Han Kyul
JF-Expert Member
- Aug 15, 2023
- 264
- 529
Talent ID:katika miaka yangu yote ya kushabikia soka hili neno sijawahi kutana nalo likizungumziwa na ninafuatilia sana mpira na kwa mara ya kwanza naliona kwa kocha wa United na sikuona huko nyuma kwa makocha matapeli wote inachekesha sana[emoji1316][emoji23][emoji23]Taratibu maji yanaanza jitenga na mafuta
Niliyoyasema miezi kadhaa kuhusu 7hag taratibu Yanaanza kuonekana kwa mbali
Erik ten hag Mfukoni mwa Gary O' Neil |
Anasema
[emoji3578]Mtaumia kusema hivi, lakini Chelsea wanaonekana ni timu bora uwanjani kuliko United na ni miezi miwili TU tangu Pochettino apewe timu... Wakati huo huo 10hag ni miaka miwili na United hii inayoonekana kuwa ya Hovyo kabisa.
[emoji3578]Nimeanza kuwa na wasiwasi kuhusu juu y Talent ID ya 10 hag.. Msimu uliopita, United walikuwa na tatizo kubwa la kushindwa kuutawala mchezo, hawana kiungo ambaye ana uwezo wa kudhibiti kasi ya mchezo, ( Control the tempo)
[emoji3578]Msimu mpya lakini tatizo bado ni lile lile, walimsajili Meson Mount, ni usajili mzuri, lakini kama mchezaji TU wakikosi (Squad player) lakini kumchezesha pamoja na Bruno na Casemiro kunaonekana hakutofanikiwa wote watatu hakuna hata mmoja mwenye uwezo wa kuutawala mchezo "
I know kila kitu cha United lazima kitafutiwe kasoro na watu wazembe[emoji23]
Halafu sasa mzee huoni Chelsea inavyosajili for fun?
Wao wameuza wachezaji ndio maana wanaingiza wachezaji wengine huku sisi deadwoods wetu hawauziki na kabla ya kupata replacement zao lazima wauzwe kitu ambacho kigumu sana.
Wanasajili wachezaji hata 8-10 kwa dirisha tena ila sisi tukijikamamua ni 3-5.hapo kuna wale wa deadline day kuwaridhisha mashabiki.
Chelsea wana mmiliki ambitious sana na pia kuna watu wanaomsaidia kocha hiyo sekta ndio maana wanaingiza tu watu na washamfanyia umafia Liverpool.
Huku kwetu tuna Arnold na Murtough mchezaji mmoja anafukuziwa miezi hata 3-4,tatizo lipo kwa uongozi hebu siku moja ETH apate DOF na Technical Directors wanaojua soka uone kama hizo ngonjera za hiyo mnayoita Talent Id zitakuwepo.
Mbona akiwa Ajax aliingiza watu wazuri ama ndio yale niliyosema juu hapo kuwa kwa United hata Pep anaweza kuonekana tapeli.