Maoni na Ushauri kwa Joshua Nassari

Maoni na Ushauri kwa Joshua Nassari

Benki ni ya Makaburu,serikali iliiuza kitambo,mnashangilia nini?
Labda ingekuwa benki ya posta,lakini NBC limebakia jina tu.
 
Niongezee lingine tafadhali. Ila kama Yeye alivyotutesa katika iliyokuwa Awamu ya Mtu alliyekuwa akimpa Kiburi na Jeuri sasa Awamu hii isiyotaka Ujinga na Upumbavu inamnyoosha na Mimi naiomba izidi tu Kumnyoosha hadi ahame na nchi kabisa aende Kenya au akaishi kabisa kwa Dada yake huko nchini Canada. Hasira zangu zote kwa Yanga SC nimezihamishia Kwake.
Utani sio vita,bila kuwepo Yanga kutaiua Simba.
Punguza hasira rudi kwenye utani.
 
Nimesikiliza maelezo ya ndugu Nassari hapo jana, ambaye ni mbunge aliyetenguliwa ubunge wake kwa kile kilichosemekana kuwa kutokuhudhuria mikutano mitatu ya bunge. Ameongea mengi, lakini nikiwa mtu niliye mfahamu tukiwa chuo kikuu cha Dar es Salaam na tukihudhuria baadhi ya madarasa pamoja hasa katika somo la filosofia kozi ya "critical thinking and argumentation" chini ya wahadhiri mahili kama Dk. Mihanjo, Dk. Lwaitama, n.k juu ya namna ya kupanga "Valid argument."

Amezungumza mengi ila mie nitajikita kujadili hoja yake akilinganisha kuwa, " kwenda bungeni ili kupata posho ya laki tatu au kubaki akihudumia mkewe kipi bora?''

Binafsi najua bunge lina shughuli kuu tatu: (a). Kuisimamia serikali(oversight function), (b). Uwakilishi (Representative function), (c). Kutunga sheria(Legislative function). Hakuna sehemu nimeona kuwa kuna jukumu la mbunge la kupokea posho ya laki tatu bali posho ni yatokanayo. Hivyo kila mbuge anapohudhuria mkutano wa bunge na vikao vyake hufanya kazi ya kuisimamia Serikali, kutunga sheria na kuwakilisha wananchi au makundi ya watu waliomtuma kuwawakilisha kwa mujibu wa demokrasia ya uwakilishi.

Hili la kulinganisha kati ya kuhudumia mke au kuhudhuria bungeni kupokea posho ya laki tatu linatoka wapi? Hapa pana maswali ya kujiuliza juu ya wabunge wetu na hususani ndugu Nassari:-

1. Je, lengo la kuhudhuria bungeni ni kupata posho ya laki tatu?
2. Je, Ushahidi wa kuwa ulihudhuria Mkutano wa bunge na vikao vyake ni kuchukua posho?
3. Je, Nassari kwa muda aliohudhuria bungeni lengo ilikuwa posho na ndiyo maana alipima kati ya posho na mkewe akaona bora abaki akihudumia mkewe?

Katika hotuba yake fupi yapo mengi ya kujadili ila tuanze na hilo baadaye tutakuja kwenye ndafu aliyo pewa Ndugai: hiyo ita fall kwenye "fallacy" ya kuomba huruma katika hoja, "argumentum ad pitium"
Maamkizi.

Ahsante kwa nadharia ya kichokozi (Provacation thesis).

Nitarudi.
karibu tujadili
 
Nasimamia katika ile dhana ya innocence until proven guilty.Katika utawala bora ilitakiwa ajieleze kwanza kwa nini Bunge lisichukue hatua kabla ya kumfukuza...Je kama ana ushahdi kuwa hajakosa mikutano mitatu au kama ana sababu za msingi za kukosa kuhudhuria vikao huoni kama bunge litakuwa limekurupuka kumfukuza?

Napenda tusimamie kanuni na sheria ila haki ionekane kutendeka.

Ameshachelewa.
 
2005-2015 Ikulu ilikuwa Kama Mgahawa wa Chai wa wana Jangwani

Sasa hivi Ni zamu yetu wana Msimbazi

Watuvumilie Basi

Tena watuvumilie kweli kweli na Sisi na Dkt. Magufuli wetu ambaye pia ni Mwana Simba SC Mwenzetu bila kumsahau na Premier Kassim Majaliwa tutawatesa mno katika hii miaka 10 mpaka Yanga SC wanyooke na watuombe Msamaha / Radhi Kudadadeki!
 
Na hakuna mtu atakaeikopesha kampuni ambayo ni bankrupt.
Ilikopeshwa ikiwa vizuri lakini kutokana na regime changes company imeshindwa kufanya kazi liability side imekuwa kubwa kuliko asset side hiyo ni literally Bankrupt

Na ktk zile 5 c's za credit(Character + Collateral+ Capital + Capacity + Conditions) worthiness wangekuwa wanazifanya sasa hivi wasingempa mkopo kwa maana hiyo C ya mwisho hapo (conditions) haipo favourable kwake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilimsikiliza Mh Nassari vizuri Sana nilianza kuishiwa nguvu kule kumlinganisha mke wake na majukumu ya Bunge sio sahihi akumbuke gharama ya uongozi unajiuliza nitalifanyia Nini Taifa langu sio Taifa langu nitanifanyia Nini

Pili sikubaliani na Mh.Nassari kabisa kuwa aliona ni bora abaki na mke wake kuliko kukimbilia posho ya laki,kumbuka amekosa mikutano na vikao vya Bunge miezi tatu yaani siku tisini, lakini pia najuliza yeye ni mkunga au Daktari bingwa wa magonjwa ya uzazi? Ukweli ni kwamba Mh.Nassari angeweza kujipanga kuaga na kuwa karibu na mke wake kuliko kumtumia Kama Kinga kujificha ili kuondoa wajibikaji wake kazi za uwakilishi.

Hatuwachagui wabunge wetu kwa sababu ya posho Mh.Nassari anatuingizia ajenda isiohitajika kabisa ktk utetezi wake anajaribu kumlinganisha mke wake na posho ya laki tatu! Hili nalo linamshushia heshima Mh.Nassari anaibua hoja mpya kama posho ingekuwa million tatu au zaidi angemuacha mke wake katika hali ya uzazi ili ahudhurie vikao vya bunge lakini ukweli miezi yote mitatu alikuwa USA kwa matibabu?

Lakini pia Mh. Nassari anajieleza yeye na mke wake walikuwa na matatizo ya kiafya lakini tujiulize swala la uzazi na kawaida mimba huchukua miezi tisa sio swala la ghafla au dharura kweli Mh Nassari hakujua kuwa kipindi hicho ili kufanya maandalizi hata ya kumuaga baba Mh.Spika au hata kiongozi wa KUB au Mkiti au Katibu Mkuu wa Chama chake? Kwangu naliona sio sio swala la dharura ! Naendelea kujiuliza kwanini hasa Mh.Nassari hakujiandaa angalau kabla ya kusafiri kuketi na Mh Spika kwanza Kama baba yake kumuaga?

Mh.Nassari anakiri alikula kiapo Cha kuwa na mke wake katika raha na taabu kanisani akumbuke pia alikula kiapo kuilinda na kuitetea Katiba ya Tanzania ktk majumu yake Kama mbunge!!

Baya zaidi kumlinganisha kazi zake uwakilisi na laki tatu za posho ukweli ni kwamba wabunge wetu hawaoni hata aibu lakini tatu ni fedha nyingi Sana ktika nchi maskini ambayo watu maskini huishi chini ya Dolla Mona kwa siku kilichomfanya aione hiyo laki tatu so kitu ni nafasi ya ubunge

Akumbuke wapo walimu waganga wakinzi wa Taifa hili ambao wapo katika kiwango sawa Cha Elimu na Mh Nassari hawapati hata hiyo lakini tatu ktk posho zao kea siku.

Tukumbuke wote sisi ni watoto wa wakulima na wafanyakazi tukianza kusahau kuwa sisi sio sehenu ya makundi hayo tutakuwa hatuwatendei haki waliotuchagua ktk nafasi hizo za kuchaguliwa.

Ndugu Nassari ni bora atumie hekima ya kumuomba radhi Mh.Spika kuliko kumlaumu katika majukwaa yasio rasmi ili yaishe asamehewe kuliko kumdhalilisha Spika Mimi nakuomba na kukusihi muombe Mh.Spika samahani nasi tunamuomba akusamehe kuliko kubishana naye kea njinsi unavyojieleza unatupekea tujiulize kwa bado kufikiria kungaliko katika kizazi chetu?!!
 
Nimesikiliza maelezo ya ndugu Nassari hapo jana, ambaye ni mbunge aliyetenguliwa ubunge wake kwa kile kilichosemekana kuwa kutokuhudhuria mikutano mitatu ya bunge. Ameongea mengi, lakini nikiwa mtu niliye mfahamu tukiwa chuo kikuu cha Dar es Salaam na tukihudhuria baadhi ya madarasa pamoja hasa katika somo la filosofia kozi ya "critical thinking and argumentation" chini ya wahadhiri mahili kama Dk. Mihanjo, Dk. Lwaitama, n.k juu ya namna ya kupanga "Valid argument."

Amezungumza mengi ila mie nitajikita kujadili hoja yake akilinganisha kuwa, " kwenda bungeni ili kupata posho ya laki tatu au kubaki akihudumia mkewe kipi bora?''

Binafsi najua bunge lina shughuli kuu tatu: (a). Kuisimamia serikali(oversight function), (b). Uwakilishi (Representative function), (c). Kutunga sheria(Legislative function). Hakuna sehemu nimeona kuwa kuna jukumu la mbunge la kupokea posho ya laki tatu bali posho ni yatokanayo. Hivyo kila mbuge anapohudhuria mkutano wa bunge na vikao vyake hufanya kazi ya kuisimamia Serikali, kutunga sheria na kuwakilisha wananchi au makundi ya watu waliomtuma kuwawakilisha kwa mujibu wa demokrasia ya uwakilishi.

Hili la kulinganisha kati ya kuhudumia mke au kuhudhuria bungeni kupokea posho ya laki tatu linatoka wapi? Hapa pana maswali ya kujiuliza juu ya wabunge wetu na hususani ndugu Nassari:-

1. Je, lengo la kuhudhuria bungeni ni kupata posho ya laki tatu?
2. Je, Ushahidi wa kuwa ulihudhuria Mkutano wa bunge na vikao vyake ni kuchukua posho?
3. Je, Nassari kwa muda aliohudhuria bungeni lengo ilikuwa posho na ndiyo maana alipima kati ya posho na mkewe akaona bora abaki akihudumia mkewe?

Katika hotuba yake fupi yapo mengi ya kujadili ila tuanze na hilo baadaye tutakuja kwenye ndafu aliyo pewa Ndugai: hiyo ita fall kwenye "fallacy" ya kuomba huruma katika hoja, "argumentum ad pitium"
Dogo kachoka siasa ndiyo linaloonekana kwa uwazi zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilimsikiliza Mh Nassari vizuri Sana nilianza kuishiwa nguvu kwa kumlinganisha mke wake na majukumu ya Bunge.

Pili sikubaliani na kabisa kuwa aliona ni Bora abaki na mke wake kuliko kukimbilia posho ya laki tatu.

Kwani tunawachagua wabunge kea sababu ya posho je posho ingekuwa million tatu angemuacha mke wake katika uzazi.

Lakini pia Mh. Nassari anaeleza walikuwa na matatizo ya kiafya na mimba huchukua miezi tisa Kama alilifahamu Hilo maana sio la dharura kwa Nini hakujiandaa angalau kabla ya kusafiri kuketi na Mh Spika kwanza Kama baba yake kumuaga?

Mh.Nassari anakiri alikula kiapo Cha kuwa na mke wake katika raha na taabu kanisani akumbuke pia alikula kiapo kuilinda na kuitetea Katiba ya Tanzania ktk majumu yake Kama mbunge!!
Baya zaidi kumlinganisha kazi zake uwakilisi na laki tatu za posho ukweli ni kwamba wabunge wetu hawaoni hata aibu lakini tatu ni fedha nyingi Sana ktika nchi maskini ambayo watu maskini huishi chini ya Dolla Mona kwa siku kilichomfanya aione hiyo laki tatu so kitu ni nafasi ya ubunge

Akumbuke wapo walimu waganga wakinzi wa Taifa hili ambao wapo katika kiwango sawa Cha Elimu na Mh Nassari hawapati hata hiyo lakini tatu ktk posho zao kea siku.

Tukumbuke wote sisi ni watoto wa wakulima na wafanyakazi tukianza kusahau kuwa sisi sio sehenu ya makundi hayo tutakuwa hatuwatendei haki waliotuchagua ktk nafasi hizo za kuchaguliwa.

Ndugu Nassari ni hekima kuomba radhi uaishe usamehewe kuliko kupigana upepo usio weza kuuzuia nakuomba na kukusihi muombe Mh.Spika samahani nasi tunamuomba akusamehe kuliko kubishana naye
Ukichambua hotuba yake ina ukakasi mwingi.
 
Natamani mchambuzi mmoja atuchambulie kuhusu ishu ya Nassari hasa juu ya maswali yafuatayo..
  • Ni kweli Nassari hakuhudhuria mikutano mitatu ya bunge kama taarifa zinavyosema?
  • Kwa sie tusiofahamu, wanaposema mikutano mitatu wanamaanisha nini?
  • Ni kweli kwamba Nassari kwa kipindi chote hicho cha mikutano mitatu ambayo inadaiwa hakuhudhuria alikuwa akimuuguza mkewe kwa matatizo aliyoyasema?
  • Kanuni za bunge zinasemaje kuhusu kuomba ruhusa ya kutohudhuria vikao/mikutano ya bunge?
  • Je, Nassari alifuata taratibu hizi?
  • Kama hakufuata, ni kwanini?
  • Kama alifuata, je alipewa ruhusa?
  • Kama alipewa ruhusa, kwanini afutwe ubunge?
  • Kama hakupewa, ni kwa sababu zipi?
  • Ni mazingira yapi kikanuni yanaweza kumfanya spika (ofisi ya bunge) kumyima mbunge ruhusa ya kutohudhuria kikao/mkutano wa bunge?
  • Je, kanuni za bunge zinasemaje kuhusu wabunge wasiohudhuria vikao/mikutano ya bunge (watoro)?
 
Nassari tumeshamsahau sasa tuko na maalimu Seif wa ACT wazalendo!
 
Back
Top Bottom