Kweli huyo ni mwanaume wa shoka! Na ushahidi wote huo anakataaa,hakika mwanaume kamili hata akifumaniwa live hakubali.
Sasa dada yangu nikupe pole nyingi sana, dunia hii imejaa dhiki nyingi sana,maumivu mengi sana na kibaya zaidi anaekusababishia maumivu ni yule wa karibu yako kuliko wote,mi hunijui hivyo hata nikutukane vipi hutaumia kama wakaribu yako akikukanyaga tuu! Na hii inatokana na mtazamo wako juu yake,pindi unapomtazama mtu yoyote kwa mtazamo hasi hapo ndipo mwanzo wa uchungu na maumivu kwako. Inasemekana umwaonapo alivyo ndivyo ulivyo wewe!
Hapa umeeleza upande wa pili ila yako haujaeleza na kama mwanadam hautakua mkamilifu, na kwa maana hio kunauwezekano hili tatizo asili yake ni wewe, pengine kuna sehemu haukutimiza wajibu wako kama mke na ndipo tatizo likaanzia hapo. Polee sana ,mi naamini katika Mungu,hayo yoote ni madoga sana kwake iwapo tumaini lako likiwa kwake, chakwanza angekupa Amani ya moyo,furaha,upendo na kuvumilia kwingi.
Dada yangu kwa imani uliokua nayo Sali sana kwa Mungu,Tubu sana kwa mumeo na kwa hao hawara zake wote,Tubu sana kwaajili yako na kwa wanawake wote wanoteseka kwenye ndoa zao itakusaidia sana hii katika imani,jitafakari tangu ulipovunja ungo ni wangapi uliowaumiza na utubu,usijefikiria hata mara moja kuvunja ndoa tena tubu kwa wazo hilo,omba sana uvumilivu,mpende mumeo kuliko maelezo,muombee sana,Mwenyezi Mungu akupe nguvu mama yangu ukayapite haya kwa usalama. Dada uonapo usiku umekua mnene sana ujue mapambazuko yamekaribia.