Maoni na Ushauri kwa Joshua Nassari

Maoni na Ushauri kwa Joshua Nassari

Nasari katika hili kazingua alijisahau sana. Au sio kua alijisahau alikua anajua alitendalo.
 
Yule dogo mjinga sana....kwani yeye ni wa kwanza kuoa na mke kujifungua....sisi waajiriwa, wake zetu wanajifungua tunachukua 3 days za paternity leave kisha tunarudi kibaruani mtoto hata 7 bado?

Sent using Jamii Forums mobile app
Labda mke wake alijifungua "Samsoni mnadhiri wa Bwana" hivyo alikuwa anahakikisha wembe haupiti kichwani mwake kwa miezi 9. Who knows?
 
Kufuata sheria au intimacy eneo la kazi kipi bora? Angeaga Kazini kwake kungetokea haya? Acheni kutetea ujinga, huyu mimi naamini kwamba amenunulika 99.9%
amenunulika ndiyo aende mahakamani? inaingia akilini kweli? mahakama ikimrudisha, then waliomnunua watasemaje?
 
Hata najiuliza hili lichama linaendeshwaje? Hakuna hata social life yaani, hata group la WhatsApp la viongozi basi! Yaani mikutano mitatu inapita mtu hahudhurii and nobody notices. Wote wanakuja kushtuliwa na barua ya spika!
Hivi Chadema hawawezi kufanya vizuri hata kitu kimoja jamani, kimoja tu
Pale Chadema kila mtu ni kambale by mzee Juma Duni Hajji
 
Nimesikiliza maelezo ya ndugu Nassari hapo jana, ambaye ni mbunge aliyetenguliwa ubunge wake kwa kile kilichosemekana kuwa kutokuhudhuria mikutano mitatu ya bunge. Ameongea mengi, lakini nikiwa mtu niliye mfahamu tukiwa chuo kikuu cha Dar es Salaam na tukihudhuria baadhi ya madarasa pamoja hasa katika somo la filosofia kozi ya "critical thinking and argumentation" chini ya wahadhiri mahili kama Dk. Mihanjo, Dk. Lwaitama, n.k juu ya namna ya kupanga "Valid argument."

Amezungumza mengi ila mie nitajikita kujadili hoja yake akilinganisha kuwa, " kwenda bungeni ili kupata posho ya laki tatu au kubaki akihudumia mkewe kipi bora?''

Binafsi najua bunge lina shughuli kuu tatu: (a). Kuisimamia serikali(oversight function), (b). Uwakilishi (Representative function), (c). Kutunga sheria(Legislative function). Hakuna sehemu nimeona kuwa kuna jukumu la mbunge la kupokea posho ya laki tatu bali posho ni yatokanayo. Hivyo kila mbuge anapohudhuria mkutano wa bunge na vikao vyake hufanya kazi ya kuisimamia Serikali, kutunga sheria na kuwakilisha wananchi au makundi ya watu waliomtuma kuwawakilisha kwa mujibu wa demokrasia ya uwakilishi.

Hili la kulinganisha kati ya kuhudumia mke au kuhudhuria bungeni kupokea posho ya laki tatu linatoka wapi? Hapa pana maswali ya kujiuliza juu ya wabunge wetu na hususani ndugu Nassari:-

1. Je, lengo la kuhudhuria bungeni ni kupata posho ya laki tatu?
2. Je, Ushahidi wa kuwa ulihudhuria Mkutano wa bunge na vikao vyake ni kuchukua posho?
3. Je, Nassari kwa muda aliohudhuria bungeni lengo ilikuwa posho na ndiyo maana alipima kati ya posho na mkewe akaona bora abaki akihudumia mkewe?

Katika hotuba yake fupi yapo mengi ya kujadili ila tuanze na hilo baadaye tutakuja kwenye ndafu aliyo pewa Ndugai: hiyo ita fall kwenye "fallacy" ya kuomba huruma katika hoja, "argumentum ad pitium"
 
Mahakama Kuu imezuia mali za mfanyabiashara maarufu nchini Yusuph Manji kutokana na madeni anayodaiwa na Benki ya NBC. Manji anadaiwa zaidi ya shilingi bilioni 25 ambazo ameshindwa kuzirejesha kwa wakati kwa mujibu wa mkataba

manji.jpg

Dar es Salaam. Mahakama Kuu imezuia mali za mfanyabiashara maarufu nchini Yusuph Manji kutokana na madeni anayodaiwa na Benki ya NBC.

Manji anadaiwa zaidi ya Sh25 bilioni na benki hiyo ambazo ameshindwa kuzirejesha kwa wakati kwa mujibu wa mkataba, hivyo mali zake zilizopo Mwanza na Dar es Salaam ambazo ziliwekwa dhamana, kuzuiwa.

Mali hizo zimezuiwa kwa oda mbili tofauti za mahakama hiyo zilizotolewa Februari 19 zinazomzuia Manji kufanya muamala wa aina yoyote kuzihusu ikiwamo kuhamisha umiliki kama zawadi, kuuza au kuweka dhamana.

Oda ya kwanza inayotokana na kesi ya biashara namba 54 ya mwaka 2018 inaizuia kampuni ya Manji Tanperch kufanya chochote kwenye kitalu namba 8, 9 na 127 vilivyopo eneo la viwanda Ilemela kwa jina la Tanperch Limited kwa kushindwa kulipa deni la Sh18.7 bilioni kutoka Benki ya NBC.

NBC ilifingua kesi mwaka 2016 ikizishtaki kampuni za Farm Equip (T) Limited, Tanperch Limited na Quality Group Limited zinazomilikiwa na Kaniz Manji na Yusuf Manji kwa kushindwa kurejesha Sh15.9 bilioni.

Desemba mwaka jana, Jaji Butamo Philip aliwataka washtakiwa wote watano kulipa deni hilo ambalo lilikuwa limefika Sh18.7 bilioni linalojumuisha mkopo wa akaunti (overdraft) na wa kuingiza bidhaa nchini.

Kati ya washtakiwa hao, nyaraka za mahakama zinaonyesha Farm Equip ndiye mkopaji mkuu na wengine ni wadhamini.
“Farm Tanperch inazuiliwa kuuza au kuhamisha umiliki kwa namna yoyote,” inasomeka sehemu ya oda.
 
Aliyekuwa mbunge wa Arumeru Joshua Nassari amevuliwa ubunge kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania kuwa hajahudhuria vikao vya bunge mara 3 mfululizo pasipo kuwa na taarifa yoyote kutoka kwa Spika wa Bunge, mh. Ndugai hakuwa na taarifa za kutokuhudhuria kwenye vikao mh. Nassari. Maamuzi yalitolewa nayaunga mkono Kwa 100%.

Sasa nimejiuliza kitu kimoja kutokana na tukio hilo, Mh. Tundu Lissu alifutiwa mshahara na marupurupu ya kibunge kwa sababu tu Mh. Ndugai hana taarifa na hajui mahali alipo Lissu, sababu hizo zilizotolewa hazina tofauti na zile zilizomuondoa Ubunge Nassari. Swali

1. Kwanini Lissu nae asifutiwe Ubunge kwasababu Spika hana taarifa zake?
2. Ni kipengele kipi cha Katiba kilichotumika kumfutia marupurupu na mshahara Lissu na kikamwachia nafasi yake ya Ubunge?
3. Kama hicho kipengele cha kufutiwa mshahara na marupurupu kwa mbunge ambae hajahudhuria vikao vya bunge bila taarifa kipo Kwanini hakijatumika kwa Nassari?
4. Kama hicho kipengele hakipo ina maana walitumia kipengele kipi cha Katiba kumfutia Mh.Lissu mshahara?

Wale wajuzi wa Sheria naombeni mnijibie maswali yangu.
 
Hakuna kipengele kinachompa ndugai ruhusa ya kufuta.mshahara

ipo sheria ambayo inapunguza kiasi cha mshahara wa mbunge lakini sio kufutiwa kabisa. Atalipwa nusu yake pamoja na malupulupu endapo atabainika na makosa ya kukiuka sheria za bunge pamoja na kutoudhuria hivyo vikao vyote bila taarifa kama sikosei.

Sent using unknown device
 
Pamoja na kwamba wewe ni kiazi, kwa hili uko sahihi sana.

Taratibu unaanza Kunikubali na nina uhakika ipo Siku wote mtakuwa ' TEAM GENTAMYCINE ' hasa ' Kifikra ' na ' Kifalsafa ' na ni suala na muda tu.
 
Huyo hakuna kitu ni danganya toto - wenzake waliondoka kwa kujivua unachama mchana kweupe yeye ametumia hiyo style kurudi nyumbani - na si siku nyingi uwe uchaguzi mdogo au mkuu ujao utasikia amepata jimbo hilo akiwa CCM

Yaani:-
(i). Miezi takriban tisa (9) hauko bungeni,
(ii). Mawasiliano ya ruhusa kutumia sms za simu,
(iii). Arumeru mpk Dom kilomita takribani 500 tu,
(iv). Barua uliyoonesha awali haina saini!

Kama si usanii ni nini? Hata Spika alikuvumilia sana!
 
Aliyekuwa mbunge wa Arumeru Joshua Nassari amevuliwa ubunge kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania kuwa hajahudhuria vikao vya bunge mara 3 mfululizo pasipo kuwa na taarifa yoyote kutoka kwa Spika wa Bunge, mh. Ndugai hakuwa na taarifa za kutokuhudhuria kwenye vikao mh. Nassari. Maamuzi yalitolewa nayaunga mkono Kwa 100%.

Sasa nimejiuliza kitu kimoja kutokana na tukio hilo, Mh. Tundu Lissu alifutiwa mshahara na marupurupu ya kibunge kwa sababu tu Mh. Ndugai hana taarifa na hajui mahali alipo Lissu, sababu hizo zilizotolewa hazina tofauti na zile zilizomuondoa Ubunge Nassari. Swali

1. Kwanini Lissu nae asifutiwe Ubunge kwasababu Spika hana taarifa zake?
2. Ni kipengele kipi cha Katiba kilichotumika kumfutia marupurupu na mshahara Lissu na kikamwachia nafasi yake ya Ubunge?
3. Kama hicho kipengele cha kufutiwa mshahara na marupurupu kwa mbunge ambae hajahudhuria vikao vya bunge bila taarifa kipo Kwanini hakijatumika kwa Nassari?
4. Kama hicho kipengele hakipo ina maana walitumia kipengele kipi cha Katiba kumfutia Mh.Lissu mshahara?

Wale wajuzi wa Sheria naombeni mnijibie maswali yangu.

Lissu kapewa barua rasmi ya kusimamishiwa mshahara?
 
Back
Top Bottom