El Tiger
Senior Member
- Aug 15, 2018
- 142
- 785
Umenena vema mkuu ila kuna kitu kimoja hujakigusia, MAMLAKA kwa mwalimu na hiyo timu ya nyuma ya pazia
Mkuu fuentte Sijagusia suala hilo la MAMLAKA kwa undani kwa sababu nilikuwa najaribu Mjibu Mdau mmoja kuhusu namna 300m inaweza kutumika vizuri kama kuna Muundo Mzuri Nyuma ya Pazia.Kwa trend hii madhani kulikuwa na maelezo toka juu kuhusu bwana Rashford,Martial na waingereza wengine weng
Mwalimu Hawezi kuwa na Mamlaka kama Hafahamu anajibu kwa Nani Masuala ya Kimichezo. UTD ilikuwa na Mkurugenzi mtendaji ila Mwenye Kujua michezo KENYON baadae akaja GILL, Wote walikuwa wanafahamu kutengeneza Uwiano kati ya Michezo na Masuala ya Biashara.
Ukimsikiliza MOU akihojiwa na RIO unaona shida kubwa ilikuwa kukosekana kwa Mizania ya Biashara na Masuala ya Kimichezo, Yeye anasema Woodward alikuwa mtu "Smart" na hili lipo wazi UTD haina mafanikio makubwa Uwanjani lakini Jamaa kapata dili nyingi sana kubwa za kibiashara. Ila kwa maelezo ya MOU unaona kabisa Wamiliki na Uongozi wa Juu hawakuwa wanajua wanachohitaji kwenye Masuala ya Kimichezo.
Sasa ETH Hawezi zungumza na Arnold ama Murtough Masuala ya michezo kwa Ukubwa huo. Kuna makala Moja ilikuwa inasema Karibu sajili zote ETH hakuweza letewa chaguo la kwanza,
ETH ana sehemu yake ya lawama lakini UTD namna Ipo ni ngumu sana mwalimu yeyote kufanikiwa kwa Muundo uliopo sasa {Ambao tunaelekea uacha}.
Angalia Mishahara wachezaji wanachukua na Jinsi imeharibu Uwezo {Martial, Pogb, n.k}
Inatakiwa tu INEOS wasafishe sasa Nyumba zije Samani Mpya {Mourinho hakoseagi sana}
{Hapa ni rahisi mwalimu kuwa na MAMLAKA, Mfano mzuri Arteta, Ametoa kina Ozil, Auba, Lacca, n.k leo ana timu ya Taswira yake} UTD ina wachezaji wa kila Mwalimu tangu Fergie ni ngumu sana kuunganisha hasa kwa tabia za wachezaji wa kileo.