Manyara: Upatikanaji wa Petroli Mbulu ni changamoto, EWURA yatoa onyo wanaohodhi mafuta

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
1689579557038.png

Kuna ujumbe wa Mdau katupia picha hii na kueleza kuwa hali ilivyo katika Mbulu Mjini Mkoani Manyara Wananchi wakiwa kwenye foleni ya kupata Petrol ni baada ya takribani wiki wakikosa huduma ya Nishati ya Petrol.

Hii inatokana na uwepo wa vituo vitatu pekee vya kutolea huduma hii muhimu na vinavyofanya kazi vyote ila ni vituo viwili pekee ndio vyenye kutoa huduma hii (vituo vyote hivyo ni vya watu binafsi).

Sasa unaweza kuta inapita hata wiki na zaidi mji mzima hakuna hata mafuta.

Pia soma > Wilaya ya Ngara hakuna petroli siku ya nne
Pia soma > Hali ya Mafuta ya Petroli Liwale ni tete kwa zaidi ya wiki sasa

===========

UPDATES...

IMG_8051.jpeg

EWURA imepokea taarifa ya uwepo wa baadhi ya Kampuni za Mafuta KUHODHI mafuta kwa ajili ya maslahi binafsi ya kibiashara ikiwemo kusubiri mabadiliko ya bei.

Aidha, kampuni nyingine zinasemekana kupakia mafuta kutoka kwenye maghala pasipo kuyauza na nyingine kukataa kuza mafuta kwa wamiliki wa vituo wasio kuwa na ubia au mikataba nao. Kutokana na hayo, EWURA imepata taarifa ya kuchelewa kufikishwa kwa mafuta katika baadhi ya maeneo va pembezoni mwa nchi na miii.

EWURA inapenda kuwajulisha wananchi woe kuwa chi ina mafuta ya kutosha katika maghala ya kuhifadhia mafuta na wakati huo huo meli zene sheena ya mafuta kutoka nie ya chi zinaendelea kuingia na kushusha mafuta kama kawaida chini ya uratibu wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA).

Mpaka tarehe 14 Julai 2023 mafuta yote yaliyokuwepo chini ni lita 169,853,692 za mafuta ya petroli, lita 209,641,670 za diezeli a lita 34,588,002 za mafuta ya dege yanayotoshelea mahitaji. Kutokana na taarifa hizo, EWURA inatoa ONYO kwa kampuni za mafuta zinazohodhi mafuta na kuzitaka kuacha mara moja kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria, kanuni zinazosimamia biashara ya mafuta ya petroli nchini a masharti ya leseni zao za biashara.

EWURA inapenda kuwataarifu wananchi kuwa inaendelea kufanya ukaguzi wa kina kwenye maghala na vituo vya mafuta na kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wote watakaothibitika kukiuka sheria, kanuni na masharti ya leseni zao, ikiwemo kuwanyang'anya leseni ya biashara kwa mujibu wa Kanuni Namba 6 ya Kanuni Ndogo za Ukokotoaji wa Bei za Mafuta GN. 57 ya mwaka 2022.
 
Back
Top Bottom