Mapenzi na ukabila....

Kwa kweli hii stereotyping sometimes inakera......miaka kadhaa iliyopita nilienda kupanga kwenye nyumba moja hapa Dar, tulikubaliana mambo yote kuhusu pango lakini mwishoni akataka kujua kabila langu...kwa vile nilikuwa na shida nikamtajia kabila langu....baadae nikataka kujua kwa nini kaniuliza....na yeye bila kuzunguka akanambia hataki kupangisha wahaya katika nyumba yake (kwa kweli ilinisononesha sana japokua mimi sio mhaya!) na ni kweli kwenye hiyo estate yake hakukuwa na mpangaji mhaya.

Ishu ya kabila tena ikajitokeza wakati fulani nilipokuwa nanunua kijisehemu cha ardhi mahala fulani.....muuzaji akataka kujua kabila langu....kama kawaida, nikamtajia....lakini baadae kwa utaratibu nikamdodosa ni kwa nini alitaka kujua kabila langu. Akanambia hapendi kupakana na mchaga! Duh, ni kachoka kabisa. Nikajaribu kuimagine kama kweli ningekuwa mchagga angekataa hela ama vipi!

Hatukatai trends au patterns za kitabia (au tamaduni) zipo lakini shida ni namna na mahala tunapozitumia. Mara kadhaa pia nimeona hata stereotyping kwa mujibu wa dini pia inakuwa tatizo.

masuala ya ukabila ni stereo types haimaniishi
ni kweli asilimia 100
ni imani tu iliyojengeka......

wapo watu wastaarabu mno na wanatoka makabila yanaonekana yako ovyo

masuala ya ukabila ni stereo types haimaniishi
ni kweli asilimia 100
ni imani tu iliyojengeka......

wapo watu wastaarabu mno na wanatoka makabila yanaonekana yako ovyo

Sijakusoma vizuri ila naomba tu niseme kwamba Kama ingekua ni kweli walengwa wasingejali...na kwasababu sio kweli ndio maana inabidi ipingwe!!

what a wonderful thread! Asante Lizzy is so educative,asomae na afahamu! Umeusemea moyo wangu sina la kuongeza,naichukia sana hii tabia,naamini watu watajifunza kitu hapa.Barikiwa

Munabisha nini ukweli kuwa wanawake wa kichaga hawajui kupenda magogo na mungu hajawatia progamu ya kupenda ushauri wa bure bora uoe simba na ulale nae kuliko kuoa _fill the blanks_

Pole Dada/Kaka!
Bado ka ushamba kakujihisi mmoja yupo juu ya mwingine imetawala wengi. Itafikia muda tutajiona tulikua usingizin na sasa tumeamka. Wengine hujihisi kuzungumza kizungu ndio kuwa mjanja! Achilia mkoa aliotoka/kabila. Bado ni usingizi tu! Wakiamka watajua walikua usingizin...wakat sisi tunapeta tuuuu! Wao wamebakia kwenye usingizi totoro!

Kwa kiasi kikubwa mila na desturi za kila kabila zina athari kubwa ktk tabia kwa wazawa mfano ukeketaji,kurithi wajane pia kubadilishana wake mfano wamasai na wagogo na msisitizo wa mafiga matatu mfano wazalamo n.k.So watu wanapoongea makabila wanakerwa na mambo kama hayo yanayofanywa na baadhi ya makabila kama hayo.

tabia zinatofautiana kati ya mtu na mtu lakini AVERAGE ya tabia ya sehemu fulani ndio inamata

Aliyeanzisha hii thread akipitia posts zake za nyuma, atagundua kuwa hata yeye amewahi kuwa-stereotype wanaume ktk masuala ya mahusiano. Hii ndio kawaida ya binadamu, ubongo wetu uko programmed kuweka watu kwenye makundi. Tunajisikia vizuri tukiwatenga "wao" na "sisi". Hata hivyo, nakubaliana na hoja, ila tusiishie hapa tu kwenye makabila, twende mbele zaidi ktk aspects zingine za maisha. Hili la ku-stereotype makabila lina wa-potray kina dada vibaya na hawalipendi, lakini kila siku zikianzishwa thread za kuponda "tabia za wanaume", wanakuwa wa kwanza kunoa panga!

Hivi kuna mtu yeyote anaeweza kujitosa hapa akasema na kuthibitisha kwamba kwenye UKOO wake wote hamna wezi..wadada wanaojiuza... wadada warahisi kupatikana...watu wakorofi...wavivu...wambea...wasiojua mapenzi..wanaojali/kupenda pesa (as if hao wapondaji wenyewe hawapendi) ...wahuni ...matapeli...wenye viburi...wenye dharau... wenye sura na mumbo unayoona wewe ni mabaya...wabahili...wachoyo...wanaopenda/oa/olewa kwa pesa n.k achilia mbali kwenye KABILA lake?!Kama wapo ningependa kuwajua ili na sie tusioisha kusemwa kila siku tujifunze toka kwao.

Ukweli na kwamba tabia ya mtu haitakiwi kuwa defined na wapi alipotoka (hata familia yake) bali na vile alivyo.Stereotypes hua zipo kwaajili ya wale waliotofauti na wanaokua stereotyped...kuwasaidia wale wa nje kuwalebel wenzao vibaya ili wao wajione/hisi kwamba ni bora hata kama sio kweli.Ndio maana hata wazungu (sio wote) bado wanatuona Waafrika kama wanyama..wanaamini hatuna akili japo wapo waaAfrika wenye akili kuliko wazungu wengi tu.Ila hili wazo linawafanya wao wajione wako juu.Kama ambavyo sisi wenyewe tunafanyiana kwanzia nchi na nchi..mkoa na mkoa...kabila na kabila..ukoo na ukoo na hata familia hii na ile.Kwenye swala zima la mapenzi naamini kabisa kwamba kabila haiplay role yoyote...kwahiyo achaneni na habari za sijui kabila hili hivi na lile lile.Kama unamjua mtu personally unaweza kumjudge yeye kwa vile unavyomjua na sio zaidi ya hapo.Pili....kama wewe hukupata experience nzuri na mtu wa sehemu fulani haina maana itakua hivyo hivyo kwa wengine wote.Ndio maana hata mwanamke /mwanaume unayemuona wewe kwamba hafai bado anakutana na mtu mwingine na anapendwa utadhani yeye ndio kila kitu.Kwahiyo waache wenzio nao wapate experience zao....kama wewe hukufanikiwa mwache mwingine nae ajaribu bahati yake.

Nasema yote haya maana hili swala la kuchambua makabila ya watu humu limezidi na linaboa kwakweli.Sijali kama ni langu au la mtu mwingine....ishu ni kwamba inachosha!!Mbaya zaidi ni kwamba yote mnayosema yanaweza kufanywa na yeyote hata anaetoka nchi nyingine achilia mbali wa kabila tofauti!

Alafu hivi hamchoki maana pamoja na sifa zote za ajabu ajabu mnazoyarushia haya makabila bado wadada wake wanaolewa SANA na wakaka wake wanaoa SANA ndani na nje ya makabila yao.Bado tu hamjagundua kwamba haisaiidii muachane nayo?!Maana kama ingekua inasaidia for the past few years usingesikia watu wa haya makabila wameoa wala kuolewa!

Mwisho...kama umempenda mtu na tabia yake inaendana na wewe upendavyo endelea nae...kama makabila ni muhimu sana tafuta wakwenu ili tabia zenu zifanane badala ya kuanza kuchambua ya wengine visivyo.Mapenzi kila mtu anaweza akayajua na kila mtu anaweza asiyajue...yote inategemea wawili wapendanao wanavyoyachukulia.

Nimejaribu from every angle niongezee na nimetoka kapa!! Great analysis....

Jamani lizzy umetoka lini segerea?au kwasababu sijatembelea jf skunyingi,pole naona umepungua,huyu mod huyu we mwache tu

Duh.....! Nimependa hii article,coz z mo than Truth.Hatuwezi kuwa wamoja kwa style hii! Pia kuna wale wenye kubeza,kucheka rafudhi(matamshi) ya makabila mengine,'SIWAPENDI' Wakati wenzetu wa jirani wanaharibu sana... lkn sisi wabongo tunaita swaga na kwa fikra finyu na za kutawaliwa bila kufahamu tunaiga! ,ni upuuzi mtupu! Let us join to eliminate these stigmatizing and discriminating attitudes of shamefully labeling others as bad conduct tribes,r u perfect WHOM U now and then label others?!

Aliyeanzisha hii thread akipitia posts zake za nyuma, atagundua kuwa hata yeye amewahi kuwa-stereotype wanaume ktk masuala ya mahusiano. Hii ndio kawaida ya binadamu, ubongo wetu uko programmed kuweka watu kwenye makundi. Tunajisikia vizuri tukiwatenga "wao" na "sisi". Hata hivyo, nakubaliana na hoja, ila tusiishie hapa tu kwenye makabila, twende mbele zaidi ktk aspects zingine za maisha. Hili la ku-stereotype makabila lina wa-potray kina dada vibaya na hawalipendi, lakini kila siku zikianzishwa thread za kuponda "tabia za wanaume", wanakuwa wa kwanza kunoa panga!

Hee! Hata kama jamani looh! Mmezidi kutusema wanawake yaani almost threads zote za makabila zinahusu wanawake khaa....! Karibia kila baya la kabila anaelekezewa mwanamke, hivi ndo kusema nyie wanaume ni wasafi sanaa? Tena wengine wanatumia kigezo cha kabila kuhalalisha/kutetea uzinzi wao! Naona imeshakuwa kama bajeti za bungeni sasa zinavojadiliwa. Kinachokera zaidi ni hii tabia ya kuandama makabila fulani, how comes.......just give us a break......hey!!! Mnaboa sana basi tu.

Mwembe wenye matunda ndo hurushiwa mawe!

Hizo mada za makabila haziwezi isha humu!

Tena mda sio mrefu utaona thread ya kabila humu

Na iwekwe ratiba basi ili tujue mtiririko! Jamani watu watakosa imani hata kwa wapenzi wao kwakweli sababu tu ya yanayosemwa kwa makabila husika.

Duh ni mbaya ila halikwepeki kabisa, nahisi lingeanzia somo kwa wazazi wetu kwanza , maana wao ndio wanaotujaza hii kitu mu kichwa zetu

Dada,

Pia inawezekana kuanza sisi wenyewe ili wazazi wajifunze kwetu..

Jamaa yangu mmoja alio kabila lake lakini ndoa ikaishia kuwa karaha kwake na familia yote. Mwisho wa siku jamaa alianza kutembea na makahaba na akafariki kwa VVU!!

Mimi nliwatega wazazi wangu kutaka kujua kama wanao upendeleo wowote kwa kabila..Na kweli walikuwa na wishes zao lakini baada ya kujadili kwa marefu na mapana waliishiwa points na kuniacha huru...Sikuhitaji kuoa kabila bali rafiki wa kuishi naye maisha yangu yote (if possible)! Kwa sasa wazazi wanaelewa nilichomaanisha!

Kuna college mate wangu naye alikataliwa na wazazi wa mume wake hadi wakasusia harusi yao. Ila baada ya kumwelewa sasa hivi wanampenda na kumpa thamani kuliko walivyowahi kufikiria!

My Ex-GF aliniacha kwa sababu sikuwa kabila lake na akaolewa na mtu wa kabila lake...Ndoa ilidumu kwa kipindi kisichozidi miaka 2!!

Naweza kuendelea tena na tena...ila nachukia sana kuongelea mambo ya msingi kwa misingi ya kikabila. Sisi wenyewe tuchukue hatua bila kusita!

Back
Top Bottom