#COVID19 Maoni ya wananchi kuhusu Chanjo ya Corona

Chanjo ya Corona: Utachanjwa au hutochanjwa?

  • Nitachanjwa

    Votes: 18 34.6%
  • Sitochanjwa

    Votes: 24 46.2%
  • Sina hakika

    Votes: 10 19.2%

  • Total voters
    52
Hata wangetaka wote ni kwamba Chanjo haitoshi..., Hii ya Hiari imepunguza mengi ingawa hali ikibadilika huenda watu wakakumbuka bora ningetumia wakati wa hiari na sio sasa wakati wa kununua na kubembeleza ili upate
 
Sishangai. Kampeni ya mwaka jana ilikuwa very effective. Na watu tuna imani zaidi na tiba mbadala kuliko za kizungu. Aidha, watu kama Gwajima na mashehe wanaaminiwa kuliko serikali. Ndio maana point ya Mwembe ni muhimu. Watu waambiwe ukweli na sio kujaribu ku rewrite history.

Amandla...
 
Subiri hadi pale itapogundulika Covid inapunguza nguvu za kiume na chanjo inarejesha majeshi vitani...

😂😂
Subiri hadi pale itapogundulika Covid inapunguza nguvu za kiume na chanjo inarejesha majeshi vitani...

😂😂
Hata wanawake nao watakimbilia kuchanjwa kama hiyo chanjo inaongeza nguvu za kiume?
 
Mkuu watu kukataa chanjo sio Tanzania tu hata US na Europe Kuna wengi tu wamekataa chanjo, unataka kusema na hao Magufuli aliwaaminisha chanjo haifai?
Nazungumzia Watanzania
Watanzania majority ambao hawakwenda shule hata hizo taarifa za marekani wanazipata saa ngapi?, wengi wanasikiliza mamlaka za nchini, na Magufuli alishawaprogramu tayari
 
Sishangai. Kampeni ya mwaka jana ilikuwa very effective. Na watu tuna imani zaidi na tiba mbadala kuliko za kizungu. Aidha, watu kama Gwajima na mashehe wanaaminiwa kuliko serikali. Ndio maana point ya Mwembe ni muhimu. Watu waambiwe ukweli na sio kujaribu ku rewrite history.

Amandla...
Fundi we ushachanjwa?
 
Nazungumzia Watanzania
Watanzania majority ambao hawakwenda shule hata hizo taarifa za marekani wanazipata saa ngapi?, wengi wanasikiliza mamlaka za nchini, na Magufuli alishawaprogramu tayari
Mkuu kuna sehemu unakosea, Ni mambo mangapi Magufuli kayasema na watu waliyapinga na kuyakataa?
Hivyo suala la kukataa chanjo wala sio sababu ya Magufuli kusema hazifai na ndio maana unaona karibu kila nchi kuna watu wengi tu wanazipinga na kuzikataa hizo chanjo.
Hata Magufuli angesema zinafaa, bado kuna watu wengi tu wangezikataa na kuzipinga
 
Yale ya level za wasomi wasomi waliyakataa na raia wa kawaida wala hawakuwa na interest nayo
Ila yale ya watu wote, Magufuli alikuwa akitumia brainwashing tactics za nguvu, na wengi alikuwa akiwapata
 
Chanjo nisizojua 10 years from now itakuwaje nichanje ya nini?, what if ikaenda kuvuruga sehemu sehemu za mfumo wangu na kusababisha hereditary deformities?.
Chanjo naziamini ila hii ya covid haina utafiti wa kutosha juu ya usalama wake
Halafu huku TZ COVID siyo serious kivile, kwa mujibu wa takwimu rasmi hawajaambukizwa watu wanaofika hata 3000
Sasa huoni hii inakinzana na hoja yako hapo juu?
 
Hata wanawake nao watakimbilia kuchanjwa kama hiyo chanjo inaongeza nguvu za kiume?

La hasha...kuhusianisha nguvu za kiume na hiyo chanjo nimeliandika kama utani na hiyo imetokana na hulka ya wanaume wengi wa kiTanzania...

Jambo la chanjo ya Covid kwa kiasi kikubwa halijapokelewa na mwamko mkubwa kwa wanaume...

Na hii ni hulka ya wanaume wa kiTanzania pengine kiAfrika, huwa hawana mwako kwa mambo ya kitaifa, yanayohitaji ushiriki wao...

Ukitazama idadi ya wapiga kura nyakati za chaguzi kuu, wanaume huwa wachache kulinganisha na wanawake...

Kuna wakati kulipotokezea taasisi ya kuzuia na kupambana na mabusha na matende inatoa chanjo hizo, kulitokea upinzani kidogo toka kwa wanaume kiasi kwamba ukazushwa 'uongo' kuwa chanjo ile inaua nguvu za kiume n.k
 
Back
Top Bottom