#COVID19 Maoni ya wananchi kuhusu Chanjo ya Corona

Chanjo ya Corona: Utachanjwa au hutochanjwa?

  • Nitachanjwa

    Votes: 18 34.6%
  • Sitochanjwa

    Votes: 24 46.2%
  • Sina hakika

    Votes: 10 19.2%

  • Total voters
    52

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,216
113,519


Kupitia BBC, haya ni maoni ya baadhi ya Watanzania kuhusu chanjo ya Corona iliyozinduliwa jana na Rais Samia.

Kwenye video hii, walioipinga [waliokataa kuchanjwa] ni wengi kuliko walioikubali.

Watu hawa sijui ndo kama wanaakisi maoni ya Watanzania kwa ujumla; yaani Watanzania wengi kuikataa hiyo chanjo.

Hebu nasi tupige kura ya maoni humu JF.
 
We kamanda ushachanjwa?
Chanjo nisizojua 10 years from now itakuwaje nichanje ya nini?, what if ikaenda kuvuruga sehemu sehemu za mfumo wangu na kusababisha hereditary deformities?

Chanjo naziamini ila hii ya covid haina utafiti wa kutosha juu ya usalama wake

Halafu huku TZ COVID siyo serious kivile, kwa mujibu wa takwimu rasmi hawajaambukizwa watu wanaofika hata 3000
 
Subiri hadi pale itapogundulika Covid inapunguza nguvu za kiume na chanjo inarejesha majeshi vitani...

😂😂
 
Chanjo nisizojua 10 years from now itakuwaje nichanje ya nini?, what if ikaenda kuvuruga sehemu sehemu za mfumo wangu na kusababisha hereditary deformities?.
Chanjo naziamini ila hii ya covid haina utafiti wa kutosha juu ya usalama wake
Halafu huku TZ COVID siyo serious kivile, kwa mujibu wa takwimu rasmi hawajaambukizwa watu wanaofika hata 3000
We ndo kamanda wa ukweli bana!!
 
Ukiwauliza wana sababu gani kuipinga, hawana

Ukiwauliza je wamelazimishwa?
 
Back
Top Bottom