Kuna rafiki yangu mmoja mtaani aliwahi niambia kua timu yetu haiwezi kurudi tena kama zamani mpaka Ferguson afe.
Siku ile nilimuona kama karopoka tu kwakua yeye ni mshika manati.
Ila kwakweli naanza kuamini mdogo mdogo.
Hata uwepo wa Ole mpaka sasa pale OT unatokana na Ferguson, laiti angekua kocha ambae hayupo ndani ya mfuko wa suruali ya Ferguson saizi Ole tulisha msahau tangu tulipo donyolewa na kuku.
Kuku alitufanya kitu mbaya sana.
Kichapo kile kiliidhinisha kabisa kufukuzwa kwa Sorkjaer, lakini kwakua yuko ndani ya mfuko wa suruali ya babu mpaka leo tunaendelea kumuona akitamba.
TATIZO SIO WACHEZAJI, KOCHA, WALA UONGOZI, TATIZO NI ZIDUMU FIKRA ZA FERGUSON.