Jamie Carragher -
"Bei za Rice na Caicedo ni bargain. Pia ni dili nzuri.
Ushahidi wa hilo ni pauni milioni 70 ambazo Manchester United walilipa msimu uliopita kwa ajili ya Casemiro.
Mbrazil huyo ataishia kuigharimu United zaidi ya Arsenal na Chelsea walivyolipa Rice na Caicedo. ."
"Caicedo na Rice ni mifano ya kufikiria mbele - kuokoa pesa kwa miaka sita au saba ijayo ambapo watachukua jukumu lao."
"Sikuwahi kuamini kwamba Casemiro angekuwa na thamani hiyo ya pesa. Sio kwa sababu kuna shaka yoyote na uwezo wake amekuwa mchezaji wa kiwango cha juu . Lakini kwa sababu yuko katika hatua ya mwisho ya kazi yake ambapo hawezi kulipa kikamilifu ada kubwa ya United.
Ni panic buy alipojiunga mwaka mmoja uliopita, alinunuliwa mara tu baada ya kushindwa kumfuatilia Frenki de Jong kutoka Barcelona"
"Casemiro alikuwa bora kama mtu yeyote duniani wakati huo. Sasa kuna hatari United wanaweza kuwa na anasa ya gharama kubwa wasiyoweza kumudu.
Hawatakuwa washindani wa mataji hadi wampate Rodri, Caicedo au Rice wao wenyewe."
(@YahooSports)