Forgotten
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 3,634
- 11,116
Juzi kafunga goli angekuwa Rashford angejiangusha.Huyu Mitoma hapo Brighton anasubiri nini?
Yule Chief Executive wao nilisikiliza interview yake wale jamaa wana mipango sana. Anasema wao badala ya kusaka wachezaji kwenye mataifa makubwa wanaenda zile nchi ndogo, kama ni South America hawaendi Argentina wala Brazil wao wanaenda Ecuador.
Akamalizia kwa kusema wao kabla hawajauza mchezaji tayari kuna mtu wa kuchukua nafasi wanakuwa wamemuandaa.
Ndiyo nikawaza timu yetu inaendeshwa vibaya. Tunatumia pesa nyingi kwa wachezaji wenye viwango vya kawaida, wakati Brighton wanajibebea mafundi na wapiga kazi kwa pesa ya karanga.
Yule Rangnick na Solskjaer ni watu ambao wanajua kupata talents. Wangepewa nyadhfa kwenye timu isipokuwa ukocha huenda wangetufikisha mbali sana.
Sasa hivi ni wazi pesa siyo kila kitu kwenye football kama hamjui matumizi yake.