MANENO MENGINE!!... Nini maana na asili ya maneno haya?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MANENO MENGINE!!... Nini maana na asili ya maneno haya??

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by WomanOfSubstance, Aug 7, 2011.

1. WomanOfSubstance

WomanOfSubstance JF-Expert Member

#1
Aug 7, 2011
Joined: May 30, 2008
Messages: 5,465
Likes Received: 72
Trophy Points: 0
Leo nilikuwa kwenye ibada, ikawepo haja ya kutafsiri neno "Ghost" basi mhubiri akasema "Mzuka"... mbona miguno na vicheko vilitawala!

Nikawa najiuliza mhubiri hajui kuwa "Mzuka" ina maana tofauti kabisa?

Nikazidi kujiuliza, kuna maneno mengi tu siku hizi ukiyatamka watu hupata maana tofauti.
Mfano mzuri ni tangazo la radio kuhusu utumiaji wa pombe.."ulevi noma!".... hili tangazo kuna siku lilizusha mjadala mkali sana.Vijana walikwa wanashangaa iweje tangazo la polisi kusifia pombe?...

Wajuzi hebu tuangalie baadhi ya maneno yenye maana zaidi ya moja tena maana zenye kukinzana.

1. Mzuka -inamaanisha mtu aliyekufa lakini pia lina maana nyingine kabisa ....
2. Noma - hebu tufafanulieni maana yake...
Ongezeeni na mengine.

Inawezekana kabisa kukawa na thread yenye kuzungumzia jambo hili.Kama ipo basi naomba mods muunganishe lakini tuendelee kupeana shule ya kiswahili.

Asanteni

2. Nyani Ngabu

Nyani Ngabu Platinum Member

#2
Aug 7, 2011
Joined: May 15, 2006
Messages: 73,651
Likes Received: 35,409
Trophy Points: 280
Lakini hapo kwenye 'mzuka' mhubiri wala hajakosea. Huenda wanamaombi wengi ndo hawajui maana halisi ya hilo neno na wanachojua ni ile maana ya mtaani.

3. Ze burner

Ze burner JF-Expert Member

#3
Aug 11, 2011
Joined: Jan 5, 2011
Messages: 460
Likes Received: 2
Trophy Points: 33
Waumini walichekelea ujinga wao coz hata kama utaondoa maana halisi ya kilugha ya mzuka wangepaswa kufahamu pia mtumiaji wa lugha husika ana fursa maalum ya kutumia lugha atakavyo kimazungumzo ambayo italenga maana nyengine tofauti anayoikusudia. mf. ninapomuita mtu shetani nini maana ya ndani ninayoikusudia.. hayo mahubiri yalikua vijijini nini?

4. MAMMAMIA

MAMMAMIA JF-Expert Member

#4
Aug 12, 2011
Joined: Feb 26, 2008
Messages: 3,822
Likes Received: 23
Trophy Points: 0
Sijui kama nitakuwa nimechangia kwa mujibu wa mada, lakini nafikiri mara nyengine hiii husababishwa na tabia yetu ya kutafsiri dhana za Kiingereza katika Kiswahili chetu.
Fikiria maeneo au dhana hizi.
- Amehukumiwa "chini" ya kifungu cha Sheria Nambari XYZ ya makosa ya jinai. Hapa neno chini tumechukua toka Kiingereza under wakati kwa Kiswahili halileti maana yoyote. Neno lingefaa zaidi ni "kwa mujibu wa".
- "Mwisho wa siku" yeye ndiye atakaye athirika- tumekuwa tukitumia maneno at the end of the day pengine hata hatujui tunasema nini. Kwa nini basi tusitumie maneno kama mwisho wa wiki, mwezi na mwaka?. Neno mwisho peke yake lingetosha. Nakumbuka pia zamani, kabla ya "mwisho wa siku" watu walikuwa wanatumia "Mwiso wa yote/Baada ya yote" au "Mwisho wa habari".

5. X-PASTER

X-PASTER Moderator

#5
Aug 18, 2011
Joined: Feb 12, 2007
Messages: 11,651
Likes Received: 105
Trophy Points: 160
Noma: (Ni neno la kiswahili) Uzuizi, Uzuivu, Upinzani, Pingamizi, Mkingamo, Mkinga, Mgogoro, Uzuio, Masumbuo, Sumbuo, uzuwiaji, Uzuiaji, Masumbulizi, Kipingamizi, Masumbufo, Makinzano, Mfungizo, Kizuio, Kizuizi, Kikwazo, Masubuko.

Ghost: Mzimu, Mzuka, Zuka, Zimwi, Njozi, Kizuka, Kivuli, Masuka, Pepo, Roho (kidini)

6. Bujibuji

Bujibuji JF-Expert Member

#6
Aug 18, 2011
Joined: Feb 4, 2009
Messages: 35,322
Likes Received: 22,146
Trophy Points: 280
nini asili na maana ya neno "afande"

7. X-PASTER

X-PASTER Moderator

#7
Aug 18, 2011
Joined: Feb 12, 2007
Messages: 11,651
Likes Received: 105
Trophy Points: 160
Afande (title of rank) Ni neno linalotokana na Lugha ya Kituruki (Turkish), Kiarabu (Afandī أفندي) au Kiajemi آفندی effendi.

(efendi hutumiwa na askari na polisi au maafisa wenye vyeo vya juu serikalini na haswa likitumika sana enzi ya utawala (Dola) y/wa Ottoman Empire)

8. nyabhingi

nyabhingi JF-Expert Member

#8
Aug 19, 2011
Joined: Oct 12, 2010
Messages: 10,896
Likes Received: 5,358
Trophy Points: 280
hivi hayakuwepo maneno mengine mpaka yatumike haya;
kibwebwezo=computer
kibaobonye=mouse
toweo=toilet paper

9. Dio

Dio JF-Expert Member

#9
Aug 19, 2011
Joined: Feb 8, 2011
Messages: 1,278
Likes Received: 4
Trophy Points: 135

kwelı kabısa sıjuı hao maraıa wamecheka nını?

10. X-PASTER

X-PASTER Moderator

#10
Aug 19, 2011
Joined: Feb 12, 2007
Messages: 11,651
Likes Received: 105
Trophy Points: 160
Labda walikuwa hawajui maana ya hayo maneno.

11. X-PASTER

X-PASTER Moderator

#11
Aug 19, 2011
Joined: Feb 12, 2007
Messages: 11,651
Likes Received: 105
Trophy Points: 160
Tarakilishi ni nini?

12. The Boss

The Boss JF-Expert Member

#12
Aug 19, 2011
Joined: Aug 18, 2009
Messages: 37,826
Likes Received: 22,465
Trophy Points: 280
kibaobonye ni keyboard

13. ndetichia

ndetichia JF-Expert Member

#13
Aug 19, 2011
Joined: Mar 18, 2011
Messages: 27,641
Likes Received: 236
Trophy Points: 160

inaonekana wao wamepeleka mawazo yao kwenye ngono zaidi..

14. MAMMAMIA

MAMMAMIA JF-Expert Member

#14
Aug 20, 2011
Joined: Feb 26, 2008
Messages: 3,822
Likes Received: 23
Trophy Points: 0
Kwa vile haya maneno yalianza na ki-bwebwezo, baobonye; nilitarajia na linalofuata lianzie hivyo hivyo, yaani ki-toweo=toilet paper. (lolz!!)
Napendekeza "pauro llitwe pauro"; kwa hiyo "toilet paper=karatasi ya chooni".

15. X-PASTER

X-PASTER Moderator

#15
Aug 20, 2011
Joined: Feb 12, 2007
Messages: 11,651
Likes Received: 105
Trophy Points: 160
Nadhani neno Kisetiri lilifaa sana kwa toiletpaper

16. Ziroseventytwo

Ziroseventytwo JF-Expert Member

#16
Aug 20, 2011
Joined: Mar 27, 2011
Messages: 3,523
Likes Received: 1,516
Trophy Points: 280
Noma,nishai,au soo, nikufanya tendo la aibu...ila anayetenda haoni "noma" (aibu) bali anayemwangalia ndo anamsaidia kuona "noma"(aibu) kwa mfano, mimi nimeamua kukojoa stand ya daladala,palipo na wa2 kibao, nani mwenye "noma"/aibu kati yangu na nyie mnoniangalia? Nyie ndo mnaNOMA..kwa sababu mi nimeona poa tu nikakojoa. Kwa kuwa nyie mna "noma"/aibu basi mnanisaidia kuona noma. Lakini mi cma noma

17. Yo Yo

Yo Yo JF-Expert Member

#17
Sep 3, 2011
Joined: May 31, 2008
Messages: 11,247
Likes Received: 73
Trophy Points: 0
Toilet Paper ni Hiyo ni Chambizi

18. Al Zagawi

Al Zagawi JF-Expert Member

#18
Sep 10, 2011
Joined: Mar 17, 2009
Messages: 1,717
Likes Received: 242
Trophy Points: 160
hapo nlipopigia mstari..kwa kiswahili cha kwetu..kizuka ni mwanamke aliyefiliwa na mumewe na wala si mzimu kwa maana ya ghost kwa kizungu.

19. A

Apta Kayla JF-Expert Member

#19
Sep 10, 2011
Joined: Nov 18, 2010
Messages: 326
Likes Received: 0
Trophy Points: 0

Fax

20. A

ANNANIAS MPALASHI Member

#20
Dec 16, 2012
Joined: Nov 15, 2012
Messages: 7
Likes Received: 0
Trophy Points: 0
Afande ni askari wa namna yoyote ile yawezakua polisi,mgambo au mwanajeshi

Loading...