Hawa ndio mashabiki wa Man utd wasio hata na chembe ya uvumilivu.
Hao Liverpool wanaooneka wazuri hawakujengwa kwa msimu mmoja pekee,kulikua na wachezaji kibao vimeo wakina sturidge,moreno n.k wakaanza kuchujwa mmoja mmoja mpaka ukatengenezwa mfumo ambao kila mchezaji akija anafit.
Na bado mashabiki wa Liva wakavumilia japo hawakuchukua ubingwa wa epl miaka 30,leo hii wanakula matunda.
Hapa tuna mwezi mmoja tu na Ten Hag ,ten pre season watu tunatoa mapooovu,tunataka kufanya ujinga ule ule wa kunnunua tu bila kutengeneza mfumo.
Bado tuna safari angalau misimu miwili tuwe vizuri,tuvute subira tusijaribu kujifananisha.
Trust the process.