Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Hii ndio kazi ya mkurugenzi wa ufundi sana. Mikakati inaanza kufanyika mapema sana na sio kwa ile style ya kuzima moto. (succession plan)

Level ya timu kubwa kama United ili ku-maintain momentum of perfomance unahitaji kuwa na mpango mbadala kwa kila mchezaji muhimu kikosini hata kwa miaka minne mbele.

Shida ya United viongozi wetu wengi wa juu wana maono madogo sana. Kwa nje timu inaonekana kubwa sana ila kwa ndani kuna vilaza wengi sana wasio na shauku kubwa sana ya kupata mataji kila siku.

Ten Hag alipopewa mkataba iliwashtua sana viongozi wengi alipowaambia anataka ku-control mpaka timu ya U-21 ili ajenge mfumo wa ku-connect vijana wadogo na timu kubwa kimfumo wa kiuchezaji.
Ikitokea Qatar wameichukua timu.

Kitu cha kwanza ni kufukuza recruitment department ya Man Utd.

Tutafute watu wanaojua kufanya maamuzi sahihi na kwa haraka.
 
Kiungo Jombaa. Hatuna mbadala wa Casemiro. Nafasi zote zilizosalia tunaweza kucheza bila yeyote yule timu ita-struggle kidogo ila tutapata matokeo. Ukimuondoa Casemiro timu inakuwa nyeupe sana.
Huyu hapa anatufaa asee, huyu mwamba hapana.
Bruno Guimaraes
20230226_213605.jpg
 
Tunatakia tupate vijana wenye damu moto hapo latikati.

Sijui Madrid huwa wanafanya vipi kuwa na quality midfield misimu yote, wana jicho kali sana.
Madrid wali struggle sana baada ya kumuuza Makelele mpaka wakaja kumpata Kroos, Casemiro na sasa wana Tchoumeni, Camavinga nk hakika wana jicho kali sana.

Man U ifanye tabia ya kuchukua viungo pale Madrid. Maana hata Makelele alivyoondoka pale Chelsea ilikuwa bora sana.
 
Ten Hag ni mwalimu mzuri.
Kikosi ni almost kilekile Cha msimu uliopita,lakini ameweza kubadili na timu inafanya vizuri, kitu ambacho Makocha wetu akina Klopp wameshindwa.

Kwa kweli man u mnaupiga mwingi..
Vijana wakiendelea kupambana hivi mnaweza beba makombe yote.
 
Hahahahahaa vikombe vingi hapo L'pool walichukuwa kipindi wachezaji wanavaa vichupi chini ya miaka ya 1990.

Kuna mwanangu ni mshabiki wa L'pool toka amezaliwa hakuwahi kushuhudia kombe la EPL ndio mwaka juzi lilipopatikana ikabidi na yeye aende kusheherekea kabisa huko huko.
[emoji13][emoji13][emoji13]wee jamaa wakikusikia wenyewe
 
Ikitokea Qatar wameichukua timu.

Kitu cha kwanza ni kufukuza recruitment department ya Man Utd.

Tutafute watu wanaojua kufanya maamuzi sahihi na kwa haraka.
Man united haina Recruiting department walishafukuzwa mbona, Eth ndio yupo responsible kwenye usajili plus Arnold na Murtough, kuna kipindi walimchukua kwa Muda kaka yake Will Keane naye pia ameshaondolewa.

Ingekua wapo kina Woodward na Timu yake Antony asingesajiliwa.
 
Kwa sasa fans tumeanza kujadili mipango ya usajili msimu ujao ila katika wote sijasikia mtu akiongelea nafasi ya goal keeper. Wakati msimu unaanza wengi tuliona De Gea ni tatizo kwa kuangalia falsafa za uanzishaji mashambulizi za EtH. Sasa tukubaliane moja,tunahitaji shot stopper (Dave) au ball playing Golie(tusajili)?
 
Fred sijui kaanza kupata confidence ya kucheza pembeni ya kaka yake Casemiro,anaupiga mwingi sana recently hadi tumesahau kama Sabitzer yuko benchi.

Anthony kaanza kuimarika kiwango hasa kwenye upande wa ushambuliaji,nahisi wale doubters wake watajua Erik hanaga kazi mbovu.

One down,Three to wrap up!
 
Man united haina Recruiting department walishafukuzwa mbona, Eth ndio yupo responsible kwenye usajili plus Arnold na Murtough, kuna kipindi walimchukua kwa Muda kaka yake Will Keane naye pia ameshaondolewa.

Ingekua wapo kina Woodward na Timu yake Antony asingesajiliwa.
Mbona mambo yanakuwa slow sana sasa?

Inatakiwa dirisha likifunguliwa watu wanasajiliwa in a week then pre season inaanza.

Sio ile mtu anakuja na ligi ishaanza.
 
Kwa sasa fans tumeanza kujadili mipango ya usajili msimu ujao ila katika wote sijasikia mtu akiongelea nafasi ya goal keeper. Wakati msimu unaanza wengi tuliona De Gea ni tatizo kwa kuangalia falsafa za uanzishaji mashambulizi za EtH. Sasa tukubaliane moja,tunahitaji shot stopper (Dave) au ball playing Golie(tusajili)?
Sioni shida ya golikipa as of now.

Huyo huyo anaweza tengenezwa akawa jinsi kocha anataka awe.

Huwa naona goalkeeping ni sensitive area haihitaji majaribio na sio wa kubadilishwa hovyo.
 
Mbona mambo yanakuwa slow sana sasa?

Inatakiwa dirisha likifunguliwa watu wanasajiliwa in a week then pre season inaanza.

Sio ile mtu anakuja na ligi ishaanza.
Dirisha lote lililopita Carrington ndio ilikuwa head of recruitment, Kocha ndio alisema nani na nani aje, hapa ni mpaka timu iuzwe ndio waajiriwe watu wengine si rahisi kuajiriwa mtu katikati ya msimu.
 
Back
Top Bottom