Maneno ya kejeli ya mume wangu

Maneno ya kejeli ya mume wangu

'KHERI KUWA NA PENGO KULIKO KUWA NA JINO BOVU'.. Fanya maamuzi magumu for your own sake!

Finally someone is getting it.. Asante kwa kumpa huu ushauri... Most of us don't know or understanding what is really meaning of marriage.. Marriage ni wito katika wito wowote tunaoitwa na Mungu kama hatofanyi bizuri God is willing help us kama tuko willing .. na akituona tuna pride in that calling God takes that calling and give it to someone else and this is including marriage.. Jamaa anajiona husband kivyake yeye na Ku act kivyake hakika hivyo Calling alishaiuuwa because of his selfish , pride and lack of knowledge .. So its up to her to decide it.. Thanks..
 
Ukisoma ushauri wa watu wengi hapa ndio unaelewa kwanini ndoa za wazazi wetu zilidumu lakini siku hizi kuachana kumekuwa kawaida kupita kiasi..I pity this generation, Lord have mercy!!!!

Ikiwa kwa kila jambo la aina hii suluhisho ni kuachana, kutakuwa hakuna ndoa kabisa..karibu kila ndoa once in a while hupitia vikwazo vya namna namna..vyanzo vya haya yote ni wanandoa kupunguza ukaribu na Mungu na kumruhusu shetani a-dictate happenings kwenye maisha yao, shetani hawezi kufurahia ndoa hata kidogo..atapata wapi wachepukaji ndoa zikitulia?

Lord have mercy..msaada wa Mungu unahitajika mahali hapa. I pray for his strength in you Nacherewa
 
Last edited by a moderator:
Kuna ya kuvumilia lakini so dharau na matusi.

Move on girlie.

Dear si afadhali na haya ..na ya kuleta wanawake home .. their matrimony home.. isitoshe basi home bali kitanda chao wanacho share andthen its not one woman , multiple women.. Jesus nisaidie ... I will never understand this ... Thanks..
 
Ni kweli kabisa kila jambo sio matatizo tu linaanzia kwenye ulimwengu wa kiroho kabla ya kuzaliwa kwetu duniani. Huwa tunashiriki na kujua maisha yetu yatakuwaje duniani. Tatizo dhambi hufunika uwezo wa kutambua na kukumbuka maisha yetu yatakuwaje duniani. Hapo tulipaswa kuwa wa kiroho kwa kudumu katika maombi na yote yanayotusumbua yasingetokea maana tungeyajua kabla. Ndio maana nikasema sio kila kitu kinaombewa, kuna vingine unaviepuka tu, na ndio Maana unawezaomba na ukajiona kama hujibiwi bila kujua lile jambo lilitakiwa kuchukuwa hatua fulani na sio kukaa na kuliombea. Sana sana kama unaweza uingie huko kirohoni na kuangalia nini cha kufanya.

Hiyo mwanzao uliyoiquote... inaonyesha uadui wetu na shetani ulipoanzia na adhabu tuliyopata kwa kutotii kwa Hawa. Hapa tunazungumzia Kuondoka katika maisha ambayo si ya raha kwetu, haina maana kwa kuwa tulitenda dhambi basi tutaishi kwa kuumia duniani na kuwa watu wa kulia na kuomboleza bila sababu ... hilo Mungu alitupa neeema kwa damu wa mtoto wake. Ni somo refu sana unaweza usinielewe. Ila point yangu inabaki kwa Nacherewa kuondoka na kutafuta amani na furaha Maana Mungu wetu alituhakikishia kuishi kwa raha tukimtegemea yeye, jicho la kushoto likukosesha ling'oe. Najua bado ni ngumu kunielewa

Dear Mimi nimekuelewa kabisaaa .. Binafsi nilishawahi kumuambia muhusika wangu aliyetaka kunioa in the past neno hilo hilo la Biblia Jicho linalokukosesha Raha ling'oe kwa maana masononeko Pia ni dhambi... Na kwa nguvu za Mungu nili moved on and now I experience the meaning of the True Love.. ..Amen.. Thanks..
 
Last edited by a moderator:
Wajameni hebu tuambiane ukweli kidogo Nacherewa unataka ushauri gani zaidi ya ule utokao ndani ya moyo wako? Nini kinachokufanya uendelee kumvumilia huyo mnyanyasaji? kwa taarifa yako kilichobaki hapo ni kuletewa magonjwa na ukute tayari unayo! Sina haja ya kukuumiza ila nakwambia acha uoga; inuka utafute furaha yako hapo sio kwako!

Waoga hawataingia hata mbinguni, na hapa duniani hawatakula mema ya nchi Mungu aliyowaandalia! Jipe ujasiri toka kwa huyo mume na furaha yako inakungoja. Mungu hakutuumba tunyanyasike lool. Hivi ukiona watu wameachana na waume zao unawaona hawana uvumilivu eeeee! au unaona ni wadhambiiiiiiiii ya kutengwa duniani eeeee ... kuna perfect wako mahali anakusubiri toka hapooooooooooooooo fasterrrrrr

God did not give us a spirit of Fear But of Power and Love and Self Control . 2 Timothy 1:6-7.. Thanks..
 
Last edited by a moderator:
Dada pole. Wewe ni wa imani gani?
kama ni muislamu basi uislamu unaruhusu mwanamke kujitoa(khul-u) katika ndoa. Na ndio moja ya majukumu ya kadhi. Wanaume wamepewa mamlaka ya talaka, na wanawake wamepewa KHUL-U. nenda kwa kiongozi wa dini katika eneo lako na mueleze shida inayokukabili. Mumeo ataitwa na taratibu za khul-u utaelekezwa na hatimae utakuwa huru kuolewa na mume mwingine. Ndoa ikifikia hatua hiyo ni HATARI. Uislamu haukumuweka mwanamke anyanyasike ndani ya ndoa kisa eti kaolewa na mume tu ndio mwenye mamlaka na talaka, BIG NO!
Nimezungumza kwa upande mmoja wa uislamu, ikiwa wewe ni wa dini nyingine basi naamini na wataalamu wa imani hiyo watakuja hapa na kukushauri.SIPENDI NIONGELEE IMANI ISIYO NIHUSU nawaachia wahusika, na huo ndio uungwana
 
Very wise advice.. Be blessed.. Thanks..
 
Rejea kiapo chako vha ndoa tafadhali, kwamba utampenda mume wako kwa shida na raha sasa hapo ndio kuna shida inabidi uongeze upendo zaidi.

Hiki ndio kipindi cha kumpenda mumeo sana ili abadilike mwenyewe.

Wewe una hormonal inbalance na mumeo ana low sperm counts, hii ni hatari sana.

Pigana kupata mtoto tu mambo mengine achana nayo utakufa mapema. Kwa aje yako unaelekea early monopouse kwa hiyo angalia usije kukosa mtoto.
 
hapo kwenye RED mkuu SHIDA si sawa na MATESO. Kiapo kilisema SHIDA NA RAHA sio MATESO na RAHA. shida inavumilika lakini mateso hayavumiliki. Na wanawake wengi wanataabika kwenye ndoa kwa sababu ya hilo neno SHIDA wakiamini SHIDA=Mateso.
Huyu bwana angekuwa na hilo tatizo tu la low sperm count hiyo ni SHIDA na huyu dada ndipo anatakiwa AVUMILIE KWENYE HIYO SHIDA lakini jamaa anachepuka tena waziwazi halafu eti huyo dada avumilie kuchepuka kwa mumewe kwa sababu hiyo nayo ni SHIDA!!Khaaa! BIG NO, hayo ni MATESO YA KISAIKOLOJIA na ni HATARI kwa afya. Akimletea UKIMWI je?

Hapo kwenye blue hiyo ni solution ya KIDHANIFU(Utopian) ,yani hivi unaanzaje au unaanza anza vipi kuongeza upendo kwa mtu wa type ya huyu jamaa? Mkuu upendo sio mafuta kwamba unamimina tu kwenye kidumu, its all about MOYO WA MTU WENYE HISIA. hivi hisia za kuongeza upendo zitatoka wapi JITU lenyewe hata nyumbani halilali?kuchepuka kila siku...lol labda huyu dada awe katolewa nyongo ndio anaweza hivyo. Na hii ndio imani potofu waliyonayo wanawake wengi kwa kuamini katika situation kama hii ni kuongeza upendo tu then jamaa atarudi kundini.....kichepuka ni SILKA, na SILKA si tabia kwamba unaweza kuibadili.
 
Habari za asubuhi wapendwa,

Mimi ni member wa Jamii Forum kwa muda mrefu ila nimesajili ID mpya kwa sababu maalum na hayo niliyooyandika ni ya kweli na ndio hali halisi

''Unaroho mbaya ndio maana huzai'' ''Najuta kwa nini nilikuoa wapenzi wangu wa zamani ni bora kuliko wewe'' nilikuoa kwa kukuonea huruma''. Haya ndio baadhi ya maneno ya kejeli ambayo nilishawahi kuambiwa na mume wangu.

Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 36, nimeajiriwa na mume wangu ana shughuli zake binafsi. Nina miaka minnne ndani ya ndoa ila sijabahatika kupata mtoto kwa sababu nimegundulika nina (Polycystic Ovarian Disease (PCOD) na mume wangu kuwa ana low sparm count.

Mume wangu amekuwa ni mtu wa kurudi usiku mara nyingi kuanzia saa sita, siku nyingine analala huko bila hata kuniambia na hata ukimpigia simu hapokei. Asubuhi anakuja anakuambia tulikuwa tuna biashara tunafanya na simu niliacha kwenye gari. Tukawa tunagombana kwa ajili hiyo hadi tukalifikisha kwa wazazi akagombezwa aakaacha kwa uda lakini karudia tena.

Siku moja alilala tena nje bila taarifa, nikampigia simu hakupokea, ilipofika alfajiri nikapigiwa na mwanamke simu akaniambia acha kusumbua waume za watu, niko naye hapa. Kama ni mumeo mbona hayuko kwako? Kidogo nizimie ila nikapiga moyo konde. Alivyorudi nikamuuliza akasema tulikuwa naye kwenye biashara kwa hiyo alikuwa na simu zetu.

Khaaa nikamwabia mdanganye mtoto ile sio mimi. Baada ya mwezi mmoja akanunua mzigo kumbe ulikuwa wa wizi akakamatwa na polisi, akaniambia mke wangu nimekamatwa kesho njoo polisi kijitonayama, hapo ilikuwa usiku. Kesho asubuhi naenda polisi kumpeleke breakfast nikaambiwa mbona mkewe kaja kuleta chai! Nikwwmbie polisi mbona mimi ndio mkewe halali? Nilidhalikika kwa kweli nikaondoka na chai yangu. Bahati nzuri nilikuwana ndugu zangu ambao ni polisi tena wana vyeo hapo kituoni, nikaweza kufuatilia hadi kesi ikaishia polisi.

Siku hiyo ya kutoka ilikuwa mida ya saa kumi na mojo, muda huo nilikuwa natoka kazini, nikawapigia maafande wakasema mume wako ameshatoka. Nikajaribu kumpigia simu yake haipatikani, kesho yake anarudi nymbani ananiambia polisi waliturudisha ndani. Nikamwabia acha uongo mie ndugu zangu walinihakikishia kama umetoka, akabisha katakata, ila mtu mwenye akili unajua ukweli.

Baada ya mwezi hivi nikwambia twende kwenye send off ya mtoto wa jirani yetu akadai amechoka, akaniambia huwa unapenda kushadadia vya watu wengine mbona mjomba wangu mke wake kajifungua hujaenda kumsalimia? ''Una roho mbaya na hutaweza kupata mtoto'' mimi huyoo nikaodoka zangu na majirani wengine. Kumbe siku hiyo walitibuana na huyo hawara wake.

Nimerudi kalala fofofo, simu yake inaita tuu. Kwa sababu yule mwanamke alishanipigia na kunitolea mbovu namba yake niliishika. Sikupokea simu kwa sababu sinaga tabia ya kupokea simu ya mume wangu.

Wazo likanijia nikaangalia messege, nikakuta huyo dada anamwabia kume una mkehukuniambia mimi na wewe basi. Kesho yake nikampigia huyo mwanamke akaniambie story yoote na ile siku aliyotoka polisi kumbe alilala kwake. Akanimbia mimi nilidanganywa na mumeo kwamba hana mke, na nilishawahi kuja hapo nyumbani pindi ukiwa umesafiri. Na kwa vile nimeujua ukweli simuhitaji tena huyo mwanaume, na roho inaniuma kutembea na mume wa mtu kitu ambacho kinaniumiza ila sikujua naomba unisamehe.

Pamoja na hayo yote anakataa katakata kuwa hana uhusiano na yule dada. Eti ''huyu dada ni girl friend wa rafiki yangu wamegombana ndio ananiforwadia hizi messege.''

Na hii sio mara ya kwanza alishawahi kuwa na mwanamke mwingine akamdanganya kuwa hajaoa hadi huyo mwanamke akaja nyumbani kuhakikisha ndio akaujua ukweli. Pindi anapokuwa na michepuko kejeli haziishi mara najuta kwa nini nilikuoa, nimekuoa kwa kukuonea huruma etc. Hizi kejeli huwa nikizikumbuka nakosa raha kabisa. Na tendo la ndoa tunaweza kufanya mara mbili kwa wiki kila akija amechoka.

Niko njia panda naona nimemchukia mume wangu ghafla, majukumu mengine ya nyumbani nafanya kawaida kama mke .

Kila mara nafikiria uamuzi wa kuachana naye lakini najiuliza is it a right decision:

Naombeni ushauri ndugu zangu wenye uzoefu na haya mambo.

Nawakilisha na mnakaribiswa kwa michango yenu

Dada wakat fulan kutengana ni muhimu na lazima!! Ili kila mmoja aone nafasi ya mwenzie ktk maisha yake ni ipi!!

Alikupenda kwa lengo la kupata watoto ila si mapenzi kutoka moyoni!!!

Jipe break! mpe break! Na ktk hiyo break trust me utapata majibu ya way forward yote! Whether ni wewe ndo unamhitaji au yeye au wote mnahitajiana!
Mungu akusaidie sana
 
Kwa ushauri kama huu kwa nini divorce rate ya TZ isiwe kama huko magharibi!!
 
Nafurahi sana nikikutana na watu kama wewe wanaotumia ubongo na si hisia kufikiri....shida na raha haimaanishi mume kulala nje...akifilisika simwachi...ndo shida hiyo....akiktwa miguu simwachi....lakini kukitembeza mchana kweupe....hell no!

Kuna mdada tena mumewe alikuwa MD alikitembeza weeee peku peku in the name of kusaka baby...hakupata cha baby wala nini na tushawazika long time....watu vumilia, vumilia....sali ...sali....aya kenda mbinguni..

Na umeniua hapo uliposema upendo si kama switch una turn on and off...mwanaume wa hivi unaendeleaje kumpenda???? watu wana mix upendo na dependency (be it financial or emotional)

hapo kwenye RED mkuu SHIDA si sawa na MATESO. Kiapo kilisema SHIDA NA RAHA sio MATESO na RAHA. shida inavumilika lakini mateso hayavumiliki. Na wanawake wengi wanataabika kwenye ndoa kwa sababu ya hilo neno SHIDA wakiamini SHIDA=Mateso.
Huyu bwana angekuwa na hilo tatizo tu la low sperm count hiyo ni SHIDA na huyu dada ndipo anatakiwa AVUMILIE KWENYE HIYO SHIDA lakini jamaa anachepuka tena waziwazi halafu eti huyo dada avumilie kuchepuka kwa mumewe kwa sababu hiyo nayo ni SHIDA!!Khaaa! BIG NO, hayo ni MATESO YA KISAIKOLOJIA na ni HATARI kwa afya. Akimletea UKIMWI je?

Hapo kwenye blue hiyo ni solution ya KIDHANIFU(Utopian) ,yani hivi unaanzaje au unaanza anza vipi kuongeza upendo kwa mtu wa type ya huyu jamaa? Mkuu upendo sio mafuta kwamba unamimina tu kwenye kidumu, its all about MOYO WA MTU WENYE HISIA. hivi hisia za kuongeza upendo zitatoka wapi JITU lenyewe hata nyumbani halilali?kuchepuka kila siku...lol labda huyu dada awe katolewa nyongo ndio anaweza hivyo. Na hii ndio imani potofu waliyonayo wanawake wengi kwa kuamini katika situation kama hii ni kuongeza upendo tu then jamaa atarudi kundini.....kichepuka ni SILKA, na SILKA si tabia kwamba unaweza kuibadili.
 
Nafurahi sana nikikutana na watu kama wewe wanaotumia ubongo na si hisia kufikiri....shida na raha haimaanishi mume kulala nje...akifilisika simwachi...ndo shida hiyo....akiktwa miguu simwachi....lakini kukitembeza mchana kweupe....hell no!

Kuna mdada tena mumewe alikuwa MD alikitembeza weeee peku peku in the name of kusaka baby...hakupata cha baby wala nini na tushawazika long time....watu vumilia, vumilia....sali ...sali....aya kenda mbinguni..

Na umeniua hapo uliposema upendo si kama switch una turn on and off...mwanaume wa hivi unaendeleaje kumpenda???? watu wana mix upendo na dependency (be it financial or emotional)

Mkuu asante, unajua kuna assumptions/theories nyingi wanawake huwa wanamezeshwa wakati wa wa ndoa na nyingi ni negative na wanawake wanazibeba na kuishi nazo kwenye ndoa kwa mateso makubwa. Kisa tu aliambiwa na bibi/somo/kungwi kuwa ndoa ni uvumilivu....hii hatari sana ,kuna haja ya kubadilika kwa kweli.
 
Back
Top Bottom