Forgotten
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 3,634
- 11,116
Sasa hapo ndiyo maana tunataka Glazers waachie timu. Kocha lazima awe na watu wanaojua football kumpa support kitu ambacho kwasasa United hakipo.Mm nakubaliana na wewe kuzidiwa msimu wa kwanza ,ila lazima Kuna key points tuziangalie ,ambazo zitasaidia kujua mbelen atafika mbali zaidi,
Kwangu mm Ole gunar anabaki moja ya watu wenye talent ID kubwa ni vile hakupewa Uhuru,huyu ndiye aliwataka kina halland, Bellingham,Sancho,n.k wakiwa hawaeleweki, huyu ndiye alimuamin Greenwood had leo mnamkumbuka
Niliwahi fanya mijadala huu na ambangile anaamini ETH kwenye Talent ID bado kwa Ole ,ila anaweza kuwa na mbinu nzuri za ukocha kuliko ole Gunar
Ole ni kocha mzuri sana. Style yake ilikuwa speed, quick transitions na counter attacks. Huu ndiyo mpira aliotesa nao babu Fergie na ndiyo identity ya United.
Tulishuhudia Pep Gurdiola akinyanyaswa na Ole na kupigwa nje ndani ktk msimu. Tatizo kubwa la Ole ni man management, asingeweza kufika mbali bila kuwa katili.
Ninachoona EtH anapata ugumu kwasababu wachezaji aliowakuta hawafai kwenye system anayotaka kucheza yeye.
EtH anataka timu yake imiliki mpira kwa 75% ktk mchezo, hiki kitu ni rahisi kusema kuliko kufanyika kwasababu siyo identity ya United so ukifuatilia wachezaji wote waliosajiliwa kabla ya EtH walikuwa wanafaa kwenye quick transition & counter attacking football.
Ole na EtH wanatumia aina tofauti kabisa ya uchezaji, nilitegemea utagundua hili na kujua kuwa ni ngumu kuwabadilisha wachezaji kwasababu kumiliki mpira kwa 75% ni lazima uwe na wachezaji wanaoweza kupiga pasi kwa usahihi.
Je, kwa wachezaji walewale wa transition football unaona hili likikamilika kirahisi?
Ndiyo maana huwa nasema inabidi mjue kwanini Glazers hawahitajiki, ktk miaka yote hiyo walipaswa kujua identity ya timu ni ipi. Unapomtoa Ole na kumleta EtH ni rebuild project nyingine inaanza.