Habari za asubuhi wapendwa,
Mimi ni member wa JamiiForums kwa muda mrefu ila nimesajili ID mpya kwa sababu maalum na hayo niliyooyandika ni ya kweli na ndio hali halisi
''Unaroho mbaya ndio maana huzai'' ''Najuta kwanini nilikuoa wapenzi wangu wa zamani ni bora kuliko wewe'' nilikuoa kwa kukuonea huruma''. Haya ndio baadhi ya maneno ya kejeli ambayo nilishawahi kuambiwa na mume wangu.
Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 36, nimeajiriwa na mume wangu ana shughuli zake binafsi. Nina miaka minne ndani ya ndoa ila sijabahatika kupata mtoto kwa sababu nimegundulika nina (Polycystic Ovarian Disease (PCOD) na mume wangu kuwa ana low sparm count.
Mume wangu amekuwa ni mtu wa kurudi usiku mara nyingi kuanzia saa sita, siku nyingine analala huko bila hata kuniambia na hata ukimpigia simu hapokei. Asubuhi anakuja anakuambia tulikuwa tuna biashara tunafanya na simu niliacha kwenye gari. Tukawa tunagombana kwa ajili hiyo hadi tukalifikisha kwa wazazi, akagombezwa akaacha kwa muda lakini karudia tena.
Siku moja alilala tena nje bila taarifa, nikampigia simu hakupokea, ilipofika alfajiri nikapigiwa na mwanamke simu akaniambia acha kusumbua waume za watu, niko naye hapa. Kama ni mumeo mbona hayuko kwako? Kidogo nizimie ila nikapiga moyo konde. Alivyorudi nikamuuliza akasema tulikuwa naye kwenye biashara kwa hiyo alikuwa na simu zetu.
Khaaa nikamwambia mdanganye mtoto ila sio mimi. Baada ya mwezi mmoja akanunua mzigo kumbe ulikuwa wa wizi akakamatwa na polisi, akaniambia mke wangu nimekamatwa kesho njoo polisi Kijitonyama, hapo ilikuwa usiku. Kesho asubuhi naenda polisi kumpelekea breakfast nikaambiwa mbona mkewe kaja kuleta chai! Nikawaambia polisi mbona mimi ndio mkewe halali? Nilikasirika kwa kweli nikaondoka na chai yangu. Bahati nzuri nilikuwa na ndugu zangu ambao ni polisi tena wana vyeo hapo kituoni, nikaweza kufuatilia hadi kesi ikaishia polisi.
Siku hiyo ya kutoka ilikuwa mida ya saa kumi na moja, muda huo nilikuwa natoka kazini, nikawapigia maafande wakasema mume wako ameshatoka. Nikajaribu kumpigia simu yake haipatikani, kesho yake anarudi nyumbani ananiambia polisi waliturudisha ndani. Nikamwambia acha uongo mie ndugu zangu walinihakikishia kama umetoka, akabisha katakata, ila mtu mwenye akili unajua ukweli.
Baada ya mwezi hivi nikamwambia twende kwenye send off ya mtoto wa jirani yetu akadai amechoka, akaniambia huwa unapenda kushadadia vya watu wengine mbona mjomba wangu mke wake kajifungua hujaenda kumsalimia? ''Una roho mbaya na hutaweza kupata mtoto'' mimi huyoo nikaondoka zangu na majirani wengine. Kumbe siku hiyo walitibuana na huyo hawara wake.
Nimerudi kalala fofofo, simu yake inaita tu. Kwasababu yule mwanamke alishanipigia na kunitolea mbovu namba yake niliishika. Sikupokea simu kwa sababu sinaga tabia ya kupokea simu ya mume wangu.
Wazo likanijia nikaangalia message, nikakuta huyo dada anamwabia kumbe una mke hukuniambia mimi na wewe basi. Kesho yake nikampigia huyo mwanamke akaniambia story yote na ile siku aliyotoka polisi kumbe alilala kwake. Akanimbia mimi nilidanganywa na mumeo kwamba hana mke, na nilishawahi kuja hapo nyumbani pindi ukiwa umesafiri. Na kwa vile nimeujua ukweli simuhitaji tena huyo mwanaume, na roho inaniuma kutembea na mume wa mtu kitu ambacho kinaniumiza ila sikujua naomba unisamehe.
Pamoja na hayo yote anakataa katakata kuwa hana uhusiano na yule dada. Eti ''huyu dada ni girlfriend wa rafiki yangu wamegombana ndio ananiforwadia hizi messege.''
Na hii sio mara ya kwanza alishawahi kuwa na mwanamke mwingine akamdanganya kuwa hajaoa hadi huyo mwanamke akaja nyumbani kuhakikisha ndio akaujua ukweli. Pindi anapokuwa na michepuko kejeli haziishi mara najuta kwanini nilikuoa, nimekuoa kwa kukuonea huruma etc. Hizi kejeli huwa nikizikumbuka nakosa raha kabisa. Na tendo la ndoa tunaweza kufanya mara mbili kwa wiki kila akija amechoka.
Niko njia panda naona nimemchukia mume wangu ghafla, majukumu mengine ya nyumbani nafanya kawaida kama mke.
Kila mara nafikiria uamuzi wa kuachana naye lakini najiuliza is it a right decision:
Naombeni ushauri ndugu zangu wenye uzoefu na haya mambo.
Nawakilisha na mnakaribiswa kwa michango yenu