mishahara ya goalkeepers, yawezekana data hizi si rasmi hivyo naruhusu masahihisho kwa yeyote atakayekuwa na taarifa sahihi.
Allison becker wa liverpool analipwa paundi 150, 000 kwa wiki.
Ederson wa man city analipwa paundi 65000 kwa wiki.
Robert sanchez wa brighton analipwa paundi 20,000 kwa wiki.
Edouard mendy wa Chelsea analipwa paundi 70000 kwa wiki.
ukijumlisha mishahara ya goalkeepers wote wanne unapata paundi 305,000.
Fanya wote hao wanne kwa pamoja wanakusanya paundi laki 350,000 kwa wiki.
Kwa wasiofahamu huo ndio mshahara anaolipwa
david de gea kwa wiki.
mpira wa kileo haumuhitaji tena kipa aina ya de gea ambaye uwezo wake pekee alionao ni kuzuia mashuti yanayolengwa golini kwake huku akiwa na madhaifu mengi, kwa mshahara anaolipwa david alipaswa kutokuwa na mlango wa udhaifu.
- David ana mwaka wa 10 tokea asajiliwe manchester united lakini bado ameendeleza tabia ya uoga wa kucheza krosi, tunafungwa goli nyingi za krosi kwa sababu yake.
- Uwezo wake wa kutawala box bado ni mdogo na haonyeshi dalili ya kubadilika
- Uwezo wake wa kucheza bado ni mdogo, anapiga pasi ovyo.
- David ni shots stopper, dunia ya leo inamuhitaji sweeper si ajabu ndio maana guardiola alimuondoa joe hart na hata arsenal wamemsajili ramsdale, lengo ni kujenga mwingi wa timu kiuchezaji kuanzia nyuma.
- David hawezi kupiga pass zinazoweza kuvuka line moja au mbili ya timu pinzani kwa usahihi mkubwa kama afanyavyo ederson. Mechi ya jana ederson alipiga pasi nyingi sana kama hizo mpaka wivu ukanijaa nafsini.
- Huwezi kucheza higher line ikiwa kipa wako ni david de gea na beki wako ni maguire.
- Uwezo wake wa kuokoa mashuti umerudi tena lakini bado anaendelea kukaa benchi spain, tujiulize ni kuwa sababu gani.
Anacholipwa david de gea hakiendani na anachotupa, ndugu zangu huyu david de gea ana tofauti gani na simon mignolet?
Overhaul inapaswa ianzie kwake kama itawezekana cause mkataba wake unaisha 2023, ni ngumu sana kumuonyesha mlango wa kutokea david de gea lakini klabu inapaswa impunguzie mshahara kama wataona haja ya kumpa mkataba mpya, kumuongezea mkataba na mshahara ni matumizi mabaya ya rasilimali pesa.
Naomba munitajie team kubwa yenye goalkeeper mwenye madhaifu kama hayo aliyonayo david de gea.
Chaguo langu mimi ni huyu sanchez wa brighton, navutiwa sana na uchezaji wake.
View attachment 2141677