Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Ngoja nitoe mfano huu kwa dhumuni la kujadili swala la frankie de jong: Jaalia manchester united ni boti, dau, jahazi au meli. Wakati huo huo erik ten hag (kocha) ndiye nahodha wa hicho chombo. Frankie de jong ndiye atakayekuwa ramani au compass ya kumuongoza nahodha na hiyo boti pindi itakapokuwa safarini (uwanjani). Erik ten hag ameshafanya kazi na frankie de jong hivyo basi hata kama atamsajili siku mbili kabla ya kuanza kwa ligi itakuwa ni rahisi kwa frankie kuadapt mazingira ya kiuchezaji ya kocha ten hag kuliko mchezaji mwengine na changamoto kubwa atakayoipata ni match fitness. Erik ten hag anataka kujenga timu yake kiuchezaji ndani ya uwanja kupitia frankie de jong, kwa lugha nyepesi frank ndiye kampasi au ramani tukiwa na mpira na tusipokuwa na mpira. Frankie atahusika na buildup kwa maana atakuwa wa kwanza kupokea mipira kutoka kwa mabeki, jukumu hili kwa sasa halifanyi vyema pale barcelona kwa sababu position yake anacheza sergio bosquet. Tumuelewe erik ten hag, kama atashindwa kumpata frankie ndio tunamuandalia mazingira ya kufeli kwake.
 
Huwa Mkuu nafurahi sana Tier 1 kama hawa wakiclarify mambo.

Pia Amesema De jong yupo Open Kujiunga Man U, tofauti na Rumors za mwanzo kwamba hataki kuja kwetu.

Kwa usalama wa Afya ya akili yako vyema ukaepuka kabisa hivi ijumaa na uwazi za ulaya.
umenisaidia sana kuvifahamu vyanzo vya taarifa vyenye uafadhali na rubbish, uzuri pia ukitembelea subreddit za timu wanakuwekea list ya chanzo sahihi na takataka. Vijarida uchwara sivifuatilii
 
anaweza kuendeleza moto wake wa kufunga magoli kwa msimu mwengine au pia ikawa kinyume chake. tufahamu darwin nunez ni msimu huu tu amekuwa bora. pia unadeal na benfica. wazee wa kuuza wachezaji wanaotrend kwa bei kubwa kama walivyofanya kwa joao felix.
Hapo yanatengenezwa mazingira tupigwe tena kama kawaida, wacha aende Liverpool haina shida kuliko kutoa mapesa yote hayo kwa mchezaji aliyewika msimu mmoja alafu anatokea timu ndogo, huo ni upuuzi.
 
Chukueni mzigo huo
FB_IMG_1654855889482.jpg
 
Hatupaswi kujiweka daraja moja na manchester city na liverpool kwa sasa, tupunguze kuwashwa washwa mdomo
Mzee unaupiga mwingi sana leo watu wapunguze matarajio. Mimi next season natamani tu ku-enjoy soka safi, kombe angalau moja hata Carabao tu ila ni ngumu maana bado tutakutana na miamba kama City na Liverpool so maybe Europa (I wish) pamoja na kurudi kwenye Champions League tu.
 
Hivi ni nini kimeikumba Barcelona?? Kosa gani kubwa walilolifanya lililopelekea wao kushuka kiuchumi kiasi hicho??

Aiseeeh
Inaitwa Bartonomics. Woodward mbovu ila Bartonomeu wa Barca alikuwa zaidi, alisajili tu wachezaji ovyo ovyo
Coutinho- 145M
Dembele- 130M
Griezman- 120M
De jong - 75M
Pjanic- 60M

Wachezaji 5 tu hao zaidi ya Euro Milioni 500, Jumla amespend zaidi ya 1B.

Ukiangalia kati ya hao wa 5 mmoja tu ndio angalau ana Afadhali, wengine wameflop,

Coutinho kauzwa Aston Villa 20m.

Baada ya kuspend hivyo na Covid ikaja wakawa na Deni kubwa sana kiasi hata kama Mesi angekubali kucheza kwa buku 2 wasingeweza Kumsajili.
 
umenisaidia sana kuvifahamu vyanzo vya taarifa vyenye uafadhali na rubbish, uzuri pia ukitembelea subreddit za timu wanakuwekea list ya chanzo sahihi na takataka. Vijarida uchwara sivifuatilii
Kama unatumia Twitter pitia page ya @centredevils kila habari wana-indicate kama imetoka kwenye Highest quality source au Proven source zinazofuata ni Average reliability, Low reliability, Not reliable na Source under review so ni rahisi kujua habari ipi uamini na ipi usiamini.
 
Back
Top Bottom