Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Mi nadhani tatizo ni crisis management approach ya Man Utd Board. Baada ya kuona macocha wote wanachemsha wakaamua kuingia na hii gear ya CARE TAKER, INTERIM COACH AND MANAGER. This is a very vague approach.

Kwamba, Care Taker, well, he takes care of the team until an interim coach is recruited (this is in a very short horizon), na sasa katika kuchagiza hili inasemekana Michael atakuwa coach mpaka jumapli tutakapocheza na chelsea, just to make it look like they have meant this to be a very brief situation.
- Mimi sintoshangaa Chelsea wakitubamiza tano na wao, sababu the whole this thing is putting Michael in a very awkward situation, sidhani kama atakuwa na utulivu kichwani mwake kukabiliana na hii situation, yaani wanamtumia yeye kama condom then wakimpata mtu wao asepe? au ndio wamlazimishe huyo mtu wao akija lazima amuaccomodate michael na hao jamaa zake wengine waliobaki?

The, INTERIM COACH, UP TO END OF SEASON. Unless wapate Jobless man, ama sivyo, nani atakubali kuachia mkataba wa mwaka mmoja kwenda kufuata mkataba wa miezi sita in a volatile club like man utd. nadhani ndio maana ukisikia maelezo juu ya Ralf inaelezwa mwisho wa msimu ataendelea na consultancy contract ya miaka miwili, huu uongo wakawaambie watoto, Ralf is negotiating a 2+ years contract ila kwa sababu wanaogopa maneno ya kina neville yasijekutokea kweli, kwamba Van Gaal, Mourniho both failed sasa wanaogopa a high profile mwingine asije akachemsha wakati anamkataba mrefu n.k so wanamuwekea hayo mambo ya consultancy, na sidhani kama Ralf atasign huo mkataba.

Alafu eti Manager, yaani Board imekuwa na akili za kizamani kwelikweli za kutaka kumpa mwanamke mimba kuprove kama anauwezo wa kuzaa ndio aolewe, Ralf akisign huo mkataba namna hiyo hiyo hata kama atataka akina Michael waondoke ntamshangaa sana.

Kwa sababu, akikubali kufanya nao kazi, anajiandaa ama kutokutumia phylosophy yake na hivyo anajiandaa kufail, ama kuitumia na hiyo phylosophy ifail. huwezi kufundisha assistant coaches phylosophy, ufundishe na wachezaji at the same time alafu upate result. sababu mkataba wa miezi sita ni short term project yenye clear target. either we want to be in top four OR we still want to win the league, etc. Now you can't achieve any of these big ambitions with such managerial terms.

Au Akina Michael waondoke, aje na kitchen cabinet yake, well, nao watapewa interim contracts? ikiisha wawe ma assistant consultant au? nao kwa sasa ni majobless? Yaani Manchester imekuwa desperate hata itoe kazi kwa majobless?

Tujiandae kwa cocha mpya kusign a three + years.
👏👏👏
 
Sikio la kufa halisikii dawa

Alisikika mlevi mmoja akilopoka maeneo ya kona bar
 
Historia ya ole united itakuwa fupi Sana ....


"Alikuja united akazurula zurula badae akafukuzwa "

Hana hata kikombe Wala sahani
 
I co-sign this. Phil Jones pia.

Hawa vilaza kama kuna timu watajipendekeza waende pia

Fred, Scott, Harry Maguire, Aaron Wan Bissaka, Marcus Rashford. Naamini ndani ya miaka miwili ya Ralf atakuwa kapunguza angalau watatu kati ya hawa.

Hapo kwa Marcus watu wengi watashangaa kidogo ila ukweli huyu mchezaji sioni aki-grow zaidi ya hapo. Nusu ya mshahara wake unaweza kutupa mchezaji mwenye uwezo mara 2 yake m.f Pedro Goncalves Pote.

Tunahitaji wachezaji walio na hadhi ya kuwa United, na sio tukicheza na vitimu kama Leicester au Everton huoni utofauti.
Kuuza Rashfood, kuiacha taka taka Martial, hayo ni matumizi mabaya ya fedha.

Martial anatakiwa afukuzwe, akigoma, piga risasi ya kichwa, tugombokane nae.
 
Hakuna picha hata moja kocha wenu akiwa ameshika kombe yaan anakuja kujifunzia man u kama ilivyokuwa kwa OLE na Arteta
Ndio mwalimu wa Klop na Tuchel sasa huyo

By the way Ragnick ana makombe 7 kwenye carrier yake

Na kufundisha timu kama Stuttgart, Hoffenheim, Leipzig sio rahisi kupata makombe huko, hata Pep angeenda kuwa kocha na msaidizi wake awe Klop na Tuchel awe kocha wa viungo wasingepata kombe hata la bata

Kama huamini muulize Klop aliyeishusha daraja Mainz na muulize Tuchel aliyekuwa na kombe 1 (German Cup, ambalo Ragnick kachukua pia) akiwa Dortimund

Makombe mengine Tuchel amechukua akiwa PSG ambapo ilimchukua Pochetino (kocha ambaye alikuwa hajawahi kubeba kombe) siku 6 tu kupata kombe lake la kwanza

Ragnick ni philosopher, trainer of the trainers and a coach of Manchester United.

Inauma but itabidi uzoee

Sent from my M2004J19C using JamiiForums mobile app
 
Hujui chochote kuhusu hii team wewe, ungekuwa unajielewa usingedhania kuwa Ronaldo pekee ndo alikuwa ni mzigo kwa OLE, yani hujaona upumbavu wa Maguire, AWB ,Mac Tominay, na mbinu hafifu za OLE ila umemuona Ronaldo tu.

Haya kama kweli unajilewa tuambie hapa, ni lini Fargie alimfokea OLE kwa kumpiga Ronaldo benchi? Wakati huo wewe ulikuwa wapi?
sikumbuki kama fergie alimfokea kwa maneno makali OGS kwa sababu ya kumweka nje Ronaldo bali hakufurahishwa moja kwa moja na kitendo chake cha kumuanzisha benchi.

Nakumbuka alikuwa anajibu swali la yule mpiganaji wa Russia anayeitwa Habib juu ya uamuzi wa Ole kutokuanza na Ronaldo dhidi ya Everton.

Yalikuwa ni mazungumzo ya kawaida tu kati ya watu wawili na bahati mbaya waandishi wa habari wakayatafsiri vibaya maoni ya ferguson,
ukijumlisha na matokeo mabaya ya ile mechi ndio ikawa habari ya mjini.

Hakumfokea kwa maneno makali
 
Hakuna picha hata moja kocha wenu akiwa ameshika kombe yaan anakuja kujifunzia man u kama ilivyokuwa kwa OLE na Arteta
Kama tungelikuwa na shida ya kocha mwenye CV nzuri ya makombe tungelimpa timu ernest valverde aliyeshinda mataji akiwa Barcelona lakini ndiye aliefeli interview hivyo akaondolewa kwenye list ya makocha wanaofikiriwa.

kinachotafutwa ni muelekeo mpya wa ujengwaji na uendeshwaji wa timu baada ya kufeli project ya Ole ilioaminiwa mpaka dakika ya mwisho na kupewa resources za kutosha ndio maana klabu imemuona Rangnick ni mtu sahihi wa kuanza naye kuliko hao wengineo(fonseca,garcia, n.K)

Hao wengineo wangelikuja na kuanzisha ideas zao zitakazodumu kwa muda mfupi then cycles ikarudi tena vile vile Kama ilivyo mwanzo.

Bodi ya klabu wamejifunza makosa kwa sasa wanaiangalia zaidi manchester ya mbeleni na si hii ya miezi 6, kama wewe na wenzako munaiangalia manchester united ya miezi 6 niwape pole na pia andaeni nguvu ya kicheko cha kutucheka na kutudhihaki kwa sababu upo uwezekano wa kumaliza tena msimu bila ya kombe tukiwa na rangnick lakini naamini atatuacha tukiwa sehemu nzuri sana.

si rahisi kuingiza philosophy mpya ya uchezaji na recruitments process ndani ya timu nzima kwa miezi 6 ndio maana hata klopp ikamchukua muda, bodi imekubaliana na mpango wake wa kumpa nafasi ya ushauri(wasiwasi wangu watampa hata timu) ili aendeleze hicho atakachokianza.

Chini ya project ya Ole tulikuwa tunakwenda kumsajili kieran trippier mwenye miaka 31 kwa paundi million 15 hadi 25 lakini imani yangu inaniambia usajili wa wachezaji aina ya trippier hautowezekana tena chini ya fikra na ushauri wa Rangnick.

Tutasajili wachezaji na kuajiri makocha kwa mujibu wa structure ya uchezaji wetu na si mafanikio yao kama tulivyofanya mwanzoni, Leo hii tuna wachezaji wanaofiti mfumo X na wengine hawafiti mfumo X kwa sababu ya sera mbovu.

Karibu rangnick
 
Ralf Rangnick wants Lars Kornetka as his Manchester United assistant manager, report Russian outlet Championat.

Rangnick said in a piece with the Coaches Voice that he made Kornetka the first video analyst in Germany in 2007 when he brought him to Hoffenheim.

Rangnick said: “He’s the best video analyst we have in Germany and my friend and colleague.”
 
When Rangnick left the Red Bull group last summer, the New York Times report he established his own consultancy firm, together with Kornetka.

That underlines the closeness of their relationship and Rangnick will need people close to him who he can trust who understand his methods if he is to succeed at United.
 
He had his first taste of life as an assistant manager when he joined Bayer Leverkusen ahead of the 2014/15 season.

That was the year after David Moyes’ United beat the Bundesliga outfit 5-0 on their own patch.

4) He also has experience as assistant manager at RB Leipzig and PSV Eindhoven.

mqdefault.jpg
 
Man U mmpata kocha. Sasa mnachotakiwa ni kumpa muda msianze kulalamika kila siku. Halafu pia akianza vizuri msipige sana mdomo kama kawaida yenu.

Jifunzeni kuwa na moderation wakuu. Kinachowaponzaga ni midomo. Kelele mingi sana.
Huu wa kwako utakua ni ushirikina, mdomo mchafu wa DAEMUSHIN aliyepo Makunduchi unachangiaje matokeo mabovu ya manchester united iliopo Ulaya.

Teh teh teh
 
Huu wa kwako utakua ni ushirikina, mdomo mchafu wa DAEMUSHIN aliyepo Makunduchi unachangiaje matokeo mabovu ya manchester united iliopo Ulaya.

Teh teh teh
Sijamaanisha hivyo mkuu. Naongelea kwanini huwa mnapata tabu sana mitaani na mitandaonu team yenu ikifanya vibaya. Nikwasababu mna kelele sana.
 
Tatizo la kushangilia timu za kurithi yaani babu yako alishabikia Manchester na wewe kijana wa miaka 23 unashabikia Manchester tutawatesa sana subil miaka 30 ijayo ndo mtachukua kikombe kingine cha ligi
 
Back
Top Bottom