Maoni na Ushauri kwa Joshua Nassari

Maoni na Ushauri kwa Joshua Nassari

Na bahati nzuri sana ni kwamba Nassari anatokea katika Familia ya Kitajiri sana ( inayojiweza Kiuchumi ) hasa kupitia Baba yake Mzazi ambaye alikuwa si tu ni mwana CCM wa Kutukuka, bali pia alikuwa ni mwana ' Eagle Wing House ' mkubwa tu hivyo sioni kwanini Yeye ang'ang'anie na asumbuke na Siasa tena hizi zetu za ' Maji Taka ' tupu wakati bado anaweza Kuyaishi maisha bora na mazuri tu.
Au kama vipi ajiunge CCM apate mkate wa watoto wake manake sidhani kama ataweza kuishi huko uraiani. Kuitwa Mheshimiwa hadi kuwa jobless ni kitu kigumu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
JE! MBUNGE ANAHUDHURIA BUNGENI KWA AJILI YA POSHO YA LAKI TATU AU KUTEKELEZA MAJUKUMU MAKUU MATATU YA BUNGE?

Nimesikiliza kwa makini hotuba fupi ya ndugu Nassari iliyojaa mambo mengi ya kujadili na yenye kuacha maswali.

Binafsi namfahamu ndg. Nassari tangu tukiwa wote wanafunzi chuo kikuu cha Dar es Salaam. Hivyo nampa pole kwa yanayoendelea. Hii historia ya kujirudia kwake. Mwaka 2008 akiwa naibu spika wa bunge la wanafunzi alivuliwa unaibu spika kwa mizaha tuu ya kutokufuata kanuni za bunge na DARUSO by-laws spika akiwa ndg. Mgeta.

Ninafahamu Nassari akiwa na rafiki yake ambaye ni rafiki yangu pia Jaccob Mlikuza hawakuwa wazembe darasani, hivyo Nassari alihudhuria vyema somo la filosofia ya ujenzi wa hoja, "critical thinking and argumentation" chini ya wahadhiri mahili kama Dk. Mihanjo, Dk. Lwaitama, n.k

Nilivyo msikia akilinganisha kati ya " KUHUDHURIA BUNGENI KWA AJILI YA POSHO YA LAKI TATU AU KUBAKI AKIHUDUMIA MKEWE ANGECHAGUA NINI!" binafsi nilishtuka.

Ninajua bunge lina shughuli kuu tatu. 1. kuisimamia serikali, (oversight function) 2. Kutunga sheria (Legislative function) na 3. Uwakilishi (representative function). Katika majukumu hayo, hakuna sehemu nimeona kuwa mbunge anahudhuria bungeni kwa ajili ya kupokea posho ya laki tatu bali kutimiza majukumuhayo ya bunge. Hapa pana maswali ya kujiuliza:-
1. Je! Nassari amekuwa akihudhuria bungeni kwa ajili ya posho?
2. Je! Kauli yake hiyo inawakilisha tabia na lengo la wabunge wetu kwa ujumla wakiwa bungeni?

Hotuba ya nasari ina mengi. Badaye tutajadili ile ya kupewa Ndafu Ndugai kuitumia kama sehemu ya kuomba huruma. " argumentum ad pitium"
 
amenunulika ndiyo aende mahakamani? inaingia akilini kweli? mahakama ikimrudisha, then waliomnunua watasemaje?
Hapa mjini, Mkuu!
Usiamini Mwanasiasa, hata kama ni mzazi wako akikuambia USIKU MWEMA, usimwamini sana.
Mahakama itatumika tu kama Cover Up ya mission, wenye akili wanaelewa nini bwana mdogo ametutenda wapenda Demokrasia.
Za Nasari, changanya na zako...!!!
 
Iko hivi labda wewe umeona meengi aliyoongea Nassari umeona hilo ulijibu.Inamaana maelezo yake kwako yamekubalika 90%.

Hoja iko hivi,kama alilipwa hiyo posho maana yake alihudhuria ndo maana alilipwa.ko hakuna haja ya kusema tena hakuhudhuria.Au mi ndo sijanwelewa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Yawezekana ndiyo namna yako ya kuelewa. Ukisoma katika hitimisho, nimesema yapo mengi ila tuanzae na hilo. Pili, je kuhudhuria bungeni lengo ni posho?
 
Mahakama Kuu imezuia mali za mfanyabiashara maarufu nchini Yusuph Manji kutokana na madeni anayodaiwa na Benki ya NBC. Manji anadaiwa zaidi ya shilingi bilioni 25 ambazo ameshindwa kuzirejesha kwa wakati kwa mujibu wa mkataba

View attachment 1048101

Halafu bado alikuwa anajifanya Kuitaka Yanga SC wakati kumbe ni ' Tapeli ' Mtupu. Hakuna Mhindi aliyetutesa, aliyetudhalilisha na kutudharau wana Simba SC kama huyu ila sasa tunafurahi kuona ' anavyonyooshwa ' na naomba Mamlaka husika wazidi tu ' Kumyoosha ' kwani amesababisha mabaya mengi ya Kiuchumi hapa nchini Tanzania. Asante sana Mahakama Kuu ya Tanzania na ' mkazieni ' hivyo hivyo na ' Hasira ' zangu Kwake zimezidi zaidi baada ya ' Wafuasi ' wake wana Yanga SC juzi pale kwa ' Mkapa ' zamani ' Shamba la Bibi ' ambapo walishangilia kupita maelezo goli la Kwanza la AS Vita Club huku wakiwa wanatudhihaki kwa kila namna. Hakuna Kumuonea Huruma / Imani huyu Gabachori / Panjuani.
 
Joshua Nassar hatoshi tenakuwawakilisha wananchi wa Arumeru. Haiwezekani akose session zotye tatu za Bunge wakati yeye ni mwakilishi wa wananchi. Kwani mke akilazwa yeye ni daktari hadi session zote tatu mfululizo asiweze kuhudhuria hata moja? Ampishe tu mwingine.
 
Mie najiuliza tu, makosa madogo kama haya,(kama ni kweli) ni uzembe .... sasa unawezaje kufanywa na vijana wanaoitwa wasomi na pengine chama kikishika hatamu wawe viongozi wa juu serikalini, watatufikisha kweli?
Masnva aya!
 
Joshua Nassar hatoshi tenakuwawakilisha wananchi wa Arumeru. Haiwezekani akose session zotye tatu za Bunge wakati yeye ni mwakilishi wa wananchi. Kwani mke akilazwa yeye ni daktari hadi session zote tatu mfululizo asiweze kuhudhuria hata moja? Ampishe tu mwingine.
Mi nadhani asiende mahakamani; agombee tu wananchi watampa tena ridhaa kama hakuwa mbaya kwao.
 
Back
Top Bottom