Erik Ten Hag ni mzuri ila ufanisi wake upo nyuma ya Edwin Van Der Sar (Football Executive) na Marc Overmas (Director of football) ukimchukua pekee yake kwa mfumo wa timu yetu namuona akifeli vibaya sana ndani ya muda mfupi sana.
Huu ni wakati sahihi sana wa ile nafasi ya Ed kupewa mtu mwenye uzoefu wa kuendesha vilabu vyao soka as a football executive. Wasifanye kosa la kuleta kilaza kama Ed, niliwahi kuelezea impact ya kuwa na mtendaji mkuu mwenye kichwa kizuri.
Wamiliki wa Man City waliponunua timu wakamtafuta football executive toka Barcelona Ferran Sorriano kuwaendeshea timu. Mtu wa kwanza kuanza kumuajiri alikuwa ni football director kutoka Barcelona Aitor Txiki Birigistan moja kwa moja wakaanza kusuka upya scouting staffs globally na wengi wao walitoka Barcelona.
Ferran Sorriano aliwaambia mabosi wa City ndani ya miaka 5 ya uongozi wake atabeba makombe 5 na Club itapunguza 50% hasara inazotumia kujiendesha na kweli msimu wake wa kwanza alimuondoa Mancini akamleta Manuel Pellegrini kichwani walifahamu fika wanamtaka Pep Guardiola. Sisi tunakosa hii kitu watu wanaojua nini wanafanya. Ole anacheleweshwa kufukuzwa ni kwa sbb Ed na DoF wake hawana mtu kichwani kwako atayeendelezea project waliyoipanga muda mrefu.
Angalia takwimu za hawa football Executive wawili walioanza kazi pamoja ndani ya hii misimu 9, Ferran Sorriano vs Ed Woodward
Ferran Sorriano (Sept, 2012 - )
Premier League trophies: 4
FA: 1
EFL:4
Ed Woodward (July, 2013 - )
Premier League trophies: 0
FA: 1
EFL:1
UEFA Europa: 1