Sababu wanazotoa goons wenzio ni kuwa David ni kocha asiyefaa kuwa wa
#ManUnited wanatoa sababu hiyo kwa kocha ambaye hata mwaka 1 hajamaliza klabuni.
Sasa ndio maana nikawaambia kama kigezo cha kufanya vibaya klabuni ndio kiashiria cha kocha kuwa mbovu, mbona Arsene Chenga anaenda mwaka wa 9 sasa bila kuwa na kikombe hata cha mbuzi?
Pili, goons wenzio wanasema David hastahili kuwa
#ManUnited kwa sababu ana uzoefu wa midtable....sasa nikawauliza Arsene Chenga wakati anakuja goons alichukuliwa kwa uzoefu upi? Kwani alitoka nchi ambayo haikuwapo kwenye ramani ya soka!!!
Ni hayo tu chifu wangu.....
Sasa nakupa sababu inayopelekea United kufanya vibaya hadi sasa:
1. Kipindi cha mpito - ili halina ubishi, kwani kwa kile alichokifanya SAF katika miaka 27 ya kuwa OT, siyo rahisi kwa kocha mpya kuja na kuyaishi mara moja. Naamini siku ambayo Arsene Chenga akiondoka goons (msimu huu ndio wake wa mwisho, kwani aliahidi hasipochukua kikombe chochote kile atajiuzulu, na sioni dalili za kuchukua chochote).
Katika kipindi cha mpito, David anapigania na kuepuka kuishi katika kivuli cha SAF; anataka aweke alama yake klabun, jambo ambalo siyo kazi rahisi.
2. Kuchemsha katika usajili wa majira ya joto mwaka jana - hapa napo panahusika. David alikuwa ni meneja mpya na Ed Woodward alikuwa ndio kwanza ameanza majukumu kama executive vice chairman mwenye jukumu pia la kutoa pesa za usajili. Sasa Ed alikuwa mzito mno katika kutoa pesa; hivyo kupelekea David kukosa wachezaji aliowataka. Hapa siasa za usajili ziliwatoa knockout wote. Mwezi huu mambo yataenda vizuri, kwani David tayari ana kikosi chake kipya cha usajili. Timu ilihitaji wachezaji kadhaa wapya karibu katika nafasi zote tatu (beki, kiungo na mbele) za uwanjani (ukitoa golini). Hiyo ni kutokana na usajili uliofanywa na wapinzani na kuongeza nguvu ya wapinzani.
3. Viwango vya wachezaji - viwango vya wachezaji kama Evra, Rio, Tom, Smalling, Kagawa na Javier vimekuwa haviko sawa sana. Ingawa kwa Javier na Shinji, naweza nisiwalaumu sana kutokana na muda mchache waliocheza. Lakini pale wanapocheza, hususani Javier wamekuwa hawapo katika viwango sawa. Shinji amefanya vizuri sana katika UCL. Evra nafikiri muda wake umefika omega; amekuwa hana spidi ya kurudi kwenye LB pale anapopigwa counter attack kwenye upande wake. Tom amepewa sana nafasi lakini hajawa bora katika kusukuma mashambulizi mbele. Smalling naye pale anapocheza kama RB amekuwa uchochoro sana; ingawa kwa upande mwingine siwezi kumlaumu sana kutokana na kwamba yeye siyo natural RB. Akicheza kama CB, uwa anacheza vizuri sana. Rio kazeeka, na nafikiri mwisho wa msimu huu, safari ya kuondoka itafika.
4. Majeruhi - kwa kweli msimu huu timu imekumbwa na majeruhi kwa wachezaji wa muhimu sana. Mfano, RvP, Rafael, Jones, Michael, Vida na Nani. Hii imepeleka timu kukosa consistency. Haswa pengo la Rafael ni kubwa sana; kwani hasipokuwepo yeye RB inakuwa uchochoro wa magoli kwa tiu pinzani. RvP, kutokuwepo kwake kumepunguza nguvu katika mashambulizi, hilo halipingiki.
5. Moyes kutotoa 'hair-dryer' treatment - ni kama bado anawagwaya wachezaji. Wakicheza vibaya, kwenye post-match inteviews anasema wamecheza vizuri. Hata pale uwanjani, anaonekana kutowakaripia wachezaji na kuonyesha who is the boss. Hili limepelekea timu kucheza bila ya
#ManUnited spirit katika mechi nyingi. Mfano, juzi dhidi ya Spurs kwa kweli kabla ya Danny kufunga goli, timu ilicheza kama imekata tamaa vile.
6. Pressure on players, haswa wanapocheza OT - wachezaji wa
#ManUnited hawajazoea kuwa katika hali kama hii. Kupoteza mechi 4 OT, ni jambo ambalo halipo katika veins zao. Sasa hiyo inapelekea kucheza na pressure ya kuogopa kupoteza tena mechi nyumbani. Hata mashabiki OT wamekuwa nao hawana morale sana wa kushangilia timu; ni kama wana fear for the worst katika kila gemu OT. Ni ajabu away fans wamekuwa wakitoa sapoti sana kwa timu.
Hayo ndiyo nayaona kama mambo yaliyopelekea timu kufanya vibaya hadi sasa.
Lakini
#ManUnited ndio klabu kubwa zaidi Uingereza, hivyo itakaa vizuri tu, na mambo yatakuwa sawa.