazuri saana. Ni vyema ukajua kuku umlaye ala nini ili ujue jinsi ya kumuosha utumbo.
 

...lol...Lizzy asante mdada,...almanusura wangelitaja na langu hapa, walishamaliza kanda ya kaskazini, nyanda za juu kusini, kanda ya kati...wakawa wanaelekea huko mwisho wa reli! Ila, kiukweli pamoja na kulichukia hili, bado ukabila una sehemu kubwa kwenye mahusiano, hasa tunapokwenda tambulisha wachumba makwetu.

Halikwepeki hili.

Big uo Lizzy kwa kuliona hili. La kwetu walilidiscuss hadi wakachoka, sasa wamenyamza naona wanendelea Ziwa Magharibi sasa kabla hawajafika huko mwish wa reli

Mnaosema makabila ya wenzenu mpo! Hope message sent and delivery.
 
Big uo Lizzy kwa kuliona hili. La kwetu walilidiscuss hadi wakachoka, sasa wamenyamza naona wanendelea Ziwa Magharibi sasa kabla hawajafika huko mwish wa reli

Mnaosema makabila ya wenzenu mpo! Hope message sent and delivery.
Na sie wamakonde lini discussion?
 
Back
Top Bottom