Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

"Lakini inaonekana bodi ya Man united haiko serious na usajili katika timu yao ni kama wanajaribu kubahatisha bahatisha."

Hapo ndiyo tatizo kubwa la United lilipo, shida kubwa inaanzia kwa wamiliki wao ndiyo walitengeneza mfumo wenye watu wasiojua mambo mengi kuhusu football. Watu hao ndiyo wakanunua wachezaji wengi wenye uwezo mdogo wengine wakaletwa kwasababu za kibiashara tu, wengine wala hayakuwa mahitaji ya makocha waliopita. Hayo yote ndiyo yametufikisha hapa tuna kikosi kimejaa majina tu. Hawa wachezaji ndiyo wanatutesa kwasababu hawauziki na hatuwezi kusajili bila kupunguza idadi ya wachezaji tulionao.

Na bado hiyo haitoshi wamiliki hawaweki pesa kwenye timu, wao wanachota tu faida. Msimu huu tumepata kocha mwenye malengo ya kueleweka lakini bado support ya wamiliki ni hamna kitu.

Hata hili la Ronaldo kubaki nina uhakika ni maelekezo kutoka juu, Ronaldo ni brand inayowasidia Glazers kutunisha mfuko. United siyo timu inayofanya cha maana uwanjani lakini bado inafamya vizuri kibiashara kwasababu ya akili wanayotumia Glazers kuliteka soko la mashabiki wa United.

Siku Glazers wakiondoka ndiyo itakuwa mwanzo mpya wa Manchester United. Mimi nimeshachoka kulaumu wachezaji, huu ndiyo uwezo wao walionao sisi tunataka wafanye kama thamani ya pesa tuliowanunulia ila hawa ni average players tukubali tu hali hilisi. Ila rebuild chini ya Glazers itakuwa ni kutwanga maji kwenye kinu.

Maneno ya Mourinho na Van Gaal yataishi milele.
Moriinho kasemaje
 
Hapo anwafundisha nn vijana huyu ndo anatuharibia team ,watu waliokuwa wanampinga walikuwa na sababu muhimu sana.

Kwa sasa aende tu ukizingatia hakuna alichobadilisha katika team ,hana mapenzi tena na club japokuwa mashabiki wanampenda
Muda Bado Aondoke. Namlaumu Sana Ferguson. Ndiyo mujaribufu mkubwa
 
Tukiongea tunaonekana sisi tuna ishu personal na Ronaldo..
Hadi tunaitwa wapumbavu asee.
Huyo jamaa atagharimu morale ya timu ikiwa hizi taarifa zinaenea alafu wachezaji wanaziona, ukute mchezaji kajituma alafu unakuta anayechukua pesa ndefu analeta ujinga na ukosefu wa heshima na hafanywi kitu.


Siku hizi ukute Ronaldo anataka afunge bila kujali hali ya timu ili kutuprove wrong, kwa hiyo sisi tunalalamika hafungi au tunalalamika anapoteza timu kuweza kuchukua Ushindi with consistency. Sio kila yeye afunge, tunapoteza muda mwingi kumpa mipira afunge wakati tukitanguliwa goli ndio imeisha hivyo.

Jamaa asepe tulete watu wa kazi kila mchezaji ajisikie kuitumikia kuleta ushindi, sio kila mchezaji akijaribu kufunga akose mara utasikia Angempasia Ronaldo, Madogo wana Dharau hawamheshimu Ronaldo, sasa kwa lawama hizo tutakua na timu inayojituma kweli?

Yaani hata Confidence ya Bruno kwenye penalty ishaisha, now akikosa utasikia Angempa Ronaldo what the f*ck?

Kama vipi Ronaldo aje kusaidiana na Maguire kwenye Ulinzi.


Maana kila kitu yeye.

Matatizo ni mengi ila tunaweza amsha moto kukiwa na morale ya kueleweka.

Morale ikifa kila mchezaji ni takataka.
 
Anatuangusha sn watu tulio nyuma yake tukimpigania kwa hali zote, anatunyima maneno ya kuongea mbele ya wabaya wake. Ni mpumbavu.
Finally Boss, tushasema hatuna tatizo ya yeye kufunga, tatizo yeye yeye kila kitu hadi timu inakosa kucheza kitimu.

Ona sasa morale inaenda kuporomoka akirudishwa tena baada ya kusepa after sub, ukute wengine wapo huko wanajiandaa kuingia kambini.

Anajivunjia heshima sana.
 
Mara 100 hawa strikers tulionao kuliko huyo Ronaldo.

Mchezaji amerudi juzi, leo anataka apangwe.

Na juzi alikuwa anataka kuondoka.

Glazers wanaiua hii club.

WTF is Ferguson doing in Man Utd?
Acha tu, ukute mechi ya Brighton atakuwepo na atataka kila chance apige yeye kule golini.
Lengo kutuprove wrong, wakati haoni anaua chemistry kule mbele.
 
Yaan mashabiki w nyumbu ni wa hovyo sana, leo hii mnatafuta w kumbebesha lawama, ronald ndio mmeamua awe mbuz w kafara.
 
Wale wapuuzi sasa hivi hawapo
Uwe unapitia mzee

Wamebaki watukutu wachache sana

Kama Flano amekua mstaarabu na heshima juu kule jukwaani
mi hua napenda tu kuwazingua halafu mnajaa upepo.
Ila msimu huu mko vizuri kinoma mpaka tunawaonea wivu.
Ila Arsenal ni Arsenal tu hata ikipewa kikosi kizima cha Manchester City bado itashindwa kuchukua kombe lolote la maana.
 
Alex Telles anaondoka pia, left back tunabaki na Shaw na Malacia.. Deal ya Laird kwenda Watford sijailewa kabisa, Dalot na AWB sioni mwenye afadhali basi tu
Dalot na AWB hamna mwenye nafuu..

Ila yule AWB wa msimu wa kwanza atleast alikuwa kisiki..one on one hizi alikuwa haachwi kibwege na blocks alikuwa anazifanya sana.. sijui amepatwa na nini.

Tunahitaji some improvements on RB..
 
Back
Top Bottom